Hili jambo limeniumiza sana

Ila nimefikilia nimeona hakuna haja ya msamaha maana mtu kukupenda au kuto kukupenda ni chaguo la moyo wake sio makosa kwahiyo huyo mama hampendi mwanae
Hamna haja ya kuumia huwezi kulazimisha mtu akupende
Chakufanya ni kupotezea na kuendelea na maisha ya kawaida
AHSANTE KWA KUNIELEWA MWAYA!
uliniuliza swali tricky kidogo,nikajiukta nimelijibu kwa maelezo!
lakini na mi nilijiuliza same question!
AKIMSAMEHE MAMA ANAYETAMANI AFE,ITAONGEZA AU KUPUNGUZA LOLOTE KWENYE MAISHA YA HUYO MAMA ,NIKAJIPA JIBU HAPANA!
so KWANINI AJIPE KAZI KUBWA YA KUSAMEHE KITU KAMA HICHO ,WHILE IT WONT EVEN WORTH A THING!

akhu mwaya!
moyo wangu sultani mie!
naweza sawa
siwezi akhaaaa!
 
Mama ni Mungu wa Pili katika dunia hii. Hakuna kitu kibaya kama kumchukia Mama. Unachopaswa kufahamu kuwa hakuna mwanadanu aliyekamilika. Hivyo uambie moyo wako kuwa huyu ni mama yangu na vyovyote itakavyokuwa atabaki kuwa mama yangu. The rest mwachie Mungu. Hata kama utaamua kumchukia haitasaidia. Nakusihi mlipe kwa wema hadi ajue kama wewe unampenda hata kama yeye hakupendi. Ukifanya hivyo Mungu ipo siku atakufanyia wepesi katika mambo yako na familia yako kwa ujumla.

Wahenga walisema: mpe mchawi akulelee mwanao...

Joseverest samahani kwa kuchukua kiti chako.
Waooo, A strong Strong Neno...
 
Wala usiende mbali, kama vile ambavyo Mungu amemuondoa aliyempenda ndivyo atakavyomuondoa hata yeye mapema kabla yako. Ila usimnenee mabaya. Lakini usikome ktk sala na maombi ukitamka yakuwa kimbilio lako li kwa Bwana Mungu wa majeshi.

Lkn tazama, kabla hajafa atakuomba radhi mara kadhaa huku akilia na kugalagala, nawe usisite kumsamehe maana visasi si vyako wewe bali Bwana Mungu wa Majeshi. Lishike sana neno hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, Mungu akutie nguvu upate kumsamehe mamaako. Naamini wewe ni muhimu sana kwake na kina siku atakuhitaji sana. Hivyo msamehe bure kwa kuheshimu kitendo cha kukuzaa .
 
Pole sana, Ila naamini Mungu anatujua zaidi tujijuavyo sisi. Yawezekana hata hicho kifo, Mungu ameruhusu kitokeea ili Kudhihirisha tabia ya huyo mama yako, juu yako. Mungu ametaka kumwonesha Mama yako kuwa nawe unastahili kupendwa na kuthaminiwa.
Pole sana ndugu yangu, msikilize huo msamaha wake Ila msamehe pale tu utakapokuwa tayari kumsamehe.
Kusamehe jambo hakulazimishwi, Bali hutokea pale tu Moyo unapokuwa tayari kufanya hivyo.

Hata sijui alikuwa anaweza nini huyo Mama yako. Wengine wanalilia kuwa na watoto wengine wanawabagua watoto wao waziwazi kha!!.
Pole sana.
 
Pole mkuu!,,, mi ilishantokea kutokupendwa na baba yangu, hadi siku naomba hela ya kulipia mtihani wa mwisho form four mzee alininyima si kwamba hana alikuwa nayo ila hakuniona km nastahili kupewa..aliniambia hivi

" WANGAPI WANAKULA NG'OMBE MZIMA WANASHINDWA MKIA? Shule ni kitu gani bhnaa rudi kaaa nyumbani" huwa siyasahau kabisa ila NILISAMEHE MNO nakuomba baraka zishuke juu yangu na uzao wangu hadi Leo Nina furaha teleeee!

Samehe Mara nyingi uwezavyo ili uishi miaka mingi duniani na upate heri uiachapo dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wala usiende mbali, kama vile ambavyo Mungu amemuondoa aliyempenda ndivyo atakavyomuondoa hata yeye mapema kabla yako. Ila usimnenee mabaya. Lakini usikome ktk sala na maombi ukitamka yakuwa kimbilio lako li kwa Bwana Mungu wa majeshi.

Lkn tazama, kabla hajafa atakuomba radhi mara kadhaa huku akilia na kugalagala, nawe usisite kumsamehe maana visasi si vyako wewe bali Bwana Mungu wa Majeshi. Lishike sana neno hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani ubarikiwe
 
Pole sana, Ila naamini Mungu anatujua zaidi tujijuavyo sisi. Yawezekana hata hicho kifo, Mungu ameruhusu kitokeea ili Kudhihirisha tabia ya huyo mama yako, juu yako. Mungu ametaka kumwonesha Mama yako kuwa nawe unastahili kupendwa na kuthaminiwa.
Pole sana ndugu yangu, msikilize huo msamaha wake Ila msamehe pale tu utakapokuwa tayari kumsamehe.
Kusamehe jambo hakulazimishwi, Bali hutokea pale tu Moyo unapokuwa tayari kufanya hivyo.

Hata sijui alikuwa anaweza nini huyo Mama yako. Wengine wanalilia kuwa na watoto wengine wanawabagua watoto wao waziwazi kha!!.
Pole sana.
Nashukuru sana kwa maneno yako
 
Pole mkuu!,,, mi ilishantokea kutokupendwa na baba yangu, hadi siku naomba hela ya kulipia mtihani wa mwisho form four mzee alininyima si kwamba hana alikuwa nayo ila hakuniona km nastahili kupewa..aliniambia hivi

" WANGAPI WANAKULA NG'OMBE MZIMA WANASHINDWA MKIA? Shule ni kitu gani bhnaa rudi kaaa nyumbani" huwa siyasahau kabisa ila NILISAMEHE MNO nakuomba baraka zishuke juu yangu na uzao wangu hadi Leo Nina furaha teleeee!

Samehe Mara nyingi uwezavyo ili uishi miaka mingi duniani na upate heri uiachapo dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
Ongera sana kwa moyo wa kijasiri
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom