Hili jambo limeniumiza sana

Pole sana kwa hayo yaliyokukuta.

Uliaji wa hivi upo.

Na nijuavyo mimi mara nyingi Mtoto akitangulia kabla ya Mzazi (Mama), waMama wengi wakilia utawasikia "kwanini nisingekufa Mimi abaki Mtoto wangu".

"Kwanini umeniacha".

Ila kwa hii yako, kwa kweli ni ngeni na inasikitisha sana
Inaumiza sana
 
Pole sana mkuu, msamehe halafu nenda zako mbali. Mama yangu anatabia za upendeleo na ubaguzi mi ananifanya kama ATM tu lakini mapenzi yake ya dhati ni kwa mdogo wangu ila Mungu kamcheka kipenzi chake hali ni ngumu. Hawezi ongea madhaifu yake kwangu ila yangu watakaa wanitete uzuri mdogo wangu ananiambia kila kitu.
Mara zingine huwa namwambia ukweli kuwa anaupendeleo ila nishamzoea namchukulia poa tu na anakili na kuniomba msamaha eti hajui kwa nini inakuwa hivyo huenda kwa kuwa alinizaa angali mdogo na hatufanani nae mi kwa kujua hilo nimeamua kuishi mbali nae tukutane Mara chache nikijaliwa chochote namtumia akiniomba nikiwa sina anachukia ili hali mwanae kipenzi hampi.
Ndo hivyo mkuu, Mzazi hakosei chukulia poa tu ila nahisi kama watoto wa kwanza wengi hawana nafasi ya kupendwa kwa wazazi nimeona kwa watu kadhaa.
Pole jamani nawe na ahsante sana
 
Sio ww tu hayo yapo sana ,hata mm iko shida kama hiyo imefikia hata watoto wangu kwenda kwa jibu yao hapana kwa yale waliyoyapata,unaweza kuwa na mapenzi au upendo mkubwa kwa mama ako lkn kumbe yeye yuko mbali na ww kabisa ukiitafuta sababu wala huipati na hiyo sababu ya mpenzi wako inaweza kuwa wala c sababu ila hayo huwepo tu ikifikia mama kutoa machozi na kuomba hayo bora yangekutokea ww,kuwa makini sana huwa kuna roho ya ajabu ya chuki vitabu viko wazi kuna maagano hapo au kulikuwa na aina furani ya urafiki kati ya mama na mwana ambayo mwezio aliyaona na kisha kuyatunza hata ww hukuyajua kwa hiyo alipendwa kwa usiri huo lkn yawezekana mama yako aliiona akili yako haiendani na yale mwenzio aliyapokea.mpende mama yako lkn kuwa makini sana na mama yako kikubwa ni kumuombea sana ili huyo pepo mchafu atoke yangu ni hayo,hapo kwa wengi sana Dada.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitazingatia sana ushauri nashukuru
 
Baadhi ya wazazi huwa na tabia yakuchagua watoto wala usiogope.

Mimi mama yangu alikuwa hivyo tena zaidi ya huyo wako ila alikuwa ananituma kazi zote namka saa kumi na mbili asubuhi nafudi saa moja kutoka shamba kwa siku ambazo siendi shule. Hili lilinifundisha kazi zote.

Cha kushangaza shuleni huko nlikuwa napendwa sana kuwa najituma na tabia njema home mama anasema ni 'bure kabisa' ila sasa mimi ndo nimefanikiwa kiuchumi&kielimu kuliko wote (labda wajitahidi baadae) Niliwajengea nyumba nzuri 3 rooms store, jiko lakini hakuna aliyewahi kusema asante mwanangu. Sasa hivi anatamani sijui anionyeshe upendo gani kuyafuta hayo ila haiwezekani maana pamoja na yote niliwapenda wazazi wangu nilimsaidia kusomesha watoto 2 secondary na sikai miezi 2 sijawatumia mazagazaga kiukweli hili linamfanya ajutie sana.

Nimeamua kushare this personal issue ili urelax wala usijali huwa hawajielewi baadae wanajuta sana.
Umenifanya niwe na amani kwamba pengine ni kawaida ya baadhi ya wazazi
 
Mama ni mama mkuu wengne hatujamwona mama since tupo vichanga mshukuru Mungu kwa kila jambo na msamehe mama yako kwani atabaki kuwa mama yako tu no way... Ningekua nae hata wa hvo ningefrah sana R.I.P ma lovely Mom...[HASHTAG]#Deis[/HASHTAG]
Pole sana muombee aendelee kupumzika kwa amani
 
Pole sana kumbuka kua huyo ni Mama na kama amekuja kuomba msamaha niwajibu wako kumsamehe,sisemi rahisi ila Mama daraja lake ni kubwa sanaaa, kufiwa sio kitu kidogo na labda utakuja kumuelewa utakapo kua Mama.
tafuta mda kaa nae chini huyo ni mzazi wako muombe msamaha hata kama kosa hulijui na muombe akueleze kama kuna kosa ulifanya uenda umelifanya bila kujua ili usije ukalirudia tena, mimi wakati mamangu anaumwa sanaaa na nampenda sanaa mama yangu nilimwambia Mama kama Nakupenda sana na kama mwenyezi mungu angeweza kunipa nafasi basi ningemtoa mtoto wangu ukabaki wewe na kumbuka hapo nilikua na mtoto mmoja tuu.
rudi kwa mzazi wako pepo yako iko kwake na furaha yako pia iko kwake hata kama mkorofi au vyovyote atakavyo kua still ndio mama mwenyezi mungu alie kupa,futa machozi nenda kaonge nae ukiweza lia usibane kilio chako toa joto lako la rohoni mweleze mama unajisikiyaje na vipi unapenda muishi sababu mmebakia nyie tuu wawili na Inshallah mwenyezi mungu atakulinda na kuwaweka salama kwa amani na Upendo.
Shukrani dada kwa ushauri mzuri msamaha ni jambo ambalo napaswa kulitenda.
 
Msamehe tu kwa sababu ni mama yako, na atabakia kuwa mama yako. Mkasa wa kwako ni miongoni mwa mikasa amabayo imewapata watu wengi, pengine mikubwa kuyliko wa kwako. Songa mbele na maisha yako, mheshimu, akiwa na shida msaidie, na unapomsaidia usimsimange kwa kukumbushia maneno aliyokuwa akiyatamka msibani.... Mungu ndiye atamhukumu
Shukrani mkuu
 
Habari zenu jamani


Katika familia yangu tumezaliwa wawili Mimi nikiwa ndiye mtoto wa kwanza alafu akafwata midogo wangu ambaye tayari ni marehemu mwezi sasa umepita.....nimebaki Mimi na mama yangu baba alishafariki miaka imepita.

Kabla ya mdogo wangu kufariki alikuwa ni kipenzi cha mama sana hilo halikuwa linanisumbua niliona kawaida sana pia hiyo ilitokana na mahusiano ya mpenzi niliekuwa nae mama hakumpenda sana jambo hilo lilifanya Mimi na mama yangu tusiwe na maelewano.
Kitu kilichokuja kuniumiza na nimuone mama tofauti ni siku mdogo wangu alipofariki mama alikuwa akilia wa nguvu na huku akilitaja jina la mdogo wangu na Mimi.......nanukuu( BORA USINGEONDOKA WW KIPENZI CHANGU ANGEONDOKA DADA YAKO (yani mimi)INGEKUWA AFADHARI.
Maneno hayo halikuwa akiyarudia kuanzia mwanzo wa msiba mpaka anazikwa jambo hili liliwashangaza wengi na liliniumiza sana mpaka Leo nikikumbuka Yale roho inaniuma sana nashindwa hata kumuangalia mama yangu naishia kulia.
Pengine nimemkosea mama yangu sana lkn sikutegemea kama anaweza kuombea Mimi kufa imeniumiza sana.
Amekuja leo na baadh ya ndugu akiomba msamaha sijasema chochote nimeishia kulia.nataman niende mbali kwasababu nimejua Mimi si chochote kwake.





Mwenye ushauri au mawazo yoyote kisaikolojia siko sawa.

Ndio mama inabidi uende naye taratibu atajifahamu
 
MI NAE ANGEKUFA KAMA ALIVOKUFA BABANGU!

mambo ya mama ni mungu wa pili asee hapana!
MAMA NI MAMA!
MUNGU NI MUNGU !
MAMA ALIUMBWA NA MUNGU KAMA ALIVONIUMBA MIMI!
kama sina maisha kwenye maisha yake,
she wont have in mine!
HIIIIIIIVYO TU YANI!
 
Back
Top Bottom