Hili la Ikulu linanitisha, sitaki kuamini!

Hili la Ikulu linanitisha, sitaki kuamini!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,026
Reaction score
20,511
Ikulu ni taasisi pana, yenye bendera na miiko yake, inakiongozi wake na watendakazi wake pia.

Mnadhimu mkuu wa Ikulu ambaye hutambuliwa kwa lugha ya mafumbo (shafron) kama AT2 ndiye kiongozi wa ikulu, Itifaki ya kirais ipo chini ya AT2 hata rais yupo chini yake. (kinadharia)

Katibu mkuu kiongozi ni sehemu ya wanaounda taasisi ya urais ndani ya Ikuli ambapo kwa sasa ni Bwana Sefue,

Pia yupo mkuu wa walinzi wote wa rais ambae kwasasa yupo kamanda Ben Mashaba,

Na pia yupo katibu muhitasi wa rais ama twaita mnikulu, ambapo kwa sasa yupo Bwana Gurumo.

Sasa kwa siku za karibuni kumeibuka kuvuja siri mhimu za rais (ikulu), jambo linalotia shaka sana ustahimilivu wa watumishi wetu hawa,

Kwanza ilianza kuvuja kwa "siri" za vikao vya siri vya Mheshiwa rais na wakala Zitto Kabwe,

Hili kwangu lilinipa hofu kubwa, kwamba kumbe unaweza kupeleka siri za nchi kwa rais na zikavuja kienyeji hivi??? Sasa sie wambeya tutapeleka wapi ili tuwe salama???

Lakini hilo likiwa halijapoa, wiki jana magazeti yameripoti mtumishi wa Hospitali ya KCMC amefukuzwa kazi kwakumpenyezea Rais taarifa nyeti zinazojiri hospitalini hapo,

Hakiki nimefadhaika sana sana, taasisi ya urais inawezaje kuvujisha taarifa za mawakala mhimu wa nchi ambao wanaripoti mojakwamoja kwa rais?? Je amevujisha rais mwenyewe au ni hawa watunza siri za urais?

Najihisi ni mkiwa ndani ya nchi yangu yenye mamlaka ya urais inayohatarisha maisha ya mawakala wake.

Vetting inazingatiwa vema kuwapata hawa watumishi wa rais?

Hali hii inanitisha na sitaki kuamini kabisa!!
 
Lakini taarifa za minungula mi mungu la ya escrow hazivuji
 
Mtumishi aliyefukuzwa alikua KCMC na sio Bugando mkuu... check taarifa zako
 
sahihisho! huyo mtumishi wa afya ni wa KCMC, alikuwa mhasibu. fanyia marekebisho hapo.
 
huu ni mwaka ambayo watanzania wanatakiwa kuwa makini sana na kila kinachosemwa na kuandikwa lakini wasitegemee raisi bora na mwadilifu kutoka ndani ya ccm tena kwani hakuna aliye msafi kwa sasa.
VOTE FOR UKAWA.
 
Akili za bavicha ni habari za kutazamia kabisa sijui ndiyo kimeandikwa nini.
 
Usiogope, muda uliobaki kwa ccm ni mdogo saana. Ufalme ukiisha fitinika, ni rahisi kuusukuma tu ka mlevi wa chang'aa ya mapapai
 
Umecopy vibaya,rekebisha hapo huyo mtumishi alikuwa mhasibu wa kcmc,ndio tatizo la kuongozwa na div 0
 
Aliyevujisha siri rais kapewa suti na saa nani?
 
Back
Top Bottom