Pole sana kumbuka kua huyo ni Mama na kama amekuja kuomba msamaha niwajibu wako kumsamehe,sisemi rahisi ila Mama daraja lake ni kubwa sanaaa, kufiwa sio kitu kidogo na labda utakuja kumuelewa utakapo kua Mama.
tafuta mda kaa nae chini huyo ni mzazi wako muombe msamaha hata kama kosa hulijui na muombe akueleze kama kuna kosa ulifanya uenda umelifanya bila kujua ili usije ukalirudia tena, mimi wakati mamangu anaumwa sanaaa na nampenda sanaa mama yangu nilimwambia Mama kama Nakupenda sana na kama mwenyezi mungu angeweza kunipa nafasi basi ningemtoa mtoto wangu ukabaki wewe na kumbuka hapo nilikua na mtoto mmoja tuu.
rudi kwa mzazi wako pepo yako iko kwake na furaha yako pia iko kwake hata kama mkorofi au vyovyote atakavyo kua still ndio mama mwenyezi mungu alie kupa,futa machozi nenda kaonge nae ukiweza lia usibane kilio chako toa joto lako la rohoni mweleze mama unajisikiyaje na vipi unapenda muishi sababu mmebakia nyie tuu wawili na Inshallah mwenyezi mungu atakulinda na kuwaweka salama kwa amani na Upendo.