Hili kabila litanikosesha mke

Hili kabila litanikosesha mke

Huo mkoa ndio no.1 kwa uwizi wa mfukoni cjui kuna chuo cha kuiba.....yani wao kwa ndole ni shida
 
Mkuu heshima kwanza,naomba sisi binadamu tuache kudhani au kuendekeza midomo ya wapumbavu,toka lini kabila fulani tu tukaliandama eti wao wanagawa hovyo miili yao?,kutaja Wahaya na kuwatwisha kashfa sio jambo jema,sababu hakuna kabila duniani ambalo halina vicheche,makabila yote duniani yana watu wa aina hiyo,ndio maana vitabu vitakatifu vimekemea uzinzi kwa mataifa yote duniani,na havikukemea uzinzi kwa Wahaya tu,tuache tabia hizo.
Umepanic mkuu huu mchezo hauitaji hasira
 
Hahahaaa inachekesha lakini ni kweli.

Humu ukitaja wewe ni Msukuma [watu wanahisi ni mimi]!

Ukitaja tu neno USA [watu wanahisi ni mimi]!

Kuna vijimambo kweli humu.

Acha ushamba basiiiiiii STATES wala hakuna deal kama unavyopa promote ZOEA BASI
 
Maelezo yako Ndugu yanachekesha yanafurahisha kama utayasoma kwakujiachia.
. Lakin kama yéyé anaupndo nawewe' muoe chamuhim co Kabila jiulize tu yéyé anakupenda kwel?
 
Mbona hata Kabila lako mwenyewe la Kisukuma ni full " matatizo? " Mmeacha ile tabia yenu ya kula kula hovyo pindi muwapo safarini? Ubungo asubuhi mnanunua miwa mnaanza kututafunia ndani ya basi, tukifika mizani mnatafuta mayai ya kuchemsha ili mtujambie vizuri mbele ya safari na hakika huwa tunawakoma, tukifika chalinze lazima mnunue mahindi ya kuchemsha, Msamvu Morogoro mnatafuta mihogo ya kuchemsha, Gairo lazima mnunue viazi vya kuchemsha pale, Dodoma huwa mnatugandisha mno kwani wengi wenu hukimbilia vyooni " kufyatua " mlivyovifakamia katika vituo tulivyovipita, maeneo ya Shelui mtanunua Chips yai na kuku za kuletewa dirishani ambazo hata hivyo nyingi huwapeni sana usumbufu wa matumbo na tukiwa tunataka kuliacha pori la maeneo hayo huwa mnamsimamisha dereva huku mnakimbilia maporini kujisaidia, Singida lazima tu mtaulizia Ugali na wengi wenu ili msichelewe katika basi huwa mnabeba kabisa huo Ugali na mkipanda nao ndani ya basi huwa mnatupa " show " ya bure hasa kwa jinsi mnavyochota na kuutafuna huo Ugali kwani huwa mnatumia sana nguvu utadhani mnaua nyoka, Shinyanga na penyewe mtatafuta vitumbua na hadi tunafika Mwanza pale Kituoni hakika matumbo yenu Wasukuma huwa yanakuwa yamechafuka mno.
Polepole mkuu. Utatuua Wasukuma uwiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Back
Top Bottom