Samia, kiutendaji amemwacha mbali sana Magufuli. Magufuli alikuwa na speed kubwa katika propaganda, na siyo katila utendaji. Mimi siyo shabiki wa Samia, lakini ukimlinganisha Samia na Magufuli, Samia pamoja na mapungufu yake, atakuwa malaika
Kitu gani Magufuli ilisema kitakamilika wakati fulani halafu kikamilika wakati uliotajwa?
Speed kubwa ya Magufuli ilikuwa katika kudidimiza uhuru wa watu, demokrasia, haki za watu, kukanyaga sheria na katiba, na kudidimiza uchumi.
Wakati wa Kikwete uchumi ulikuwa unakua kwa 7%, Magufuli aliuporomosha mpaka 1.9% (taarifa ya WB), uwekezaji mwaka 2015 ulikuwa unakua kwa 28%, Magufuli aliuangusha mpaka 4%. Utalii mwaka 2015 ulikuwa unakua kwa 15%, mpaka 2019, Magufuli alikuwa ameuangusha mpaka 3.6%. Kwa takwimu hizi, Magufuli alikuwa anaenda spidi kali katika kuangamiza Taifa.
Kitu pekee alichofanikiwa Magufuli kuliko watangulizi waje ni siasa za ulaghai. Na wajinga aliwapata sana, hata wengine kufikiria kuwa alikuwa anafanya mambo makubwa sana kuliko watangulizi wake. Kwa kweli wajinga aliwaokota hasa, lakini wenye akili wanajua kuwa Magufuli alikuwa janga kwa Taifa. Hakuistahili ile nafasi.
Jbo jingine, ni kwamba marehemu Magufuli anasemwa sana sasa kwa sababu moja kubwa, alikuwa dikteta aliyewanyima watu haki ya kusema. Nani angemkosoa Magufuli wakati akiwa hai, halafu angebaki salama? Tazama alichofanyiwa Lisu. Yuko wapi Ben Saalnane aliekosoa PhD ya Magufuli?
Usizungumze kama vile umeshuka leo toka ahera. Ka ulikuwepo nchini wajati wa Magufuli, huwezi kushangaa kwa nini watu wanasema leo, na siyo wajati wa uhai wake.