Wiki iliyopita Bw. B. Membe amejitokeza na hoja zinazo kosoa utendaji mbali mbali wa Mh. Rais J.P. Magufuli. Sisi wengine ambao si wanasiasa au wanachama wa vyama vya siasa tunajiuliza timing ya hoja zake na nia ya hoja hizo. Hii ni serikali ya CCM ambayo yeye ni member wa NEC. Katika busara ya kawaida ukitaka kumkosoa ndugu yako hupandi juu ya mti na kutangazia umma, au kwenda nyumba ya jirani kulalamika. Unamwita na kuzungumza naye. Nitashangaa kama Bw. Membe haoni hilo hasa kama mwana diplomasia. Lakini vile vile, kama kuna mtu aliye iokoa CCM kutoweka ni JPM. On the other hand, kama kuna mtu ambaye angeimaliza CCM ni pale ambapo Bw. Membe angewekwa kama mgombea wa urais. Hiki hakipingiki, kama anaelewa approval rating ya JPM kwa Watanzania. Kwa maoni yangu, kama hoja za Bw. Membe anaziwakilisha kwa niaba ya kundi moja la watu ndani ya CCM, basi ielekwe hiki chama kitasambaratika. Mwisho wa siku, kundi la JPM litabakia washindi kwa ridhaa ya wananchi. Watanzania wamesha choka na siasa uchwara. Ni vyema Bw. Membe (na kundi lake -kama lipo) ajipime kama anayo integrity ya kuhoji anacho hoji. And, nadhani viongozi wa chama kaeni na kuliangalia hili.