Hiki kitakuwa nini?

Passed

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
561
156
Uwezo wangu darasani ni mzuri nipo chuo nilianza masomo mwaka huu semister ilopita matokeo yalikuwa na A mbili na masomo yaliyobaki nikapata B. Lakini hata hiyo mitihani ya hiyo semister nilifanya kwa mawazo kuna roho inakuja muda wote kwamba niache kitu ambacho sikifurahii na kinaumiza sana moyo msimamo wangu ni kwamba nataka kusoma.

Nikaamua kufunga maombi siku tatu nikimwomba mungu anisaidie kutatua ili tatizo ninaomba mawazo yenu tafadhali nataka tatizo liishe sihitaji liendelee kutawala akili yangu kwani maisha yangu ni magumu nikiacha chuo yatakuwa magumu zaidi
 
Pole sana mkuu...

Unakaa hstl au geto??

Vp aina ya marafiki zako wakoje????

Umewashirikisha wazee wako, kaka au mkuu wako wa kiroho???

Sali sana, Hakikisha hukai pekeako pekeako,
Uwapo mwenyewe Soma biblia .

Usiache shule, Ukifaulu kuliepuka ili,utakua umetusia !!!.
 
Kijana ulokole umekuharibu,
soma kwanza,
ukianza mambo ya kusema "roho inakujia"
nyie ndiyo wale mnakuja kuwa watu wa kushinda makanisani mkilia kama mazuzu,
sasa hapo sijui ndipo iweje.
hapo umeacha mambo yako ya msingi yakiharibika kwa kujifanya wewe unawajua sana mapepo na roho wachafu, kumbe wewe mwenyewe ndiye pepo.
Hayo mambo ya pepo mbona sisi wengine hayaji kujionyesha kwetu?
Mtu una matatizo ya uzazi mfano, unaenda kwa mchungaji njaa, anakujaza upepo kuwa umetupiwa roho na pepo la utasa,
hapo sasa badala uende kituo cha afya ukatibiwe, unakomaa kanisani ukisubiri miujiza.
Ujinga mtupu.
 
Asante
 
Sikai hostel may be inachangia na kukaa peke angu mda mrefu nikikaa na wezangu mawazo hupotea nikikaa tu peke yangu uanza tena yan mda wote inabid niwe na watu nimeomba kuamia hostel wamega kumejaa
 
Back
Top Bottom