singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
NI daraja la aina Afrika Mashariki na Kati hasa ikizingatiwa kuwa limejengwa juu ya bahari, ni faraja na fahari kwa Watanzania kwa kuwa limepewa jina la Baba wa Taifa, Julius Nyerere. Rais John Magufuli amelizindua Aprili 19. Lina urefu wa mita 680, barabara sita, tatu zikitoka Kigamboni kwenda Kurasini na tatu kutoka Kurasini kwenda Kigamboni. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, muundo wa daraja kama hilo hujengwa nchi za nje tu, lakini sasa limejengwa Tanzania.
Anasema, ujenzi wa daraja hilo umehusisha mabomba tofauti na madaraja mengine katika nchi za Afrika, na ni wa kipekee. Daraja hilo ni mkombozi kwa wakazi Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa kuwa litasaidia kukuza uchumi, kupunguza tatizo la msongamano na kumaliza kero ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni.
Rais Magufuli anasema, daraja hilo lina uwezo wa kuhimili uzito wa takribani tani 1,300 na litatumika kuunganisha barabara kadhaa zitakazokuwa na barabara za juu kwa pande zote za Kurasini na Kigamboni, ikiwemo barabara ya haraka ya Kigamboni-Chalinze.
Anasema, wakazi wa Kigamboni wana bahati kwa kuwa wataunganishwa na barabara ya Chalinze-Kigamboni, itakayokuwa na barabara za juu takribani tano ambazo zitakuwa katika maeneo ya Tazara, Ubungo, Kurasini, Mlandizi na Chalinze. Daraja hilo limejengwa kwa ubia kati ya Serikali na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). NSSF imechangia asilimia 60 ya fedha za ujenzi, Serikali imechangia asilimia 40.
Anasema kutokana na uzuri wa daraja hilo, maharusi watependa kupiga picha hapo. Rais Magufuli ametaka daraja hilo la kisasa liitwa Nyerere ikiwa ni moja ya njia ya kuenzi jitihada za kiongozi huyo katika kuwaunganisha Watanzania bila kujali tofauti za dini, rangi au makabila yao. Rais Magufuli anasema, aliombwa daraja hilo lipewe jina lake (Magufuli) lakini yeye hastahili kupewa heshima hiyo ila Baba wa Taifa.
“Jamani mimi kwanza jina langu hili la Magufuli si zuri, wala halitii raha, kama mtaniruhusu naomba tuliite Daraja la Nyerere,” anasema Rais Magufuli. “Nafikiri kama Wizara ya Ujenzi itakubali kutokana na historia ya daraja hili, wapo viongozi wetu waliofanya makubwa, waliunganisha watu zaidi ya makabila 200, tukapendana bila kubaguana kwa vyama, rangi, lugha wala dini...na daraja hili halitabagua mtu wa kupita, halitabagua CCM wala Chadema, wote hawa watapita,” anasema Rais Magufuli.
Anasema, wazo la ujenzi wa daraja hilo lilianzia tangu miaka ya 1930 na baadaye katika kipindi cha uongozi wa Mwalimu Nyerere mwaka 1971. “Nampongeza sana Rais Kikwete na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau kwa jitihada zao katika kufanikisha ujenzi wa daraja. Niseme ukweli Dk Dau amefanya makubwa katika daraja hili, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,” alisema Rais Magufuli.
“Nafikiri wote mnaliona daraja hili linapendeza, lakini pia ni bora na imara ninawahakikishia litadumu kwa miaka 100. Ndio maana hata jirani zetu wameanza kusema lipo kwao jamani na sisi Watanzania tujivunie na vyetu. Tujivunie daraja hili, ukipiga picha sasa hivi utafikiri uko Ulaya,” anasema Rais Magufuli. Anasema, kulikuwa na changamoto za ujenzi zilizosababisha matumizi makubwa ya fedha.
“Kuna watu wameanza kuwa mainjinia (wahandisi) utasikia wanasema daraja limejengwa vibaya sijui wapi hakujawekwa njia, jamani si mngejenga la kwenu tuone,” anasema. “Jamani mtu unaposikia daraja limejengwa kwa Shilingi bilioni 214 halafu useme fedha zimeibwa ni kwamba umeshindwa kuelewa. Hivi tunashindwa kufikiri kidogo tu, wakoloni walishindwa kulijenga lakini leo weusi wenzetu wamejenga eti wameiba?” Anasema Dk Magufuli.
Anawataka Watanzania kujivunia na vitu vyao na kuvisifu kwa kuwa wasipofanya hivyo hakuna mtu atayewasifia. Anasema wananchi watakaolitumia watatozwa fedha ili kufidia gharama kubwa za ujenzi. Anasema kwa sasa fedha hazitotozwa kwa watu wenye ulemavu na watembea kwa miguu. Anasema watu watakaotozwa malipo ya matumizi ya daraja hilo ni wenye magari pikipiki, guta, pikipiki ya matairi matatu (bajaj) na baiskeli.
“Nafahamu kuwa wakazi wa Kigamboni mmepata adha ya muda mrefu ya usafiri, wapo waliopoteza maisha kutokana na matumizi ya mitumbwi pindi usafiri wa kivuko unapokwama. Sasa hivi jamani kuna daraja hili tena la bure, miguu yako tu. Ngoja hivi vivuko vikarabatiwe,” anasema Rais Magufuli. Anasema, daraja hilo linatarajia kuajiri wafanyakazi takribani 300, lakini pia litatumiwa na wakazi wa Dar es Salaam hususan wakazi wa Kigamboni.
Amewaomba wananchi walitunze na kulithamini. “Kwa hili nitakuwa mkali, naomba vyombo vya ulinzi msimamie kikamilifu ikibidi mtu yeyote atakayegonga hata taa atozwe faini kubwa ili kujenga heshima ya mali za umma. Lakini pia naomba mzingatie suala la usafiri. Ni marufuku biashara kufanyika pembezoni mwa daraja hili,” anasema.
Aliihimiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha inakamilisha barabara nyingine zinazounganisha daraja hilo, ikiwemo barabara za juu za upande wa Kurasini na upande wa Vijibweni ili kuwarahisishia usafiri wakazi wa Kigamboni. “Fanyeni haraka kupanua barabara ya Rangitatu-Gerezani, kukamilika kwa daraja hili lazima sasa kuwe na mipango wa haraka wa kuwapunguzia wananchi safari ndefu,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara anasema, hadi kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo gharama za ujenzi ni Dola za Marekani 135 na asilimia 25 inalipwa kwa fedha za Kitanzania na nyingine asilimia 75 inalipwa kwa fedha za kigeni. Hivi karibuni Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu ilitembelea daraja hilo.
“Ubora wa daraja hili pamoja na muda uliotumika kujenga tumeridhika kabisa, lakini mharakishe kukamilisha hatua zilizobaki ili kuipa heshima Serikali ya Magufuli na pia wananchi wapate unafuu wa usafiri,” alisema Sigalla. Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF, Karim Mataka ameieleza kamati hiyo kuwa, daraja hilo lililojengwa kwa ushirikiano kati ya shirika hilo na Serikali lina urefu wa mita 680 na upana wa mita 32.
“Ujenzi wa daraja hili umefanywa na kampuni ya China Railway Constration Enginering Group ikishirikiana na China Major Bridge Engeneering kwa takribani miezi 51 kwa gharama ya Sh bilioni 214.6 na msimizi wa daraja hilo gharama yake ni Sh bilioni 7,” anasema Mataka. Mataka anasema daraja hilo linahusisha mihimili ya chini 202, vitako vya juu ya mihimili ya chini, nguzo fupi 20, sehemu ya daraja iliyoungana na barabara ya lami, daraja kuu na nguzo ndefu.
Daraja hilo lina barabara za maingilio zenye urefu wa kilometa 2.5 ambazo zimekamilika kwa kiwango cha zege la lami. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Joseph Nyamhanga anasema kwenye eneo la daraja hili kuna kituo cha Polisi ambacho kitakuwa na mahabusu. “Kituo hicho tutakuwa tunakamata watu ambao watakuwa wakorofi wasiotaka kutii sheria hivyo kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa daraja,” anasema Nyamhanga.
Katika daraja hilo pia kutakuwa na mizani ya kupima magari ya kubeba mizigo yatakayokuwa na njia ili yasisababishe foleni kwa magari mengine. “Daraja hili pia litakuwa na ofisi mbalimbali, kamera kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa daraja, tutakuwa na watu wa usafi muda wote kwa sababu daraja hili litakuwa la kimataifa na la mfano na pia kutakuwa na vyoo ambavyo vitakuwa vya kulipia,” anasema Nyamhanga.
Anasema ili daraja hilo liweze kuwa na ufanisi ni pamoja na ujenzi wa upanuzi wa barabara zinazopokea na kuleta magari darajani kama vile ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara yenye urefu wa kilometa 1.5 kwa upande wa Kigamboni.
Ufanisi mwingine utatokana na upanuzi wa barabara ya Vijibweni- Mjimwema, upanuzi wa barabara ya Feri-Kibada, upanuzi wa barabara ya Bendera Tatu-Kamata ambayo inatarajiwa kufanyika kwa udhamini wa Serikali ya Japan. “Pia Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itagharimia ujenzi wa flyover za Uhasibu na Chang’ombe chini ya awamu ya pili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka,” anasema Mataka.