Hii ya kuoa Maiti imeshapitwa na wakati

Hii ya kuoa Maiti imeshapitwa na wakati

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Posts
4,291
Reaction score
14,787
Imetokea sintofahamu hapa mtaani kwetu jamaa alikuwa anaishi na mwenza wake sasa mwenza amefariki ndugu wamekuja juu wanataka aoe maiti.

Siku zote hizo mlikuwa wapi kwenda kudai Mahari mpaka mnasubiri mtoto wenu afe ndio muje muanze kusumbua mfiwa?

Hii desturi imekaa kizamani, kwani akishalipa hizo Pesa mtoto wenu ndio atafufuka?

Tuwe tunadai vitu watu wakiwa bado hai, na kama ilishindikana wakiwa hai basi ihesabike imekula kwenu wazazi.

Na nyie vijana hakikisheni basi mnatoa hata Posa ili nyumbani angalau wakufahamu kuliko kuja kuaibika mbeleni.
 
😀😀😀😀 Mkuu vyuma vimekaza kila mahali, jamaa anakuwa anasubiria hali ibadilike na hayo yanatokea.
 
Akome,acha adaiwe,kwanini hakutoa mahari wakat mzima? Alipuuza mila na desturi.Mwache apate taabu aliyataka mwenyewe
 
Akome,acha adaiwe,kwanini hakutoa mahari wakat mzima? Alipuuza mila na desturi.Mwache apate taabu aliyataka mwenyewe
Tatizo hiyo pesa anapata wapi...maisha yenyewe haya....hakuna asiyependa kuoa Kama mfuko unaruhusu...
 
Atajua,unakuta kakaa na dada wa watu zaidi ya miaka 5,liwe fundisho kwa wengine,ndugu wamchangie na asilete uhasama hizo ni mila na desturi.
 
nikiwa na mtoto wa Kike, ataolewa bure, wao wataamua watakachokileta kama familia.
Mahali isitupeleke kwenye Modern Slavery.
kwanza mahali ni ZAWADI, huwezi kulilia zawadi.
 
nikiwa na mtoto wa Kike, ataolewa bure, wao wataamua watakachokileta kama familia.
Mahali isitupeleke kwenye Modern Slavery.
kwanza mahali ni ZAWADI, huwezi kulilia zawadi.
Bure hapana mkuu, (hii naona kama tusi kwa bint yako)
Labda bint mwenyewe aseme Naenda kwa mwenzangu ila hana kitu akipata ataleta na wewe baba ndio uridhie.
Lakini sio kumwambia nakuozesha bure.
 
Bure hapana mkuu, (hii naona kama tusi kwa bint yako)
Labda bint mwenyewe aseme Naenda kwa mwenzangu ila hana kitu akipata ataleta na wewe baba ndio uridhie.
Lakini sio kumwambia nakuozesha bure.
hapo ni suala la mtazamo na kiutamaduni zaidi sio uhalisia.
ukimuelimisha.
Form two, kwenye Home economics tulifundishwa Mahali (dowry) ni mfumo wa zawadi inayotolewa na anayetarajiwa kuoa au wazazi wake kwenda kwa wazazi wa binti.

Point yangu zawadi isiwe kama kodi, au nauli au lazima.
Ikiwa wao wataona kuna ulazima au uwezo wa kutoa zawadi ni jambo jema, ila wakiona wahawezi au uwezo hawana ni jema pia.
hapo sioni tusi kwa binti maana mahali hapewi binti anapewa mzazi wake mimi. Yeye hausiki.
ingawa niliwahi kugusia hilo kwa mama watoto akageuka mbogo hahahaha
 
Mahali ni udhalilishaji wa kiwango cha Lami
 
hao ndungu ni wakucharazwa viboko, badala ya kuwaza msiba wanawaza pesa
 
Back
Top Bottom