Hiki ndicho kitakachoiangusha CCM 2020

CCM itapata wakati mgumu sana Uchaguzi 2020.
1.Matajiri ambao taabia zao ni kutengeneza faida ,wamebanwa mpaka hawapumui,watamwaga pesa Upinzani ili waweke mtu wanaemtaka ili kutafuta nafuu.

2. Wasaliti waliopo ndani ya CCM ni wengi kuliko hata wapiga kura wa Upinzani,awali watu waliokuwa CCM walikuwa wanapata kinga ya kufanya mambo yao,Iwe Ujambazi,kukwepa kodi,biashara haramu nk. Sasa hivi Wote ni wahanga na wanaisoma namba,hakuna tena vile viposhoposho vya vikao,wanapoga kelele kuliko hata waponzani wanavyopoga kelele.

Hawa ni wale CCM maslahi aliosema Mzee Warioba ambao kimsingi ni wengi ndani ya CCM kuliko hata CCM asilia,hapo watapiga kura za hasira kwakuwa watakuwa hawana chakupoteza.

3.Vyombo vya habari navyo sasa hivi vinaogopa kupigwa pini kwakuwa Siri Kali ipo kazini,haina ubabaishaji,ukifika mwaka wa kampeni Mabilionia ambao ni jamaa zao na wale waliopo Segerea watamwaga pesa kwa waandishi na wamiliki,vitafukuliwa vitu na kwakuwa watanzania ni wazee wa kushangilia na kwenda na upepo,basi watasahau utumbuaji wote unaofanyika.

4. Watumishi wa Umma ambao wao huaminiws sana na wananchi hasa wa vijijini katika kutoa mwelekeo wa yupi wa kuchaguliwa,hili kundi lina manung'uniko makubwa lkn hawana chaguo lingine zaidi ya kuvumilia ,kundi hili ndilo linalosimamia chaguzi zetu na huenda ikatumika hasira za maisha magumu kuiondoa CCM madarakani (ingawa mshahara utaongezwa 2019 )ili kuwasahaulisha.

5.Bomoabomoa,hii itawatesa sana CCM 2020,maelfu ya wananchi wakiwemo wana ccm tena viongozi waandamizi nao wamekumbwa na kadhia hii,wamejaribu kutumia vyeo vyao kama zamani walau kulainisha mambo lkn wapi.Mamlaka zinasisitiza kuwa Bomoabomoa ipo palepale,sasa hawa wanaenda kutumbukia kwenye wimbi la umaskini na kukosa makazi kwa maelfu ya wana wananchi hasa wana CCM.

6.Tumbuatumbua ya viongozi waandamizi serikalini,wale jamaa huenda mpaka sasa wan chama cha siasa walichojipanga kukiunga mkono,Orodha yao ni ndefu sana lakini ni watu wenye kipato,Elimu na wenye ushawishi kwa jamii,kubwa zaidi watu wanaojua mambo mengi yanavyofanyika,hawa wanaweza kukiangusha chama cha mapinduzi ifikapo 2020.

7.Uelewa wa wananchi,wananchi wengi wanaamini Mabadiliko hufanyika ghafla hasa yale ya Kiuchumi,wengi huku mtaani wanakwambia Serikali inakusanya kabla ya 2020 itaanza kumwaga pesa kwa wanyonge.

Wanadhani unaweza kuyaona mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja ndsni ya miaka mitano(Mimi sio mtaalamu wa Uchumi) lakini kitakachotokea ni kuwa wale wanaokula mlo mmoja huenda wakendelea na huohuo mmoja mpaka 2020,wale wenye milo mitatu huenda wakaendelea na hiyo mitatu mpaka 2020,sasa Kampeni zikifika wananchi watalishwa sumu kali,wataulizwa kila mmoja ajitathmini maisha yake yamebadilika wapi? hayo yatafanyika majukwaani na kwenye vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya Kijamii.

8. Kupiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa,hili linalalamikiwa sana na wapinzani lakini huenda ikwa ndio sababu ya kukiangusha Chamam cha mapinduzi, kuzuia Mikutano ya hadhara maana yake ni kulimbikiza silaha na makombora ya kisiasa.
Ikifika mwaka 2020 hakuna atakaeyazui mashambulizi mengi kwa muda mfupi wa Kampeni,CCM itakuwa upande wa kuzuia badala ya kushambulia,wananchi wataambiwa mambo mengi yatakayokosa muda wa ccm kuyafafanua na wananchi wayaelewe,Rejea Makomboroa ya zitto kwenye kile alichokiita Oparation Linda Demokrasia pale Zakhiem mbagala,Makombora yale yalileta mtikisiko kiasi cha Polisi kumuhoji kuwa anachafua taswira na heshma ya Rais. Hatimae mikutano ikafungwa,lakini hakuna atakaezuia mikutano 2020,Makombora mengi yatavujishwa na wasaliti wa ccm na hapo unaweza kuwa mwisho wa ccm.

Lakini ili ccm Ianguke Chali ya mende wapinzani wasifanye kosa la kuweka Mgombea,Alieshinda 2015 hakushinda si kwa sababu alikuwa mwanasiasa mkubwa,bali alishinda kwakuww hakukuwa na mwanasiasa bora zaidi yake.

Pia Kushinda kwa upinzani kunategemea sana uhuru wa tume ya taifa ya Uchaguzi.

Nilikuwa najaribu Mitambo,japo mimi sio Shekh Yahya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LINGINE..HUU UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA..UNAJUA JANA WAMESEMA ILIBIDI WAPUNGUNZE KODI NYINGI..MAANA YAKE HATUTAPATA MANUFAA YEYOTE MAKUBWA SERIKALINI.
LINGINE.. HII HABARI YA KUHAKIKISHA KILA SHILINGI INAFANYA KAZI INAYOFAA..SIS WATANZANIA TUNAPENDA DILI HIVYO HUYU HATUFAI.

Kama Kuna ka ukweli vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm inaanguka bila tume huru labda wachukue bunduki ndiyo watatushinda, lakini kosa la 2015 limeahatafutiwa dawa ccm watatulia tu
 
Ukiona hivo ujue athari za ile kauli kwenye mabango wakati wa Laurent, "chagua Magufuli" imeanza kuonekana
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom