Hii ya Malaysia Airlines ni maajabu tu

Hii ya Malaysia Airlines ni maajabu tu

Kuna mtu kaniambia na watanzania walikuemo, sijui ni kweli?
 
Leo ni siku ya nne, lakini hakuna alamu yoyote ya ndege ya Malaysia Airlines, haijulikani kama imedondoka au imezama baharini na kama ingezama mabaki yangeonekana au hata kama ingelipuliwa mabaki nayo yangebaki, sasa sijui imepotelea wapi! Kila nikifuatilia nakutana na still missing!

imepatikana mkuu..kitu hiko hapo
 

Attachments

  • 1898291_820244691324308_1798191310_n.jpg
    1898291_820244691324308_1798191310_n.jpg
    44.6 KB · Views: 1,047
Mkuu, mabaki ya Air France yalionekana baada ya siku moja tu ajali kutokea, na sio miaka miwili kama ulivyosema. Kilichoptikana baada ya miaka miwili ni black box kwani ilingukia takriban mita 4000 chini ya bahari. Just kuweka record sawa, kwani walimwengu wanashangaa maajabu haya ya sasa.
The Air France plane that crashed a few years back was found after 2 and a half years at the bottom of the Atlantic ( inside a deep trench of about 8 kms under the water). Siku nne sio kitu.
 
Dunia imekuwa uwanja wa mapambano haswa watu wanatafuta hela kwa kila njia, hawa jamaa wawili waliokuwa na passport fake lazima watakuwa ni engineers kwani la kwanza kufanya blackbox wameivuruga kabisa. Nafikiri hawa jamaa wameiiba hiyo ndege msishangae sana wait and see
 
.............Ninaamini kwamba unapoamua kupanda ndege kwenda kokote kule unakuwa tayari umejitoa muhanga kwa lolote linaloweza kutokea.... ukifikiri mara 2 unaweza kughairi kwamba inakuwaje nikae angani masaa 10 nafanya mambo yangu yote huko nakula nakunywa nalala... mara nyingine mnalazimishwa kulala mnagawiwa na mablanketi na taa zinapunguzwa mwanga ili mlale....:scared::deadhorse: :amen: :behindsofa:
 
Leo ni siku ya nne, lakini hakuna alamu yoyote ya ndege ya Malaysia Airlines, haijulikani kama imedondoka au imezama baharini na kama ingezama mabaki yangeonekana au hata kama ingelipuliwa mabaki nayo yangebaki, sasa sijui imepotelea wapi! Kila nikifuatilia nakutana na still missing!

Imechukuliwa na alliens
 
The Air France plane that crashed a few years back was found after 2 and a half years at the bottom of the Atlantic ( inside a deep trench of about 8 kms under the water). Siku nne sio kitu.

Actually, Miili na mabaki kidogo ya ndege yalipatikana soon after the crash but the main body of the plane and the black box took two and half years to recover.

As Air France crash showed, recovery can be long, daunting

Hii ya Malaysia Airlines ni strange sababu hata hayo mabaki kidogo hayaonekani.
 
Mi mwenyewe nashangaa haya maajabu, ndege kubwa vile kupotea tu ghafla haionekani popote kweli haya ni aajabu ya dunia.
 
Mwaka 1978 February; East Africa Airways walikuwa na dege kubwa la mizigo lililoitwa Simba. Rubani wake alikuwa Capt. Wilbert Urio, katika fani hii kuna vimbwanga kadha wa kadha kuna kisa kimoja anasimulia kwamba wakati wanavuka atlantiki instruments zote kwenye cockpit ziligoma kufanya kazi baada ya mwanga mkali kupita mbele yao na kuwaachia kiwi cha macho.



Ndege ilikosa nguvu na kuanza kushuka chini mdogomdogo mpaka tumbo la ndege likaguza maji ya bahari wakati huo walikwisha kata tamaa na kuanza kusali lakini ghafla kwa nguvu za ajabu ndege ikaruka kwa mruko usio wa kawaida mpaka kwenye attitude waliyokuwa wana i maintain na ghafla instrument zote zikaanza kufanya kazi na pia kwenye radar ikaanza kuonekana, baada ya kufika kwenye destination iliyokusudiwa salama ndege ilifanyiwa uchunguzi wa hali ya juu lakini hakuna dosari yeyote iliyoonekana.
 
Back
Top Bottom