Hiki ndicho kitakachoiangusha CCM 2020

Haya maneno kwa Mara ya kwanza yaliandikwa kwa mkono Wa MTU asiyeonekana yakimuonya mfalme Nebukadreza aliyekua jeuri na kiburi kuliko kawaida hata alidiriki kuwataka watu wamuabudu.

Kama mwandishi alikuwa haonekani, sasa wewe au hao walijuaje kama ameandika mtu kwa kutumia mkono wake? Ukumbuke kuna walemavu wanatumia miguu kuandika.

Hii inawezekana kuwa yameandikwa na mtu asiyejulikana NA SIO hasiyeonekana. Kwa maana aliandika na kuweka sehemu bila watu kumuona. Na kama alitumia mkono basi hakukuwa na watu wenye uwezo wa kuandika wenye ulemavu wa mikono.
 
Kuna utafiti nimeufanya takribani week mbili nimegundua chama cha mapinduzi ikiwemo baadhi na makada wemeanza kusahaulika.
Miongoni mwa watanzania.

Sasa hivi ukizungumzia ccm watu wengi hawawezi kukuelewa ni chama ambacho watu wengi wameanza kukisahau hata wale makada tuliokuwa tukiwasikia mitandaoni , ITV KATIKA mijadala,
Siku hizi hawasikiki .......

Siku hizi story ya mjini ni LIPUMBA, SEIF , LISU ,MBOWE, CHADEMA, BASHITE NA MAGUFULI .

LAKINI UKISEMA CCM WATU HAWAKUELEWI
Subiri 2020 uone evergreen itakavyo chipua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM itapata wakati mgumu sana Uchaguzi 2020.
1.Matajiri ambao taabia zao ni kutengeneza faida ,wamebanwa mpaka hawapumui,watamwaga pesa Upinzani ili waweke mtu wanaemtaka ili kutafuta nafuu.

2. Wasaliti waliopo ndani ya CCM ni wengi kuliko hata wapiga kura wa Upinzani,awali watu waliokuwa CCM walikuwa wanapata kinga ya kufanya mambo yao,Iwe Ujambazi,kukwepa kodi,biashara haramu nk. Sasa hivi Wote ni wahanga na wanaisoma namba,hakuna tena vile viposhoposho vya vikao,wanapoga kelele kuliko hata waponzani wanavyopoga kelele.

Hawa ni wale CCM maslahi aliosema Mzee Warioba ambao kimsingi ni wengi ndani ya CCM kuliko hata CCM asilia,hapo watapiga kura za hasira kwakuwa watakuwa hawana chakupoteza.

3.Vyombo vya habari navyo sasa hivi vinaogopa kupigwa pini kwakuwa Siri Kali ipo kazini,haina ubabaishaji,ukifika mwaka wa kampeni Mabilionia ambao ni jamaa zao na wale waliopo Segerea watamwaga pesa kwa waandishi na wamiliki,vitafukuliwa vitu na kwakuwa watanzania ni wazee wa kushangilia na kwenda na upepo,basi watasahau utumbuaji wote unaofanyika.

4. Watumishi wa Umma ambao wao huaminiws sana na wananchi hasa wa vijijini katika kutoa mwelekeo wa yupi wa kuchaguliwa,hili kundi lina manung'uniko makubwa lkn hawana chaguo lingine zaidi ya kuvumilia ,kundi hili ndilo linalosimamia chaguzi zetu na huenda ikatumika hasira za maisha magumu kuiondoa CCM madarakani (ingawa mshahara utaongezwa 2019 )ili kuwasahaulisha.

5.Bomoabomoa,hii itawatesa sana CCM 2020,maelfu ya wananchi wakiwemo wana ccm tena viongozi waandamizi nao wamekumbwa na kadhia hii,wamejaribu kutumia vyeo vyao kama zamani walau kulainisha mambo lkn wapi.Mamlaka zinasisitiza kuwa Bomoabomoa ipo palepale,sasa hawa wanaenda kutumbukia kwenye wimbi la umaskini na kukosa makazi kwa maelfu ya wana wananchi hasa wana CCM.

6.Tumbuatumbua ya viongozi waandamizi serikalini,wale jamaa huenda mpaka sasa wan chama cha siasa walichojipanga kukiunga mkono,Orodha yao ni ndefu sana lakini ni watu wenye kipato,Elimu na wenye ushawishi kwa jamii,kubwa zaidi watu wanaojua mambo mengi yanavyofanyika,hawa wanaweza kukiangusha chama cha mapinduzi ifikapo 2020.

7.Uelewa wa wananchi,wananchi wengi wanaamini Mabadiliko hufanyika ghafla hasa yale ya Kiuchumi,wengi huku mtaani wanakwambia Serikali inakusanya kabla ya 2020 itaanza kumwaga pesa kwa wanyonge.

Wanadhani unaweza kuyaona mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja ndsni ya miaka mitano(Mimi sio mtaalamu wa Uchumi) lakini kitakachotokea ni kuwa wale wanaokula mlo mmoja huenda wakendelea na huohuo mmoja mpaka 2020,wale wenye milo mitatu huenda wakaendelea na hiyo mitatu mpaka 2020,sasa Kampeni zikifika wananchi watalishwa sumu kali,wataulizwa kila mmoja ajitathmini maisha yake yamebadilika wapi? hayo yatafanyika majukwaani na kwenye vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya Kijamii.

8. Kupiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa,hili linalalamikiwa sana na wapinzani lakini huenda ikwa ndio sababu ya kukiangusha Chamam cha mapinduzi, kuzuia Mikutano ya hadhara maana yake ni kulimbikiza silaha na makombora ya kisiasa.
Ikifika mwaka 2020 hakuna atakaeyazui mashambulizi mengi kwa muda mfupi wa Kampeni,CCM itakuwa upande wa kuzuia badala ya kushambulia,wananchi wataambiwa mambo mengi yatakayokosa muda wa ccm kuyafafanua na wananchi wayaelewe,Rejea Makomboroa ya zitto kwenye kile alichokiita Oparation Linda Demokrasia pale Zakhiem mbagala,Makombora yale yalileta mtikisiko kiasi cha Polisi kumuhoji kuwa anachafua taswira na heshma ya Rais. Hatimae mikutano ikafungwa,lakini hakuna atakaezuia mikutano 2020,Makombora mengi yatavujishwa na wasaliti wa ccm na hapo unaweza kuwa mwisho wa ccm.

Lakini ili ccm Ianguke Chali ya mende wapinzani wasifanye kosa la kuweka Mgombea,Alieshinda 2015 hakushinda si kwa sababu alikuwa mwanasiasa mkubwa,bali alishinda kwakuww hakukuwa na mwanasiasa bora zaidi yake.

Pia Kushinda kwa upinzani kunategemea sana uhuru wa tume ya taifa ya Uchaguzi.

Nilikuwa najaribu Mitambo,japo mimi sio Shekh Yahya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchambuzi wako murua kabisa tena umehitimisha vizuri kabisa kuwa ushindi kwa upinzani inategemea Uhuru wa tume ya uchaguzi. Nakukumbusha kuwa hayo makundi yote uliyoyataja mchango wake ktk kuiondoa CCM mdarakani kupitia ballot box ni ndoto endapo referee (TUME) ataendelea kubaki huyu huyu, sheria zilezile na uwanja uleule. Lakini vilevile nikukumbushe kuwa watanzania wengi sasa hivi hawana hamasa na CCM Bali JPM na wapinzani wanapaswa kujipanga kimkakati kumkabiri JPM na sio CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahahahaha
JPM hakamatiki jamani mnaona misafara yake inavyozuiwa njiani? Mnadhani kwanini Umma una hamu nae? Unafikiri watu wanaojaa barabarani ukifika wakati wa uchaguzi watafanya nini?
Pambaneni na hali zenu JPM hakamatiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanashindwa kupambanua kuwa Umma hauna habari na CCM Bali unahamasika na JPM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
It is very true.

Ile Lumumba buku 7 team kwa nadra sana nowadays utawaona humu JF......

Wapi akina Ritz, Lizaboni, mama Faizafoxy na wengineo waliokuwa wakidominate sana Jukwaa la siasa humu JF?

Huyu jamaa amekaba kila mahali....

Usije shangaa ule utabiri wa Mwalimu Nyerere ukaanza timia....

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa upinzani
wa dhati wa kuinng'oa CCM lazima utatoka huko huko CCM.

Sasa hivi tayari wapo akina Lowassa, Sumaye, Kingunge, Masha na wengineo wapo opposition.

Lakini kutokana na hii style ya utawala wa huyu Mheshimiwa wa ONE MAN SHOW anayoindesha, ambapo wanasiasa almost wote ndani ya CCM wamepotea......

Ni dhahiri ingawa makada wengi hawasemi openly, lakini wengi wapo dissatisfied na utawala huu na upo uwezekano wengi wao wakajoin Ukawa in the near future....

Let us wait and see
Is there any logic for us to wait for something positive to happen accidentally? Things are made to happen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini asiite Tanzania yake? Hata wewe kama una uraia wa Tanzania nia Tanzania yako. Kuna kitu kibaya hapo amekisema? Acheni lawama ambazo hazina tija. Si shangai nyie kuwa miongoni mwa watu ambao mko tayari kusifu mazuri ya nchi nyingine kuliko yanayo tokea kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app

JPM hana nchi wala Taifa ana uraia tu.Tanzania ni yetu sote ataondoka ataiacha Tanzania. Anaweza kuwa na CCM lakini siyo Tanzania. Hana hata Chato sembuse Tanzania!

Msiabudu binadamu mwenzako ni dhambi
 
Kama mwandishi alikuwa haonekani, sasa wewe au hao walijuaje kama ameandika mtu kwa kutumia mkono wake? Ukumbuke kuna walemavu wanatumia miguu kuandika.

Hii inawezekana kuwa yameandikwa na mtu asiyejulikana NA SIO hasiyeonekana. Kwa maana aliandika na kuweka sehemu bila watu kumuona. Na kama alitumia mkono basi hakukuwa na watu wenye uwezo wa kuandika wenye ulemavu wa mikono.

Pole sana nenda kasome biblia ndiyo utaelewa.Mungu ni muweza wa kila jambo,wala hashindwi kufanya maajabu yake au Muujiza wake.

Ndiyo sababu hata siku na wapi binadamu atafia ,binadamu mwenyewe hapajui
 
Wewe jiaminishe hivyo hivyo......

Hata Goliath alidiriki kutamka kwa kiburi kikubwa kwa kusema mnaniletea hska "katoto" Dsudi ndiyo apambane na Mimi?

Nini kikichomtokea Goliath kama siyo kupokea kipigo cha aibu kutoka kwa "bwana mdogo" Saudi?

Unayoina nguvu ya CCM inatokana zaidi ya kuwa ni chama dola.......

Kwa kuwa CCM ina support ya vyombo vya dola.

MaDC na naRC wote wako upande wa CCM.

Msajili wa vyama yuko upande wa CCM.

Polisi wako upande wa Sisiem.

Tume ya Taifa ya uchaguzi ipo upande wa CCM.

Siku ambayo CCM itavuliwa kutoka chama dola na kubakia kuwa chama cha kawaida cha siasa kama vyama vingine vya siasa kama vile Chadema na CUF bila kubebwa na "mbeleko" ya vyombo vya fola, siku hiyi hiyo ndiyo The end of CCM!
Sasa ndugu hiyo CCM itavuliwa kutoka kuwa chama dola na nani kama sio umma na vilevile kama hakuna mikakati thabiti toka ndani ya umma wa Watanzania wenyewe huyo Mungu wa mbinguni ataingilia mlango gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba Mungu kabla haijaanguka,reli ya kati iwe
imekamilika na barabara ya pale tazara ikamilike
mengine malizia wewe.
Kwa nilichokiona uchaguzi
uliopita,sijui kama kura za wapiga
kura zinahitajika ili chama kishinde
labda hiyo sheria ya nebkadreza.
Hawa jamaa sasa hivi wameshindwa kuja na hoja za kimkakati kuthibitisha namna CCM itakavyoshindwa 2020 badala yake wanakuja na matumaini ya ki-Ramli kuwa CCM itaondolewa kutoka kwa majaaliwa ya mbinguni na siku zote hii ndio dalili kuu ya mtu mchovu aliyekata tamaa ktk mapambano ya maisha huwa anajifariji kwa usemi kuwa anamuachia Mungu wakati ni majukumu yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote uliyo yaandika mkuu yana substance. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa Magufuli atapita tu. Na amekwisha kuwa Rais wa hawamu nyingine. Kama wewe huoni mabadiliko makubwa ambayo yametokea basi wewe huishi Tanzania. Sasa hivi unaenda ofisi yeyote kutaka huduma na unaheshimiwa kama binadam. Jamani watumishi wa umma walivyo kuwa wanakusanyika wanyanyasa watu! Hat passport unapata bila hongo halafu wewe unasema eti CCM inaweza anguka kwenye 2020? Labda bila Magufuli. Kwanza hao watu ulio waita matajiri hela sasa hivi hawana. Na isitoshe kama huoni clip za maadamano za Magufuli basi tatizo lako. Sisi enzi ya Nyerere tulikuwa tunaandaliwa tukasimame barabarani ili kumpokea lakini kwa Magufuli ni spirit nyingine. Watu wanakusanyika wenyewe kwa hiari yao kumpongeza na shauku la kumwona. Tatizo ni wengi wanamwona yeye ni kama mkombozi. Nyie mliokuwa upande mwingine wa maisha mna chuki zenu binafsi.

Nakupa siri tu ndugu yangu. Magufuli ame waamusha watanzania kudai haki zao. Yale yaliyokuwa yanafanyika kipindi cha utawala wa Kikwete hayatarudi tena. Watanzania wata question kila kitu kisicho enda sawa. Wamesha jifunza kuwa menge ni haki yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Obvious haya ni macho ya kiutu uzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naridhishwa na utendaji kazi wa Magufuli na usimamizi wa ilani ya uchaguzi unaofanywa na CCM
 
Utawala wa mabavu watu hawalijui maana ya hizo pushapu, kilikuwa kitendawili nini maana ya kupiga pushapu watu wakashindwa kujibu kumbe utawala wa kuwapeleka wananchi kwa nguvu uonevu na udkteta hata sasa watu wanajifanya kushangilia tu lkn maumivu wanayo makubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM hana nchi wala Taifa ana uraia tu.Tanzania ni yetu sote ataondoka ataiacha Tanzania. Anaweza kuwa na CCM lakini siyo Tanzania. Hana hata Chato sembuse Tanzania!

Msiabudu binadamu mwenzako ni dhambi
Tanzania is our MOTHERLAND, ukiitambua maana ya Nahau hii kongwe utagundua kuwa hata wewe Tanzania ni nchi yako. Hakuna anayemuabudu JPM lakini kumheshimu mfalme ni wajibu wa kimaandiko na amri ya Mungu ktk Misahafu ya dini zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom