Hii ya kulipa ili utumie daraja la Kigamboni, itakimbiza Wabongo, subirini muone!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Eneo la Daraja la Kigamboni ambalo linakaribia kumalizika, Daraja linapendeza lkn kuna hii kitu hapo chini yaani kulipia kulitumia, hapa ndipo shida ilipo kama kuna waliotegemea kwamba Kivuko cha Pantoni shilingi kadhaa kitapumua sasa, basi wafikire tena, hakuna mbongo atatia mguu kwenye hili daraja, muda utaongea!

IMGS6733.JPG

IMGS6736.JPG

IMGS6700.JPG
 
Kwani tozo ni sh ngapi?!
 
Ukumbuke kwamba wanaelipa ni wenye magari tu,kwani pantoni gari hawalipii? Wewe wa wapi?

Hata hao wenye magari watalikimbia tu subiri utaona, sehemu kubwa watarudi kwenye pantoni na hapo yatabakia magari SU, ST, CD na mengineyo!
 
nasikia upande wa kigamboni hakuna barabara ya kuliunganisha na barabara zingine!
Nafuatilia kwingine duniani kujua kama kuna muundombinu unaojengwa kwa pesa ya umma alafu wananchi wanaamuliwa kuulipia, basi hata Japan na Marekani wangejenga vijumba vyao kwenye barabara zote walizotukopesha pesa ili wawe wanatoza ada kurudisha pesa zao.
 
Ukiwa na haraka utalipia tu, kwani bei gani hata washindwe?

Sijui tozo ni ngapi lkn inapaswa kukusanywa fedha ambayo itatumika kuliendesha Daraja, sasa hapo unaweza tu kukadiria itakuwa ni kwenye maelfu!
 
Hata hao wenye magari watalikimbia tu subiri utaona, sehemu kubwa watarudi kwenye pantoni na hapo yatabakia magari SU, ST, CD na mengineyo!
Sijui ni utaratibu gani utakao tumika, lakini kwenye nchi zenye utaratibu kama huo, unalipia mara moja tu kwà siku, yaani tiketi inakaa kwa masaa 24 ndio ina expire
 
Ukumbuke kwamba wanaelipa ni wenye magari tu,kwani pantoni gari hawalipii? Wewe wa wapi?
Hata wasio na magari watalipia acha kuwa na mawazo mafupi. wasio na magari watalazimika kupanda mabasi yatakayopita hapo nauli itakuwaje? hapo mmepigwa changa la macho. Au utatembea kwa mguu toka posta ukavuke bure kwa mguu
 
Sijui ni utaratibu gani utakao tumika, lakini kwenye nchi zenye utaratibu kama huo, unalipia mara moja tu kwà siku, yaani tiketi inakaa kwa masaa 24 ndio ina expire

Sidhani kama hilo ni tatizo, hata kama ikiwa kwa wiki au mwezi ila tatizo nifedha yenyewe kuipata ya kulipia hapo ndipo ishu ilipo, hivyo basi wengi wataendelea kubanana tu kule kwa kajamba nani kwenye Pantoni yetu!
 
Too bad to make generalization as if your are in the pockets of others,the matter of affording or not is something personal.
 
Too bad to make generalization as if your are in the pockets of others,the matter of affording or not is something personal.

Hahah mimi nimezaliwa na kukulia hapa hapa Bongo hivyo nawajua ndugu na jamaa zangu wa Kibongo, mtu kuendesha gari siyo kama ana hela, nina washikaji wengi tu nawajua wana magari lkn hawana hela, anaondoka nyumbani asubuhi na mafuta ya kwenda tu anapitia Sheli anajaza na kurudi itajisoti jioni, hivyo najua ninachokiongea, na muda utaongea sio mbali sana!
 
Back
Top Bottom