Hii ya kutaifisha korosho Imekaaje??

Hii ya kutaifisha korosho Imekaaje??

Watu hawaelewi tu jinsi wafanyabiashara wanavyomkandamiza mkulima kwenye haya mazao ya biashara...
Serikali ilitakiwa itoe msaada kwa muda fulani ila serikali inakua haina pesa ndipo mkulima anapomwangukia mfanyabiashara anamletea korosho kiasi alizonazo anapewa pesa
 
Magufuri kweli jembe hapa amewaweza wale wanao penda kuwalalia wakulima kweli alimaanisha awamu hii akuna dili na wapiga dili awana nafasi safi sana mjomba magu japo sometimes unazingua lakini sio tatizo maana akuna binadamu aliyetimia ukimkera Huyu unamfurahisha mwingine sarut Mr President
Wewe umeandika tu, kwa sababu hujui maisha halisi ya wakulima, kuna wakulima hupata shida, huenda shida 1.milion ili apate kirahisi hizo hela, uhahidi kumpa kiasi kadhaa cha korosho.

Kwa mfano hivi sasa, wamewakataza wale wenye viwanda vidogo vidogo, vya kubangua korosho, wasinunue korosho, na kulipwa mpaka leo wengi hawajalipwa, shida zao wanazitatuaje.
 
Sawa mkuu halotel tunawapa pesa na kuwapa ajira vijana wetu na wao wakatupa dili LA kuwauzia korosho kwao lakini wafanyabiashara wa kitanzania wakajiongeza kuchanganya mawe na korosho ili wapate kilo nyingi mjomba acha kujazwa na story za magazeti na za humu kwenye mitandao waache serikali wafanye yao awataki kurudia kosa na hii serikali sio ya wapiga dili
Awamu hii wapiga dili ni wawili Tu, ndicho kitu kinachoumiza zaidi. Wameifanya Tanzania kama ni familia yao binafsi.
 
Hamna jambo kama ilo mjomba mambo yatakuwa mzuri tu kwa wakulima serikali ina dili na wafanyabiashara makajanja ambao waliwauzia waveitnam korosho zilizo changanywa na mawe
Mzee Baba ulivyokomaa na Vietnam hadi nakushangaa, unadhani wateja wa korosho ya Tz ni Vietnam Tu.
Kwa ufinyu wa akili yako umesahau kuwa Majaliwa alipewa kazi ya kutafuta wateja na wakapatikana, lakini One man Show akambadilikia !!
 
Natamani Kama wafanye hivyo na kwenye PAMBA,KAHAWA,KARAFUU,ALIZETI, KARANGA na DENGU
 
Ni kweli kuna baadhi ya watu account zao zmeshikiliwa mpaka watakopohakiki sehemu unayolima.Napozungumza wengine wameshakimbia kusini,unakuta kuna mtu amezalisha tani 30(abnormal)hivyo lazima wajue huyu mkulima anapatikana wapi ili kama unazalisha wakupongeze na kama umenunua wakufilisi.Kumbuka kuna wengine wamechukua mikopo na kuanza kununua,serikali inajua ikiwaachia wafanyabiashara hakuna mkulima atakayepeleka mzigo ghalani.Malipo yote yatakuwa kwa watu wa kangomba,ukiwa na mtaji kusini unatajirika kumbuka zaidi ya bil 700 zitalipwa hivyo watakaozilamba kutoka kwa wakulima ni wenye maduka ya Nguo,Ujenzi,chakula etc Ila wakulima wote watapata pesa kwani utaratibu wa ulipaji umebadilika hivyo subira muhimu.
Trust me, malipo kwa wakulima waliopeleka koro-show yatakuwa story kama za wastaafu was East Africa. Muda utaongea!
 
Sawa endeleeni kutaifisha korosho zisizotoka shambani, yaani zilizolimwa baharini

Nafikiri hujaelewa mantiki ya hili zoezi. Sikiliza hapa:
Serikali imekuja na mbadala wa kuwainua wakulima ili wafaidike na kilimo wanachokiendesha badala ya kuumia kwa jasho lao wenyewe huku wakilipwa ujira mdogo.
Kinachofanyika kwa madalali ni kuwafata wakulima na kuwalalia kwa kuwakopesha fedha wakati wa kilimo kwa makubaliano ya kubadilishana na korosho. Sasa mkulima anakopeshwa fedha halafu anaambiwa akivuna korosho basi kilo moja atakatwa 1500/= au 2000/= iwe ndio malipo ilihali mfanyabiashara akiichukua hiyo kilo moja yeye anakwenda kuiuza kwa sh 20000/= hadi 25000/=
Yes mfanyabiashara yeye anaangalia faida baada ya kutoa gharama zake zote lakini kiuhalisia huo ni unyonyaji na wizi mkubwa sana. Tofauti ni kubwa mnoo, kama mbingu na ardhi. Ndio maana JPM alipoongea nao akawaambia wafanyabiashara wakanunue korosho kwa 3000/= akijua fika kwamba hata wakija uza kwa bei zao watapata faida tu. Akawapa muda lakini wao wakadindisha, sasa akaamua achukue maamuzi magumu.
Uhalisia ni kwamba wengi waliochukua korosho ni madalali, wapo hata wafanyakazi wa serikali ambao walifanya michezo hiyo. Sasa serikali nia yake ni kuwainua wakulima ambao ndio wahanga wakuu, hivyo ikaja na mikakati hiyo. Kama wewe ni mkulima kweli, basi kaonyeshe shamba then serikali itanunua hiyo korosho yako. Tatizo liko wapi?
Kwa wale msiojua, kuna korosho nyingi sana inaingia pia kutoka Msumbiji, ambayo nayo ikifika Tanzania inadakwa na madalali, sasa bila ya kufanya scrutiny hiyo manake ni kwamba serikali itawafaidisha watu wengine na walengwa kukosa, lengo halitatimia.
Nakubaliana na mawazo kwamba kama mtu kashindwa kuonyesha shamba basi labda serikali isingenunua korosho zake lakini pia isimnyang’anye, imwache nazo akahangaike mwenyewe huko mbele kwa mbele. Lakini pia ukitaka kukomesha vitendo vya dhuluma, wakati mwingine ni lazima kuja na mikakati itakayowafanya watu wasitende tena vitendo hivyo, na ndio hiyo sasa ya kuwanyang’anya korosho ambazo wengi wamezipata kwa kuwalalia wakulima.
Kuna mwaka wakulima walilipwa bonus pia baada ya kuwa wameshalipwa fedha za korosho na baadae vyama vyao vya msingi vilipouza korosho vikapata faida na kuwalipa bonus wakulima.
Hii saga usipoongea na wakulima wenyewe na madalali pia, huwezi elewa na ukaishia kulaumu serikali but ukweli uliopo ni tofauti sana.
 
Trust me, malipo kwa wakulima waliopeleka koro-show yatakuwa story kama za wastaafu was East Africa. Muda utaongea!
Usisikilize maneno ya vijiweni,Mimi mpaka Leo sijalipwa ila Majina yangu ya vyeti 5 nimehakiki na nitalipwa wiki ijayo.Ninapozungumza pesa ishaanza kumwagika Vijijini,Mimi hata nikilipwa siwezi kuwaambia watu cze vizinga vitaongezeka.Hivyo kuna wengine kulalamika ndio mtindo wa kuepuka kuombwa pesa.Kuna ndugu na jamaa ukiwatangazia umelipwa mil 20 basi lawama na kuombana mitaji kunaanza.Mfano mzuri wastaafu wengi nao hawatangazi wakipewa pesa kuepuka lawama
 
Hamna jambo kama ilo mjomba mambo yatakuwa mzuri tu kwa wakulima serikali ina dili na wafanyabiashara makajanja ambao waliwauzia waveitnam korosho zilizo changanywa na mawe
msimu huo uliokwisha serikali baada ya kuchukua ile export levy umejua nini kimetokea??ulisikia kuna bei ya pembe jeo ilivyokuwa kubwa ni wangapi walizinunua?
 
Wewe umeandika tu, kwa sababu hujui maisha halisi ya wakulima, kuna wakulima hupata shida, huenda shida 1.milion ili apate kirahisi hizo hela, uhahidi kumpa kiasi kadhaa cha korosho.

Kwa mfano hivi sasa, wamewakataza wale wenye viwanda vidogo vidogo, vya kubangua korosho, wasinunue korosho, na kulipwa mpaka leo wengi hawajalipwa, shida zao wanazitatuaje.
Hawajakataliwa kununua korosho bali wanunue kwa bei ya mnada.angalia clip kwenye utube kuna mtu anaitwa nafikiri asineni akiongea
 
Magufuri kweli jembe hapa amewaweza wale wanao penda kuwalalia wakulima kweli alimaanisha awamu hii akuna dili na wapiga dili awana nafasi safi sana mjomba magu japo sometimes unazingua lakini sio tatizo maana akuna binadamu aliyetimia ukimkera Huyu unamfurahisha mwingine sarut Mr President
Hujui usemalo chunguza / uliza
 
Kilichotakiwa kwa serikali ni kununua tu korosho kama kuonewa wakulima wenyewe ndio wangelalamika na tena hasa kama walilaliwa
Mi ninashamba ...sina pesa za kulihudumia...nikijakwako ukaniwezesha then tukakutana kwenye mavuno kunaubaya?
 
hamna mjomba ni maamuzi tu magumu yamefanyika inshu ilikuwa hivi kuna dili lilifanyika kati ya Tanzania na vetinamu sisi tuwauzie korosho wao walete hallo tel sasa kilichofanyika wajanja wakijiongeza kuenda kununu korosho kwa wakulima kwa bei rahisi na hizo korosho wakachanganya namawe kuwauzia was vetinam hivi kwa mfano kama ndio kiongozi ungejisikiaje
Ningezikagua kabla ya
 
Ningeomba wakulima wa koroshow ndio waje kutupa majibu ya maswali yetu. Maana hata mimi nina maswali mengi tu.[emoji18] [emoji53]

Kuna wapo wanaolalama hawajalipwa mpaka sasa, wakati serikali imesema wameshalipwa (lakini kwa waliokua hawana mashamba imekula kwao).
Bado wanahakiki hakuna alielipwa pesa ya serkal. ,,,ila kuna mnada ulifanyika kwa 2700, hawo ndo wamepata visent wengine wote wapo hoi kololoo
 
Magufuri kweli jembe hapa amewaweza wale wanao penda kuwalalia wakulima kweli alimaanisha awamu hii akuna dili na wapiga dili awana nafasi safi sana mjomba magu japo sometimes unazingua lakini sio tatizo maana akuna binadamu aliyetimia ukimkera Huyu unamfurahisha mwingine sarut Mr President
Usilolijua
 
Hii biashara ya Kangomba inafaida kwa mkulima na ukiidhibiti mkulima ndo ataumia zaidi,,, mfn mkulima anaanza kuvuna mwanzon mwa October ,,,shughuli za uvunaji zina gharama yake ,,,na maandalizi ya msimu yana gharama ,kama kununua madawa na mbolea,, ko mkulima anahitaji fedha kwa wakati ili mambo yaende,,,,mfumo unaotimika na wanunuzi halali ni wa stakabadhi gharani,, hawatoi pesa cash
 
Duu!!!!!!kangomba inafaida kwa mkulima?????
Sema tuboreshe stakabadhi ghalani au ushirika boss !!
 
Duu!!!!!!kangomba inafaida kwa mkulima?????
Sema tuboreshe stakabadhi ghalani au ushirika boss !!
Hao wanaotaifisha umesikia wanazungumzia kuboresha?.. Unazani hawajui hali halisi,, unauza na kusubir mauzo kwa zaid ya miez 2,, what do u expect,?,, kwa situation iliyopo haiepukiki,,
 
Back
Top Bottom