Hili jambo la leo limenitoa machozi kwa kweli

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Askari wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu. Hawa traffic. Jua yeye, mvua yeye. Hivi watanzania kwa nini hatuna huruma?

Nimekuta jamaa mmoja amekamatwa na traffic sababu tairi zake zimechakaa. Kiukweli huyu jamaa alipaswa ampe traffic hata 200,000 ya asante kwa kugundua hilo tatizo la kuhatarisha maisha yake dereva.

Kilichoniliza ni kuona jamaa anabembeleza asamehewe? My gosh, hii imenishtua sana. Yaani traffic kakukamata unahatarisha maisha yako na ya wengine, badala umshukuru unataka hata ya fine kumnyima? Tuwe na ubinadamu.

Traffic wa namna hii unapaswa kwanza ulipe faini kama ilivyo halafu na yeye unampa angalau 200,000. Kama asante kwa kuokoa maisha yako.

Huyo jamaa ilibidi niangalie nyuma kama anatumia gari au usafiri. Nikaona hicho chombo kimeandikwa Rav 4. Nilimuonea huruma sababu tairi zake ni kipara. Akasema tairi za gari zangu haziwezi funga mwenye huo usafiri wake. Niliumia sana.

Nikamuuliza kama tairi za Ford Ranger zinaweza fungwa pale au Range Rover ili niende naye home nikampe. Mimi tairi zangu huwa kila miezi 8 nabadilisha.

Jamaa zangu wengi wakija wanazichukua wanadai ni mpya kabisa. Wao wanaenda tumia miaka 2 zaidi.

Basi nilimwambia tu jamaa awe responsible alipe faini na pia aoneshe uungwana, ampe traffic hata Tsh 100,000 kama asante ikiwa hana 200,000.

Tujifunze ku appreciate wanapofanya vizuri. Upo vibaya sana mwachie hata 100,000. Naye aone unamjali na kutambua uwepo wake. Ma ukiwa na kosa lipa tu ndugu yangu ukiweza hata unalipa in advance. Nilijikuta tu natokwa na machozi.
 
Umpe traffic police laki moja.Kwani huyo hakagui gari kabla ya kuendesha?
 
Back
Top Bottom