Kwanini tukio liwe karibu na Ubalozi wa Ufaransa?

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,076
3,797
Inasemekana jamaa alishuswa na bodaboda na akaenda kwenye kibanda cha askari pale kwenye makutano kama vile ana shida.

Akachomoa bastola na kuwauwa askari wawili, askari mmoja akapigwa risasi kwenye bega.

Akachukua silaha za wale askari akawa anatesa nazo.

Lakini kwanini iwe maeneo yale? Alikuwa mgeni mjini?

1. Nyumba ya balozi wa uingereza ipo kama mita hamsini kutoka kwenye sehemu ya tukio ambapo askari walipigwa risasi na kuna ulinzi wa askari wenye silaha.

2. Bank ya Stanbic ipo jirani na kawaida wanakuwepo askari wenye silaha za moto.

3. Ubalozi wa ufaransa upo maeneo yale yale ambapo kuna askari wenye silaha.

Lakini pia tukumbuke kuna msafara uliyokuwa unakaribia kupita ile barabara. Ulikuwa ni msafara wa nani?

Sheria ya ulinzi hairuhusu askari kuacha lindo na kwenda sehemu nyingine, isipokuwa pawe na genuine reason.

Kwanini walichagua hilo eneo?

UPDATES:

Askari polisi watatu ndiyo waliyopigwa risasi na yule gaidi kutumia pistol.

Mlinzi wa SGS pia amefariki, na takriban raia sita wamejeruhiwa.
 
Ukiangalia video ile vizuri inaishiria kwamba jamaa alikua na tatizo la akili, yule sii gaidi hamna gaidi wa namna hiyo, angekua gaidi zaidi ya police 10 wangekufa pale kwanza hawana shabaha mtu iko kati kati ya barabara peke yake bila kizuizi chochote wanapiga lisasi zaidi ya 20 na mnamkosa askari zaidi ya 30.
 
Mmh kumbe Siku hizi kumeendelea adi wenye matatizo ya akili wanajua kutumia siraha teh teh teh
 
Tatizo mishahara midogo ya polis na njaa zinawafanya wawe na stress za maishaaa mwambie mama Samia awaongezee pesa, polisi wengi njaa wamekonda na wamepauka midomo.
 
Kuna mtu anatafutwa appa wa kupewa kessi ya ugaidi muda utaongea tusubili upelelezi wa kinafki

2897435_IMG-20210825-WA0023.jpg
 
Mmh kumbe Siku hizi kumeendelea adi wenye matatizo ya akili wanajua kutumia siraha teh teh teh
Kila kicha anafani yake wengine wanawokota makopo wengine wanarusha mawe, wengine wanaigiza kama wanavyo ona kwenye filamu au vitani, kwa hiyo ni rahisi sanaa, kawa na stress/trauma/ mental case za kivita kama Somalia, na akatekeleza, sio mistake yule alikua mentally disturbed cause ndo haijulikane
 
Ukiangalia video ile vizuri inaishiria kwamba jamaa alikua na tatizo la akili, yule sii gaidi hamna gaidi wa namna hiyo, angekua gaidi zaidi ya police 10 wangekufa pale kwanza hawana shabaha mtu iko kati kati ya barabara peke yake bila kizuizi chochote wanapiga lisasi zaidi ya 20 na mnamkosa askari zaidi ya 30.
Mimi naamini nigaidi. Na kama alikuwa hana akili nzuri, sidhani kama ile timing ya kuwauwa askari kwa pistol na kuchukua silaha zao ingefanikiwa.

Kuna tetesi askari mmoja wapo alikuwa anakimbia kuelekea baharini na jamaa akampiga risasi.

Jamaa ana akili timamu kabisa, kwa sababu hakutaka kuwauwa raia kabisa, yeye ilikuwa ni polisi.
 
Akili za kupiga risasi na kujua silaha alikua nazo ila wengi watu wa aina yake wanapata vichaa kutokana na trauma za vitaa, wanashindwa ku balance akili zao na wanakua na chuki na police.
 
Kama Taifa bado tuna safari ndefu sana kuhusu tahadhari na utayari kwa suala zima la usalama. Mara nyingi nimekuwa najaribu kudadisi madhaifu ya polisi wetu ila nimegundua kitu kimoja kuwa WAMEBWETEKA sana.
Umeongea ukweli na kwa uchungu sana.

Ni kweli baadhi ya watu wanaajiriwa kwa MEMO na kwa sababu wana ndugu zao wenye vyeo bila kuwa na moyo wa ndani wa utumishi.

Lakini nadhani kwenye hii issue, hata kama una moyo wa utumishi namna gani uvamizi waliyofanyiwa hawa askari ungempata askari yeyote yule.
 
Akili za kupiga risasi na kujua silaha alikua nazo ila wengi watu wa aina yake wanapata vichaa kutokana na trauma za vitaa, wanashindwa ku balance akili zao na wanakua na chuki na police.
Hii ni mental case. Psychoanalyst akiwekeza muda akafanya tracing ya maisha yake atapata majibu sahihi.

Tatizo letu sisi wabongo tunachukulia mambo simpo simpo sana. Mbele huko wapo tayari ku-uncover kila detail za mhalifu ili kupata ujuzi wa kudhibiti mambo yanayofanana yanayoweza kutokea siku zijazo.

Asilimia 90 ya matukio ya kihalifu na hata ugaidi yangeweza kuzuilika kama binadamu tungekuwa na umakini wa kujiuliza maswali ya ziada.
 
Back
Top Bottom