GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,318
Imeingia week ya pili sasa tangu ndugu Membe aanze Kusikika kwenye magazeti akijitutumua kusikika na kusomeka.
Katika lile kundi liliohujumu uchumi wa nchi yetu yeye ameteuliwa sasa kuwa muongeaji akijaribu kukosoa utawala wa Magufuli. Kiuahalisia ni haki yake ya kikatiba hakatazwi.
Ila kilichopo nyuma ya pazia na maumivu baada ya kuona kuwa amesahaulika na ktk kila ambalo wao walifanya kwa ushirikiano na wenzake kuhujumu uchumi wa nchi hii.
Mtandao uliokuwa unawasidia TRA na bandarini umeondolewa.
Ni mtu mwenye majeraha na anayeonekana kuwa ana nafasi ya kusema kwa kuwa ashakata tamaa ya kupata cheo chochote.
Membe ni mnafiki ambaye alianza kwa kumsifia Magufuli alipositisha safari za nje na kudai watu walikuwa wanapishana angani kama nchi inawaka moto.
Baada ya teuzi zote kupita na pia yeye na watu wake kuathiriwa ameanza kupiga kelele.
Membe amewah kuikosoa CCM lini katika miaka 10 iloyopita? Leo ana uzalendo gani?
Membe ni mnafiki huyu ndo alitamba miaka ile uwa nchi haiwezi chukuliwa na wahuni kwa kutumia land cruiser mkonga akijipendekeza kwa Muaamar Ghadafi.
Hatimaye watu walichukua nchi na kumuua kwa aibu Ghadafi. Ni Membe huyu huyu aliwaunga mkono tena waasi kwa kuwatambua.
Ni mtu asiyeaminika hata kidogo ana haki kukosoa Maguful si mtakatifu. Ila nauliza ALIKWI? Alikuwa wapi?

Wadau, amani iwe kwenu.
Liwe jipu ama tambazi, kutumbuliwa kwake kunaambayana na maumivu makali. Hakuna mtu ambaye anachekelea namkufurahia wakati jipu lake linatumbuliwa. Uzoefu unaonesha kuwa watumbuliwaji wote wanatoa sauti kubwa ya mguguno na wakati mtumbuliwaji anafanya hivyo, jukumu la mtumbuaji ni kuendelea kutumbua na kukamua mpaka kiini kitoke. Akiacha kutumbua kwa kusikiliza sauti ya mtumbuliwaji basi zoezi linakwama na hali inakuwa mbaya sana.
Naam tumesikia sauti ya Lowasa akisema eti Rais Magufuli anawaonea wafanyabiashara waliounga mkono UKAWA. Hapo hapo Lowasa anatoa kauli kuwa wale wafanyabiashara waliounga mkono UKAWA watapata umbendeleo kwenye zabuni za manispaa ambazo UKAWA wanaongoza.
Makongoro Mahanga na Benard Membe nao wamelialia wakati majipu yao yanatumbuliwa. Wote ni katika kumshawishi mtumbua majipu asiendelee na kazi hiyo. Hata hivyo, kwa vile mtumbuaji amedhamiria kutumbua majipu yote na kutoa viini, kelele zao hazijasaidia.
Tutarajie kelele nyingi kutoka kwa watumbuliwaji. Hata hivyo, mtumbuaji amejivika ukiziwi na upofu hivyo hasikii wala haoni kelele zao mpaka kazi ya kutumbua majipu ikamilike
Jukumu letu wananchi ni kuendelea kumuombea kwa Mungu Muumba ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi.