Hiki kisa kimenisikitisha Mno, wazazi kizazi hiki kimeharibika, saidieni Binti zenu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
HIKI KISA KIMENISIKITISHA MNO, WAZAZI; KIZAZI HIKI KIMEHARIBIKA, SAIDIENI BINTI ZENU.

Anaandika, Robert Heriel

Mama mmoja amenipigia simu juzi, akanisimulia kisa hiki;
" Nina Binti yangu, nimemsomesha mpaka CHUO akamaliza shahada yake ya Kwanza Mwaka 2016. Hakurudi nyumbani akatomea Huko mjini. Akapata Mchumba, akanijulisha, nami nikawa namsisitiza amlete hiyo Mchumba nyumbani, Binti akaniambia atafanya hivyo. Nikaona miaka inaenda, nikawa namsumbua nikihofia anaweza kuchezewa akaachwa.
Binti akawa ananisisitiza niondoe hofu.
Mwaka Jana mwezi Nane akarudi nyumbani akiwa na mtoto mchanga WA miezi Saba hivi. Nikashtuka! Iweje anifiche Jambo kubwa kama Hilo. Baba yake akaja, Kwa kweli alikasirika mno"

" Baadaye tukamuuliza vipi Baba WA mtoto akasema wanaishi vizuri tuu, wanapendana na Maisha yanasonga hivyohivyo. Lakini Sisi wazazi tulikuwa tunamaanisha kuja kutoa Posa, akasema atakuja.
Ulipoisha mwezi Binti yetu akataka kuondoka, Mimi na Baba yake tukamzuia, tukamwambia kama huyo kijana hatokuja hutoondoka hapa nyumbani.
Binti akakasirika, lakini hakuwa na jinsi akatusikiliza.
Tukaweka kikao siku chache zilizofuata, tukamwambia Binti ampigie Huyo mwenzake amuambie msimamo wetu. Binti akapiga akaeleza tulivyomuagiza,
Kijana akasema Sawa"

" Lakini tukashangaa kimya, mwezi wa pili nao ukaisha, na watatu. Binti yetu akaanza kununa nuna, tukamwambia atuambie nini kinaendelea, Binti akatuambia kijana amesema Kwa sasa hawezi kuja, tukamwambia Kwa hiyo, akajibu hajui hata afanye nini.
Nikampandia hewani Yule kijana, nikamwambia vile alivyomfanyia Binti yetu, nikamuambia yeye aje tuu, nikamuambia Kwanza anatakiwa atoe Pesa ya adhabu ya kumzalisha Binti yetu Kabla ya kumuoa. Kijana hakuonyesha kukataa. Tukamalizana.
Tilikubaliana angekuja mwezi wa kumi na mbili katikati"

"Siku ilipofika, tukamuambia Binti vipi, amewasiliana na mwenzake, Binti akabako analia na kuanza kutulaumu wazazi.
Binti anasema, ati Kwa nini nimemtajia Pesa ya adhabu ya kumzalisha, ati nimemtajia Pesa nyingi"

Hapo Taikon nikauliza kwani ni kiasi gani cha Pesa ya adhabu ya kumzalisha ulichomtajia?
Yule Mama akanijibu;
" Nilimtajia milioni moja, yaani hapo ni adhabu pamoja na kumkomboa mtoto"

Taikon nikamuuliza; " hiyo ni nje ya Mahari?"
Yule Mama akanijibu, "Ndio"
Nikamuambia aendelee, akaendelea kusimulia;
" Binti yangu akasema, hiyo hela ni nyingi Sana. Alafu bado atoe Mahari, kweli Mama!!"
"Nikamwambia Kwa hiyo unamtetea huyo mjinga mwenzako? Sikiliza Binti yangu, tunafanya haya kwaajili yako"
" Binti akasema, kwaajili yangu Wakati mnaniharibia mahusiano yangu, kijana amesema hatakuja, Ila kama ninashida ya kwenda niende atanipokea"
" Nikasema, Kwa hiyo usipoenda, Binti akanijibu, unaniuliza Mimi tena"
"Nilikasirika Sana, Yule kijana hana adabu, nikamwambia Binti yangu, mwanaume sio yeye pekeake, wapo wanaume wengi tuu, utaolewa"
"Binti akasema, yeye anampenda huyo kijana, na wanaelewana vizuri. Nikamkatisha, nikamuambia, Mimi ndio mama yako hivyo nisikilize Mimi"
" Binti akasema, Mama sitaki kuzaa Watoto Kwa Baba tofauti tofauti, alafu Yule ndiye ninayempenda,
"Nikamuambia lakini yeye hakupendi, angekuwa anakupenda angekufuata hapa nyumbani na sio wewe kujipeleka,
" Binti akanijibu, tatizo ni hela Mama"
"Acha kutoa visingizio, sasa kama Hana Pesa mtaishije?"
Tukatishe kisa hiki.

Kisa hiki sio tuu kinasikitisha lakini kinatoa mafundisho yafuatayo;

1) Ni muhimu kufuata utaratibu wa kisheria, kimila na kiutamaduni unapoanzisha mahusiano Kabla mambo hayajawa mazito.

2) Wazazi wanatakiwa watumie nguvu kubwa kudhibiti mabinti kuishi na Vijana bila utaratibu Kabla mambo hayafika mbali. Kuliko yafike mbali ndio watumie nguvu, Hii inaweza sababisha Mabinti kubaki single mother na watoto kulelewa bila ya Baba na Mama.

3) Vijana ni muhimu Kabla hujaishi na Binti WA MTU, kwenda kwao kujitokeza angalau wakufahamu, hata kama hauna Pesa. Ikiwa unaona Binti anakupenda Sana. Ili kumfanya Binti ajisikie huru na aone hajawakosea wazazi wake.

4). Wazazi punguzeni kupenda Pesa, inagharimu mabinti wengi wa Zama za leo. Adhabu ya milioni moja ndio nini. Kwa Vijana wa siku hizi ninavyoelewa Akili zao hawawezi kutoa hiyo Pesa hata kama anayo.

5) Ushindani wa wanawake ni mkubwa Mno katika kuipata Ndoa, Ni muhimu wazazi wakaelewa Jambo hilo ili waweze kuwasaidia mabinti zao.
Huwezi mzuia Binti Kwa miezi sita nyumbani kwako ATI mpaka Mchumba aliyemzalisha aje nyumbani ilhali wapo Wanawake maelfu wanamsarandia kijana huyo.

6) Ni vizuri Wazazi kutoruhusu mabinti zao kwenda kufanya utafutaji wa Maisha mbali. Binti akimaliza CHUO arudi nyumbani, atafute mume aendelee na hatua zinazofuata.

7) wazazi wa Watoto wa kiume, msikubali kijana wenu aishi na Binti WA MTU kama hajafuata taratibu.
Msaidieni ikiwezekana kufuata utaratibu Kwa Ushauri, Mali na Hali.
Kuoa ni Jambo la kheri, kama wazazi mliweza kumsomesha nini kinawashinda kupeleka Posa Kwa kijana wenu?
Mbona zamani wazazi wa kiumeni waliwapa Vijana wao Pesa au Mali za kwensa kutoa posa?
Msiishie kuwalaumu vijana, wasaidieni.

Jamii ielewe kuwa, Vijana wa siku wakike Kwa wakiume wanaelewana, wanaongea Lugha moja ambayo ni tofauti na Lugha tunayozungumza Wazazi. Hiyo huchangia kudororesha mahusiano.

Binti anajua Maisha ya kijana anayempenda, anajua kazi yake, anajua kipato chake, anajua Ndugu zake.
Mchakato wa Kutoa posa Kwa baadhi ya jamii ni Mgumu mno Hali inayopelekea Vijana wengi kushindwa na mabinti wengi kuamua kuishi na washkaji kisela hivyohivyo Kutokana na upendo.

Jamii ielewe kuwa Vijana wengi ni Maskini na wametoka katika familia Maskini.
Kijana afikiri;
i) kumsafirisha mshenga Kutoka Mkoa X mpaka Mkoa Y. Hiyo ni Pesa.
ii) Kusafiri kwenda kutoa mahari, hapo kuna Mahari yenyewe na Pesa ya nauli.
iii) Kijana kama Kodi yenyewe haijai, anamsumbua mwenye nyumba, Kula yake ya kuvizia vizia ingawaje halali njaa, huyo ndio unataka umlaumu au umpige Faini ya milioni moja😂😂
iv) Kijana ambaye Hana kipato cha uhakika lakini wazazi wake wanampigia simu kila wiki awatumie angalau elfu 10 ndio huyohuyo unategemea aje atoe Mahari😀. Come on!

Wakati Unafikiri na kusema kijana huyo bado Hana uwezo wa kuingia ndoani Kwa sababu hajiwezi kiuchumi, lakini Binti yako anafikiri na kuona kuwa kijana huyohuyo kuwa ndiye Mume wake, na anampenda Kwa Moyo wake wote. Na Binti anaona huyo kijana anamaisha ya kuishi Naye, na ameridhia kuishi Naye katika Hali yoyote

Kwa Muktadha huo tunafanyaje kama wazazi?
Subiri,
Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mabinti ndo wajinga

iNatakiwa wakae na hao vijana ila wazuie kuwahi kujitagisha hovyo wakati muelekeo wa kijana hujaujua

Sasa wao wakichukuliwa na hao vijana hata mwezi hauishi tayar kesha jibebesha mimba
 
Mabinti ndo wajinga

iNatakiwa wakae na hao vijana ila wazuie kuwahi kujitagisha hovyo wakati muelekeo wa kijana hujaujua

Sasa wao wakichukuliwa na hao vijana hata mwezi hauishi tayar kesha jibebesha mimba

Tatizo la mwili wa Mwanamke siku yoyote anaweza Kupata Mimba.
Kilichopo ni Low chance, medium chance, na High Chance.
Siku pekee ambazo Mwanamke hawezi kutungisha UJAUZITO ni akiwa Period
 
Mimi naona mama Aliweka Tamaa sio Busara kwa Hatua iliyofikia ilibid tuu kijan ashinikizwe aje tuu kivyovyote vzr hayo yote angelezwa pale na wangeongea na kumalza swala vzr hatakam taratbu zngne zngebak
 
Wazazi watatulaumu Bure tu...hali zetu ngumu tumemaliza masoma hatuna hela...wanashindwa kupunguza mahali tukaoa kilichobakia ni mwendo wa kuviziana tu
 
Kalenda usiiamini Sana.
Siku yoyote Binti anaweza Kupata mimba, mwili wa Mwanamke unaweza Kubadilika ndani ya masaa 24.
Kuna mawili aidha umwagie nje, au utumie dhana za kuzuia mimba,
Vinginevyo kuna siku utaimba Hallelujah.
Mkuu p2 zipo mbona
 
Hayo yote mtaongea shida LIFE IS TOUGH NOWDAYS mahali zimepanda atari...bint kawa kitega uchumi..!!!
Hata kama ningekuwa mm ndio huyo kijana SIENDI NG'OOOOOOH..!!
 
Tatizo la mwili wa Mwanamke siku yoyote anaweza Kupata Mimba.
Kilichopo ni Low chance, medium chance, na High Chance.
Siku pekee ambazo Mwanamke hawezi kutungisha UJAUZITO ni akiwa Period

Si kweli, siku za kutunga mimba ni siku nne au tano tu,
Wakati yao la mwanamke linajengeka huwezi pata mimba na wakati yai lina anza kuharibika huwezi pata mimba ni sawa na Mwezi unavyo uona angani na tumbo la mwanamke la uzazi liko hivyo hivyo!
Kama untaka more information google!
 
Si kweli, siku za kutunga mimba ni siku nne au tano tu,
Wakati yao la mwanamke linajengeka huwezi pata mimba na wakati yai lina anza kuharibika huwezi pata mimba ni sawa na Mwezi unavyo uona angani na tumbo la mwanamke la uzazi liko hivyo hivyo!
Kama untaka more information google!

Mimba inatunga siku yoyote Sheikhe.
Ingawaje kikawaida(kisayansi) mimba inauwezekano mkubwa wa kutungwa siku ya Ovulation day ambayo Kwa Wanawake wengi huwa ni siku ya 14 tangu aingie P.
Kuanzia siku ya 11-17 Ipo High chance ya Kupata mimba.

Zingatia neno High Chance, Low chance na medium chance.
Siku pekee ambazo ni safe ni akiwa Period.
Ila siku zingine zote mimba huweza kuingia
 
Back
Top Bottom