Mbona hata Kabila lako mwenyewe la Kisukuma ni full " matatizo? " Mmeacha ile tabia yenu ya kula kula hovyo pindi muwapo safarini? Ubungo asubuhi mnanunua miwa mnaanza kututafunia ndani ya basi, tukifika mizani mnatafuta mayai ya kuchemsha ili mtujambie vizuri mbele ya safari na hakika huwa tunawakoma, tukifika chalinze lazima mnunue mahindi ya kuchemsha, Msamvu Morogoro mnatafuta mihogo ya kuchemsha, Gairo lazima mnunue viazi vya kuchemsha pale, Dodoma huwa mnatugandisha mno kwani wengi wenu hukimbilia vyooni " kufyatua " mlivyovifakamia katika vituo tulivyovipita, maeneo ya Shelui mtanunua Chips yai na kuku za kuletewa dirishani ambazo hata hivyo nyingi huwapeni sana usumbufu wa matumbo na tukiwa tunataka kuliacha pori la maeneo hayo huwa mnamsimamisha dereva huku mnakimbilia maporini kujisaidia, Singida lazima tu mtaulizia Ugali na wengi wenu ili msichelewe katika basi huwa mnabeba kabisa huo Ugali na mkipanda nao ndani ya basi huwa mnatupa " show " ya bure hasa kwa jinsi mnavyochota na kuutafuna huo Ugali kwani huwa mnatumia sana nguvu utadhani mnaua nyoka, Shinyanga na penyewe mtatafuta vitumbua na hadi tunafika Mwanza pale Kituoni hakika matumbo yenu Wasukuma huwa yanakuwa yamechafuka mno.