Menemene tekeli na peresi.
Haya maneno kwa Mara ya kwanza yaliandikwa kwa mkono Wa MTU asiyeonekana yakimuonya mfalme Nebukadreza aliyekua jeuri na kiburi kuliko kawaida hata alidiriki kuwataka watu wamuabudu.
Maneno haya yalimaanisha ufalme unaanguka na kusambaratika.
Kiburi siku zote huleta kujiamini kupita kiasi, huleta ugumu Wa moyo, huleta majivuno, pia kiburi kinasababisha mtu asisikilize mausia na aone yeye tu ndo anayejua kuliko wengine wote, pia kiburi humwaminisha mtu kuwa yuko salama hata anapoingia shimoni.
CCM na mfumo wake wote imefikia wakati wa "menemenetekeli na peresi" na ndio maana hawaoni kwamba, watanzania hawahawa waliowaita kichwa cha mwendawazimu leo wanadhubutu kuwakosoa wanapofanya uovu.
Mwendawazimu ni mtu ambaye kila kitu kwake ni sawa, hana baya wala jema, hana furaha wala huzuni, lakini sio Tanzania ya Leo. Tanzania ya Leo watu wanajua majira na nyakati, ila CCM bado hawalijui hilo japo wanaamini wao ni werevu kuliko wenzao wote.
Wanaendesha nchi kama wanaendesha familia, baba akiamua kuwacharaza watoto bakora wawe wamekosa ama la, ili mradi kiu yakeyake ni kuwachapa basi, lazima wale bakora.
Nchi sio familia kuongoza nchi kunahitaji akili na na maarifa, unaendesha watu ambao wengine wamekuzidi upeo na ufahamu, unapa swa kukubali kukosolewa,kuonywa, na kurekebishwa lakini ukiwa na kiburi huwezi kukubali, na ukikataa maonyo na marekebisho anguko lako litakuja gafla.
Kwasababu ya kiburi, dharau, jeuri, majivuno, majigambo, usanii,uongo, ukaidi na ubabe, CCM itaanguka anguko LA aibu na haitarudi tena.
Itasambaratika ili neno "menemene tekelinaperesi" litimie. Watch and see.
Kwa sababu ya kiburi watakuja hapa na kuanza kukufuru tena.