Wananchi walia njaa JWTZ kuchukua Ardhi yao, watishia kuandamana kwa Rais Samia

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wakazi zaidi ya 500 katika kata ya Moshono na Mlangarini Mkoani Arusha wametishia kuandamana kushinikiza serikali kuwalipa malipo yao zaidi ya bilioni 1, mara baada ya Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kuchukua maeneo yao kwa mabaliano ya kuwalipwa fidia ,lakini hadi sasa ni zaidi ya miezi 10 wamekosa mahala pa kuishi na kulima na wanateseka kwa njaa.

Aidha wananchi hao wameitaka serikali kuwapatia chakula cha kujikimu kwa kipindi hiki wakati wanasubiri malipo yao , kwani wamezuiwa kulima wala kufanya shughuli zozote za kuwaingizia kipato jambo linalowafanya wawe na maisha magumu ikiwemo kushindwa hata kupeleka watoto wao shule na baadhi yao wakifariki dunia.

Wakiongea mara baada ya kujikusanya kwenye ofisi ya mtendaji wa kata ya Moshono kujadili fidia ya maeneo yao,walisema kuwa serikali iliyataka maeneo yao kwa ajili ya matumizi ya jeshi hilo na kuwataka wananchi hao kupisha kwa makubaliano kuwa watalipwa fidia lakini wameshangaa serikali kukaa kimya na hawajui kinachoendelea

Mmoja ya wananchi hao Mosses Kivuyo alisema kuwa januari 30 mwaka huu walifika wataalamu wa Ardhi kutoka halmashauri ya Arusha DC jiji la Arusha ,wanajeshi na wawakilishi wa wananchi na kupima maeneo yao na baadaye kuyafanyia tathmini na kila mwananchi alijulishwa kiasi cha malipo ya ardhi yake.

"Baada ya kufanya tathimini wataalamu hao waliwajusha wananchi kuwa malipo yao yangefanyika kati ya mwezi Mei na June mwaka huu 2023 lakini hadi Leo Oktoba hakuna taarifa zozote juu ya malipo yetu na tunaishi kwa mateso makubwa"

Naye mkazi mwingine wa Moshono,Emmanuel Masamaki aliiomba Serikali kuwahudumia wananchi hao kwa kuwapatia chakula wakati wanasubiri malipo yao ambayo hadi sasa bado hayajajulikana watalipwa lini huku baadhi ya waathirika wakifariki dunia kwa maradhi bila kunufaika na malipo yao.

"Jeshi walitaka maeneo yetu kwa ajili ya shughuli zao, sisi hatukupinga tulikubaliana nao wakapima maeneo yetu toka januari mwaka huu na walituahidi ndani ya miezi miwili au mitatu tutalipwa na wakatuzuia kulima ,lakini chaajabu hadi Leo hawajatulipa chochote tunateseka na njaa na baadhi ya wenzetu wamekufa bila kufaidi malipo yao"

Masamaki aliiomba serikali kuharakisha malipo yao ili kuwapa fursa wananchi hao kutafuta maeneo mengine ya kilimo ili kunusuru familia zao na njaa.

Mwananchi mwingine ,Paulo Mollel mkazi wa Mlangarini,alisema mgogoro wao na JWTZ kambi ya Tanganyika pekasi Moshono,ulianza tangu mwaka 2012 wakitaka kutwaa maeneo yao lakini wananchi walipokubali maeneo yao kuchukuliwa kwa kuahidiwa kulipwa fidia ,hadi sasa hawajalipwa chochote.

"Mwaka 2012 jeshi walikuja kuorodhesha maeneo yetu na kuondoka baada ya miaka saba jeshi walikuja tena kutaka kutulipa fidia na baadhi yetu walikubali kulipwa na wengine wakikataa"

Alisema januari mwaka huu 2023 jeshi walifika tena kwenye makazi yao na kutaka maeneo mengine walifanya tathimini na baadaye mwezi wa tatu mwaka huu walirejea na kuwajukisha kiasi cha maliponkwa kila.mwanannchi mwenye eneo lakini hadi Leo hakuna malipo yoyote na wanazidi kuteseka.

Mwananchi huyo alimwomba waziri mwenye dhamana kufika na kuonana na wananchi ndani ya wiki moja kabla hawajafanya maandamano makubwa ya kumwona rais Samia Suluhu Hassan.

Akiongelea suala na wananchi hao Naibu kamishna wa Ardhi Mkoa wa Arusha,Jofrey Mwamsojo alisema anafahamu madai ya wananchi hao , hivyo aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa kuwasiliana na mamlaka za jeshi na serikali na kuahidi ndani ya siku kumi ataleta majibu kwa maandishi kupitia ofisi zao za kata.

"Ndugu zangu nimesikia kero ya wananchi na Jeshi , naomba nipewe muda niwasiliane na mamlaka za jeshi na ndani ya siku 10 nitaleta majibu rasimi kwa maandishi kupitia ofisi zenu za kata"

Alisisitiza kuwa suala la malipo yao lipo ngazi ya wizara ya fedha na hivyo ofisi yao itafuatilia kujua malipo yao yamefikia wapi na watawajulisha wananchi kupitia ofisi zao za kata.


Akiongea kwa njia ya simu mkuu wa kikosi cha 977 cha JWTZ Tanganyika Pekasi Kanali Hamis Kinguye aliwatoa hofu wananchi hao na kudai kuwa malipo yao yapo na yanashughulikiwa ngazi za juu .

"Hao wananchi waambie waondoe hofu serikali haimrushi mtu malipo yao yanashughulikiwa na hakuna haja ya kuandamana na muda wowote watajulishwa"

Alifafanua kuwa mara ya kwanza wananchi waliletewa malipo ila baadhi yao walikataa wakidai wamepunjwa ila tathimini zilifanyike tena na malipo yao watalipwa kama walivyokuwa wameahidiwa .

Ends ......








.
 
Watanzania ni viumbe wa mwisho katika huu uso wa dunia....Yaani ni watu wa kulalamika tu bila kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom