First Half Bunge Maalumu la Katiba: CCM 2, UKAWA 0.

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Kwanza nitangulie kusema jambo moja… CCM na UKAWA ni wale wale tu; hakuna tofauti yoyote miongoni mwao. Kila mmoja hapa ni mtetezi wa maslahi yake. Ni bahati mzuri kwa UKAWA kwamba Rasimu ya Pili imejibu maslahi yao lakini endapo mapendekezo ya muundo wa muungano yangekuwa ni serikali mbili, wala leo hii tusingewasikia wakipita huku na kule na kusema LAZIMA MAONI YA WANANCHI YAHESHIMIWE!
Turudi kwenye mada. Hatua ya UKAWA kususia BMK moja kwa moja inatoa ushindi kwa CCM… angalau kwa sasa, ni ushindi wa 2-0! Ni ushindi kwa CCM kw​avile endapo UKAWA hawatarudi bungeni, moja kati ya haya yafuatayo kitatokea:

  • Rais Kikwete, ikiwa anayo mamlaka hayo, anaweza kuamua kufuta mchakato wa katiba. Ikiwa hili litafanyika, tutaendelea kutumia katiba ya sasa kwa miaka mingine kadhaa. Who knows? May be even ten years or so! Hili litategemea sana na Rais ajaye 2015. Na hapa tukumbuke kwamba, wananchi wengi watamuunga mkono JK endapo ataamua kufuta ama kusimamisha mchakato. Je, hili likitokea ni nani atakuwa ameshinda? CCM au UKAWA?

  • Endapo Rais hatafuta mchakato, basi BMK linaweza kuendelea hapo August kama ilivyopangwa ama kwa kiburi tu na jeuri ya CCM au kwa matarajio kwamba labda UKAWA watarudi. Hata hivyo, kwavile Sheria ya Mabadiliko ya Katiba [Act 26(2)] inataka theluthi mbili kutoka bara na visiwani, basi katika mazingira kama hayo, BMK lisilo na UKAWA halitakuwa na ubavu wa kupitisha Rasimu unless CUF wajitoe UKAWA na kurudi BMK. People should never despise the possibility ya CUF kuwasaliti CHADEMA na kuamua wao kama wao kurejea BMK. CUF na CHADEMA hawa si wamoja… ni vile tu wanaunganishwa na kile kinachofahamika kama “adui wa adui yako, rafiki… and in fact, si kwamba adui wa adui yako ni rafiki bali ni mshirika wako wa muda”. ANYWAY, kwa mara nyingine tena, ikiwa BMK halitaweza kupitisha Rasimu, tuataendelea kutumia katiba ya sasa hadi pale itakavyokuwa vinginevyo. Hapa napo, CCM 2, UKAWA 0.

  • Possibility ya tatu ni kwamba CCM wanaweza kufanya usanii wakaamua kukubali matakwa ya UKAWA ya kujadili Rasimu. CCM wanaweza kuamua jambo hilo ili kuonesha kwamba wao hawana tatizo na bado wanahitaji mchakato uendelee! JK atapongezwa na wananchi kila pahala na kuonekana jinsi alivyo msikivu! Lakini kwa upande mwingine, hili likitokea UKAWA watavimba kichwa na kupita huku na kule wakitamba kifua mbele kwa kujiona wameshinda. BMK litaendelea wakati UKAWA wapo ndani ya nyumba. At the end of story, CCM wanaweza kukwamisha kwa kutopitisha rasimu… hapa tena tunarudi kule kule katika kuendelea kutumia katiba ya sasa and eventually turning the score board into, CCM 2, UKAWA 0.

Kama hivyo ndivyo, ni nini basi kilicho bora? Serikali ya Tanganyika au Katiba iliyo bora inayojali maslahi ya Watanzania?

Kwa mtu ambae amesoma rasimu atakubali kwamba Rasimu ile ina mambo mazuri sana tena yenye kutia matumaini kuliko suala la muundo wa muungano. Ni uongo uliopopitiliza na usio na maana yoyote kudai kwamba mambo mazuri yaliyomo ndani ya Rasimu hayawezi kutekelezeka kwenye mfumo/muundo mwingine EXCEPT serikali tatu! Yote yaliyomo yanaweza kufanyika ama iwe ndani ya muundo wa serikali moja, mbili, tatu au wowote ule.

Kwa maoni yangu, ikiwa leo hii UKAWA wanaamua kurudi BMK basi hapo hapo itakuwa score board itabadilika na kusoma UKAWA 3, CCM 2. Kabla ya yote, hili likitokea bila kujali kwamba watazomewa wakati wanaingia bungeni au la, kwanza UKAWA watapata RESPECT ya hali ya juu sana kutoka kwa wananchi wa kada mbalimbali kwa ile tu kuonesha nia ya ku-sacrifice matakwa yao kwa ajili ya katiba! Hapa tusisahau kwamba, wanazi wa CCM wanaomba UKAWA wasirudi ili katiba ya sasa iendelee kutumika kwa sababu inawa-favor. Inawa-favor si kwa sababu muundo uliomo kwenye katiba hiyo ni mfumo wa serikali mbili bali inawa-favor kutokana na contents zingine zilizomo kwenye katiba... contents ambazo unfortunately UKAWA wanataka ziendelee kutumika in other way round at the expense of muundo wa serikali tatu; muundo ambao wao kama wapinzani hauna direct benefit yoyote kwao; hususani kwa CHADEMA (angalau hii ya sasa).

Itakuwa ni busara kwa Mbowe na Seif Sharrif kuwarudisha wanachama wao kundini kisha wapiganie kuwamo yale ya msingi kabisa yaliyopendekezwa na tume. Sidhani kama muundo wa muungano ni jambo la msingi zaidi kuliko suala la Maadili ya Uongozi na Utumishi wa Umma ambayo, ikiwa Rasimu niliyonayo ndiyo update, basi yamewekwa kwenye sura ya Tatu. Sidhani kama muundo wa muungano ni jambo la msingi zaidi kuliko suala la Haki za Binadamu, Wajibu wa Raia na Mamlaka ya Nchi Yaliyomo kwenye Sura ya Nne. Sidhani kama muundo wa muungano ni jambo la msingi zaidi kuliko suala la Muundo, Haki na Madaraka ya Bunge la JMT kama ilivyo katika Sura ya Tisa. Sidhani kama muundo wa muungano ni jambo la msingi zaidi kuliko suala la Muundo wa Mahakama na suala zima la utoaji haki ambayo yamo Sura ya Kumi.

Mifano ni mingi… kwahiyo napata shida sana kuamini kwamba ni sahii ku-sacrifice yote hayo at the expense of serikali tatu! Hapa tusisahau jambo moja la kisaikolojia. Ikiwa UKAWA wanarudi bungeni, basi CCM watalazimika kutokuwa ving’ang’anizi huko mbeleni kwavile tayari UKAWA wameshaonesha nia njema na CCM wakiendelea kuwa ving’ang’anizi kwa wayatakayo wao tu, basi hapo ndio moja kwa moja watadhirisha kwamba hawataki katiba mpya! In contrast, ikiwa leo hii CCM wanaamua ku-sacrifice na mjadala unaotakiwa na UKAWA ( wa serikali 3) kuendelea, basi hapo mbeleni, UKAWA watalazimika ku-sacrifice mambo ya msingi kabisa yatakayokataliwa na CCM. Watafanya hivyo coz’ wakiendelea kila wakati kung’ang’ania kile watakacho wao tu kwa kisingizio chochote, hatimae wao ndo wataonekana wasio na nia njema coz’ pamoja na CCM ku-sacrifice sera yao (hata kama watakuwa na nia ya kukwamisha hapo baadae) lakini bado UKAWA wanataka kila wakati wasikilizwe wao!!!
 
Toka lini CCM watakubali kuitowa nchi hii jambo la mwanzo hawatakubali hata siku moja kuwa na TUME huru Ya Uchaguzi
 
Tusijidanganye kuwa CCM wana nia ya kupata katiba mpya; wao toka mwanzo hawakutaka zoezi la katiba kwasababu walisema halikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi hivyo ni Kikwete personally katika shauku ya kutenegeneza legacy yake ndio akalileta suala la kuandika katiba mpya.

Mchakato mzima itakukuwa busara kama utaanza upya kwani it had a false start; tukianzia kwanza na ile sheria tu iliyompa madaraka Rais kuteua wajumbe wa bunge la katiba ambalo linawajumuisha wabunge na wajumbe wa baraza la wawakilishi. Sio sahihi kwa wabunge na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa wajumbe wa bunge la katiba kwasababu mambo mengi yanayohitaji uamuzi yanawahusu wao na maslahi yao hivyo itakuwa vigumu sana kwao kuwa objective . Kuna masuala kama vile ukomo wa muda wa kuwa wabunge; masuala ya wabunge kutokuwa mawaziri; kupunguzwa kwa viti vya ubunge [ constituencies] pamoja na masuala yahusuyo kuwepo au kutokuwepo viti maalum vya wabunge ,Yote haya na mengine mengi yanahitaji kuamuliwa na wajumbe ambao hawana conflict of interest!!

Itakuwa busara kama process yote ikaanza upya taking into account concerns hizo at the same time mambo mengine kama kuwa na tume huru ya uchaguzi; kuwa na independent candidates na mengine yatakayoamriwa yakatekelezwa by legislation wakati utaratibumzuri wa kupata katiba iliyobora ukiandaliwa through consensus. Katiba iliyo bora haiwezi kundikwa kwa muda mfupi ili kukidhi matakwa ya kisiasa!!!
 
Ni kweli kabisa ccm na kikwete mwenyewe hawaipendi rasimu ya pili ya katiba maana ni mwiba kwao na vizazi vyao.
 
nazDaz
Muundo wa muungano ni jambo muhimu kuliko unavyodhani.
Ibara zote za katiba kwa namna moja au nyingine zinategemea muundo wa muungano.

Laiti isingekuwa hivyo, basi kusingekuwa na mvutano. CCM wanatambua hilo, wapinzani wanatambua hilo.
 
Last edited by a moderator:

Usizunguke mbuyu,tanganyika iliyo jificha kwenye koti la muungano ndio donda sugu la muungano huu,ili lipoe donda hili lazima tanganyika ifichuliwe huko iliko jificha. zanzibar kwanza.
 
Ndiyo maana tunataka Serikali ya Tanganyika. Kikwazo ni wznz wanaotaka S2. Wznz wamepatwa na nini hadi kumkana Jumbe na leo Nyerere ni shujaa wao. Kwanini wanakula matapishi yao! Je, kuna ufahamu, utambuzi au kaelimu hapo!
 
Ndiyo maana tunataka Serikali ya Tanganyika. Kikwazo ni wznz wanaotaka S2. Wznz wamepatwa na nini hadi kumkana Jumbe na leo Nyerere ni shujaa wao. Kwanini wanakula matapishi yao! Je, kuna ufahamu, utambuzi a.u kaelimu hapo!

Acha kupotosha umma,zanzibar haihusiki na upotevu wa tanganyika,kadri watanganyika mnavyo jificha kwenye koti la muungano ndio mnazidi kujikubalisha kuwa nyinyi watumwa milele,zanzibar kwanza.
 
Terrible shit analysis! Huwezi ukasema Muundo wa serikali siyo muhimu kuliko miundo ya mihimili mingine! MUUNDO ndo unatoa uelekeo wa mfumo mzima. Mfano, huwezi ukatengeneza ndege ikiwa na umbo la meli ukategemea itapaa, au huwezi kutengeneza Boti ikiwa na muundo wa treni ukategemea itaelea! Ukasema bora kuna mifumo mizuri ya umeme na viti! Ni uwendawazimu ndo maana hakuna maendeleo ya maana tunayopata. Umbo la serikali yetu halilingani na mazingira na speed tunayoitaka. Rudisha Tanganyika ijidhibiti utaona kasi ya maendeleo itakayopiga kulingana na rasilimali tulizonazo.
 
nazDaz
Muundo wa muungano ni jambo muhimu kuliko unavyodhani.
Ibara zote za katiba kwa namna moja au nyingine zinategemea muundo wa muungano.

Laiti isingekuwa hivyo, basi kusingekuwa na mvutano. CCM wanatambua hilo, wapinzani wanatambua hilo.
Nguruvi3,
Kwamba muundo wa muungano ni jambo muhimu sijapinga na kwamba Ibara zingine zote zinategemea muundo wa muungano, ni jambo ambalo pia siwezi kupinga! Hoja yangu hapa ni kwamba, ni Ibara ipi... kwa jinsi vile ilivyo, au hata kama itabadilika lakini content yake kubaki vilevile, bado ikawa okay kwa mfumo wa serikali X na sio Y! Mathalani, hivi kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kunahitaji kuwa na muundo fulani wa muungano? Hivi kuwa na Tume Bora ya Maadili ya Utumishi wa Umma kunahitaji muundo X na sio Y? Hivi kuwa na Ibara itakayolazimisha uwajibikaji kunahitaji muundo huu wa muungano na sio ule? Hivi kuwa na chombo kitakachohakikisha uwazi na uwajibikaji panahitaji muundo fulani wa muungano na sio wa aina fulani? Hivi kuwa Mahakama Huru, Bunge Huru n.k kunahitaji muundo huu na sio ule? Mifano ipo mingi... sidhani kama kuna jambo lenye maslahi kwa umma ambalo linaweza kufanya kazi vizuri kwa muundo fulani tu na sio mwingine unless kama unataka kuzungumzia masuala la utawala... ambayo ndiyo ninayoyaona sana wanasiasa wanayazungumzia. Matatizo ya msingi ya nchi hii ambayo ni Rushwa na Uwajibikaji yanaweza kupatiwa suluhu kwenye muundo wowote wa muungano bila kujali kama ni muundo wa serikali 1, 2, 3 au wowote ule!
 
Terrible shit analysis! Huwezi ukasema Muundo wa serikali siyo muhimu kuliko miundo ya mihimili mingine! MUUNDO ndo unatoa uelekeo wa mfumo mzima. Mfano, huwezi ukatengeneza ndege ikiwa na umbo la meli ukategemea itapaa, au huwezi kutengeneza Boti ikiwa na muundo wa treni ukategemea itaelea! Ukasema bora kuna mifumo mizuri ya umeme na viti! Ni uwendawazimu ndo maana hakuna maendeleo ya maana tunayopata. Umbo la serikali yetu halilingani na mazingira na speed tunayoitaka. Rudisha Tanganyika ijidhibiti utaona kasi ya maendeleo itakayopiga kulingana na rasilimali tulizonazo.
Acha kutoa mifano ambayo wala haina mashiko kwenye mada.. ni kituko muundo wa muungano kuulinganisha na muundo wa ndege!! Hoja ya msingi hapa ni jambo gani linaweza kuwa efficient kwenye muundo X na lisiwe efficient kwenye muundo Y taking into consideration matatizo ya msingi ya nchi hii!! Moja ya matatizo ya msingi ni ufisadi ambao whether uwe na serikali 1 or mia moja, bado muundo husika hautaweza kuondoa ufisadi! Labda njia pekee ni kuwa na muundo huru wa mahakama na suala zima la uwajibikaji.... mahakama huru au uwajibikaji haungalii una serikali mbili, tatu au nne....
 
Ndiyo maana tunataka Serikali ya Tanganyika. Kikwazo ni wznz wanaotaka S2. Wznz wamepatwa na nini hadi kumkana Jumbe na leo Nyerere ni shujaa wao. Kwanini wanakula matapishi yao! Je, kuna ufahamu, utambuzi au kaelimu hapo![/QUOTE Nguruvi3, unaweza kuniambia serikali ya Tanganyika itakavyoweza kutatua matatizo sugu ya Watanganyika hususani yale ya ufisadi na kukosekana kwa uwajibikaji?
 
Kwakweli sijaelewa swali lako,hebu fanya ufafanuzi kidogo.
 
Kwakweli sijaelewa swali lako,hebu fanya ufafanuzi kidogo.
Mkuu wangu Nguruvi3 hata mimi nimeshindwa kukuelewa kv ume-quote ndivyo sivyo manake hata wewe mwenyewe umeona... umeji-quote mwenyewe na hapo hapo umeniuliza mimi swali!!!! Anyway, let me guess... labda unauliza swali ambalo nimehoji jinsi serikali ya Tanganyika itakavyoweza kutatua matatizo sugu ya Watanganyika hususani yale ya ufisadi na kukosekana kwa uwajibikaji!! Msingi wa swali langu ni kwamba, wengi ni kama tunataka kuamini kwamba kurudi kwa Tanganyika ndio suluhisho na ndio maana hata mjadala wa bunge umeingia dosari kv tu upande mmoja unaamini katika kurejea kwa Tanganyika! Mimi binafsi, naamini matatizo sugu ya nchi hii ni UFISADI/RUSHWA, WIZI na ukosefu wa UWAJIBIKAJI! Matatizo mengine yote utakayotaja, utakuta mzizi wake ni ufisadi na ukosefu wa uwajibikaji! Kutokana na hilo, ndipo nikahoji Tanganyika itafanya nini cha kuondoa maradhi hayo... kitu ambacho hakiwezi kufanyika kwenye mfumo mwingine wowote ule except ule tu ambao ndani yake kuna Tanganyika!!!
 
Unaelemea CCM hata katika maelezo yako. Bado hata UKAWA wakiamua kutoka nje sasa na milele bado katiba mpya itakuja tena hili ndiyo litachochea wananchi waitake katiba mpya iliyo bora kuliko UKAWA wakirudi na baadaye washindwe kwa kura za CCM kulazimisha muundo mbovu wa sasa wa serikali 2
 
Mkuu wangu Nguruvi3 hata mimi nimeshindwa kukuelewa kv ume-quote ndivyo sivyo manake hata wewe mwenyewe umeona... umeji-quote mwenyewe na hapo hapo umeniuliza mimi swali!!!! Anyway, let me guess... labda unauliza swali ambalo nimehoji jinsi serikali ya Tanganyika itakavyoweza kutatua matatizo sugu ya Watanganyika hususani yale ya ufisadi na kukosekana kwa uwajibikaji!! Msingi wa swali langu ni kwamba, wengi ni kama tunataka kuamini kwamba kurudi kwa Tanganyika ndio suluhisho na ndio maana hata mjadala wa bunge umeingia dosari kv tu upande mmoja unaamini katika kurejea kwa Tanganyika! Mimi binafsi, naamini matatizo sugu ya nchi hii ni UFISADI/RUSHWA, WIZI na ukosefu wa UWAJIBIKAJI! Matatizo mengine yote utakayotaja, utakuta mzizi wake ni ufisadi na ukosefu wa uwajibikaji! Kutokana na hilo, ndipo nikahoji Tanganyika itafanya nini cha kuondoa maradhi hayo... kitu ambacho hakiwezi kufanyika kwenye mfumo mwingine wowote ule except ule tu ambao ndani yake kuna Tanganyika!!!
Hapa unachanganya vitu viwili. Kuna tatizo la ufisadi, wizi na umasikini. Halafu kuna tatizo la muungano.
Ufisadi na wizi ni matatizo yaliyopo katika jamii na yanahitaji kushughulikiwa bila kujali muundo wa muungano. Iwe ni S1,S2,S3 tatizo linahitaji kushughulikiwa.

Tatizo la muungano ni manung'uniko na linafunika sehemu kubwa ya matatizo ya umasikini, ufisadi na wizi.
Ili tuweze kuondoa wingu hilo ni lazima kwanza tushughulikie tatizo la muungano.

Kurejea kwa Tanganyika kuna maana moja, kumaliza manung'uniko yasiyo ya lazima kwa upande wa wazaznibar na Watangayika. Kutoa nafasi kwa kila upande kushughulikia fiscal autonomy yake.
Ni kuanzia hapo kila mmoja anapswa kujua au ku design mkakati wa kupambana na matatizo ya jamii husika.

Hatuwezi kupambana na ufisadi ili hali kuna wingu nene la malalamiko, kutuhumiana na kubaguana kunakosababishwa na malalamiko yasiyo ya lazima. Structure ya serikali na muundo wake ni vitu muhimu sana katika kupanga, kutekeleza na kufikia malengo yakiwemo uliyosema.
 
Wala cjachanganya mambo... mimi nilichotaja ni yale ambayo nayaona matatizo ya msingi yanayolikabili taifa hili... manung'uniko hayawezi kuwa matatizo ya msingi kv sidhani kama patatokea muundo ambao hautakuwa na manung'uniko. Kusini, kwa maana ya Lindi na Mtwara na Kaskazini kwa maana ya Arusha na Kilimanjaro, zote zipo Tanganyika lakini bado kusini hawajaacha kunung'unika kwamba serikali inaelekeza shughuli za maendeleo kwa upendeleo... manung'uniko ni silika ya mwanadamu, labda jambo la kuangalia ni endapo manung'uniko yenyewe yana msingi na kweli yana athari kwa jamii husika na si tu kwamba ni manung'uniko ya watu wachache wenye sauti lakini kutokana na sauti zao yanabadilika kuwa ni manung'uniko ya wengi ambayo kimsingi athari ama chanzo cha manung'uniko hayo ni ya hao wachache. Mathalani, watu wanaoongoza kwa manung'uniko ni Zanzibar... hususani wafuasi wa CUF. Ni wananchi ndio wananung'unika lakini ukiangalia kwa makini ni manung'uniko yenye maslahi kwa viongozi na wala sio watu wa kawaida unless wawe ni wale wenye mwamko wa utaifa!

Kwamba tatizo la muungano ni manung'uniko ambayo yanasababisha hata kufunika matatizo ya msingi, hapa naomba nisikubaliane na wewe! Sidhani kama mwananchi wa kawaida ana shida sana na muundo wa muungano kuliko kushughulikwa matatizo yake ya msingi. Mimi binafsi, wala sioni kama kuna kitu chochote ninakikosa kwavile tu tupo kwenye mfumo wa serikali mbili lakini kuna mengi nayakosa kwa sababu tu watu hawataki kuwajibika, kuna uzembe kila mahali, kuna ufisadi na wizi wa hovyo n.k.... haya yote wala hayasababishwi na muundo wa muungano otherwise kwenye mataifa ambako suala la muundo si tatizo, haya yasingekuwepo!!!!
 
Back
Top Bottom