Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimetafakari sana juu ya hii Serikali ya CCM inayodai ipo kwa ajili ya wananchi, hasa wanyonge. Na hakuna mtu anakaebisha kwamba Kigamboni kuna hao wanyonge wengi tu.
Sasa kwanini hawa wanyonge wa Kigamboni walazimishwe kutoa fedha kwa kutumia daraja la Nyerere kwenda Kigamboni? Tunajua kwamba hata ukienda Kigamboni kwa daladala bado unalipa kutumia daraja hili. Huu ni ubaguzi unaofanywa na Serikali kwa wananchi wa Kigamboni na haukubaliki hata kidogo.
Daraja la kwenda Kigamboni ni huduma ambayo serikali inapaswa kutoa kwa wananchi wake, sawa tu na kujenga daraja la Mkapa ili kuwahudumia wananchi kwenda Rufiji, au daraja la Mto Wami kwa wananchi wanaokwenda mikoa ya Kaskazini.
Sasa kama wale wanaovuka daraja la Wami kwenda Arusha, au Rufiji kwenda Lindi, au hata Ruaha kwenda Iringa - kama hawa hawatozwi fedha kuvuka haya madaraja, kwa nini wananchi wanaokwenda Kigamboni watozwe fedha?
Suala la kusema wananchi wanalipa kwa kuwa serikali inamiliki 40% na NSSF 60% halina mantiki. Serikali inapaswa kuwalipa NSSF hizo 60% ili daraja hili liwe ni mradi wa serikali ambao ulijengwa ili kuwahudumia wananchi, kama vile madaraja mengine ya Mkapa, Wami nk.
Na tusisahau kwamba katika kila lita ya petroli au dizeli tunayonunua, kuna tozo kwa ajili ya Tanroads kujenga vitu kama haya madaraja, flyover na barabara na kuzifanyia ukarabati, juu ya fedha inayotengwa na serikali na misaada kwa ajili ya miradi ya Tanroads. HUiyo basi, kuwa na tozo la daraja la KIgamboni ni sawa na kuwatoza wananchi road toll mara mbili, kinyume cha sheria za kodi.
Ninatoa wito serikali ikomoshe ubaguzi huu kwa kuwafanya baadhi ya Watanzania walipie huduma ya kutumia daraja na wengine wasilipie. Hakuna mtu anakwenda Kigamboni kwa upendezi wake (personal interest), kwa hiyo kuvuka daraja hili hakupaswi kuwa huduma ya kulipia ikiwa kutumia madaraja mengine hatulipii.