longalonga
Member
- Aug 22, 2007
- 17
- 2
Ndugu Zangu wana JF siku zote nimekuwa ni msikilizaji tu wa mambo humu ndani zaidi ya kuchangia threats zinazowekwa na wanamapambano wenzangu.
Labda nianze kwa kusema kuwa wengi wenu mnaifahamu vizuri ishu ya uchukuaji na uthaminishaji ardhi kwa wananchi wa kibamba,binafsi naipongeza serikali kupitia mipango miji kwa kutaka kuanzisha satelite city eneo la kibamba kwani hii pamoja na mambo mengine itasaidia kupunguza mrundikano wa shughuli zote katikati ya mji kwa sababu kulingana na masterplan niliyoichungulia nimeona hata stendi kuu ya mabasi itahamia huko pamoja na central facilities zote.
Tatizo lililonikera sana ni juu ya uthaminishaji na ulipaji wa fidia kwa wananchi ambao wamefanyiwa eviction hii kwa kweli imenisikitisha sana, mimi si mmoja wa waliokumbwa na mkasa huo na wala siishi maeneo hayo ila nimeshindwa kulifumbia macho kabisa.Kwa ufahamu wangu finyu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 na Town Planning Ordinance serikali ikiamua kuchukua ardhi(acquisition)basi wananchi walio eneo hilo hukadiriwa malipo kulingana na bei iliyopo kwenye soko kwa muda huo.Chaajabu nikuwa pamoja na wathamini ardhi ambao wamesomea taaluma hiyo kufanya uthamini ambao ni Tsh 3000/= kwa mita moja ya mraba, serikali ilipangua uthamini huo na kupunguza hadi kufikia pungufu ya sh 500/=ambayo ni valuation rate ya miaka mingi iliyopita,na hivyo kuwanyonga sana wananchi ambao walikuwa na mategemeo makubwa kulingana na bei ya soko,mtu badala ya kulipwa lets say million thelathini (30,000,000/=) mtu analipwa chini ya milioni tano.(5,000,000/=).Eti wizara wanajisifu kuwa wamesave zaidi ya billion moja sijui ni kwa manufaa ya nani.
Hivi leo asubuhi jopo lote la wizara magufuli inclusive linaenda kibamba kuongea na wananchi baada ya kitimoto kikali sana jana wizarani.
Mimi kwa mtazamo wangu wana JF hili jambo si la watu wa kibamba tu, tusilifumbie macho hata kidogo sababu hii ardhi kwa sera zetu tumepangishwa tu, leo ni wale wa kibamba kesho ni sisi,serikali wataendelea kujineemesha kupitia migongo yetu daima.
Dodoma nao wanafuatia nina hakika wao ndo itakua worse kabisaaa.
Naomba Kuwasilisha.
nauunga mkono mpango wa kujenga satelite city kimara ..nasikia inakuwa wilaya ya KIMARA...tayari kuna chuo kikuu cha muhimbili wametoa tenda ya michoro kwa ajili ya chuo kikuu pale...pia catholics wana chuo kikuu pale cha st joseph engneering..so many prospects eneo lile hongera magufuli na rais wako jk....
nimetembea duniani nimeona miji inayojengwa kwenye vilima kama vya kibamba ..huwa inakuwa na scenery nzuri sana sana...tena kama wataweka open space za kutosha....pia napendekeza kibaha mjini iwe sehemu ya hii satelite city na makao makuu ya mkoa yahamie chalinze ,...pale wilaya ya kibamba makao makuu yawe kibaha mkoani....kuna barabara pia ya kufika bagamoyo toka kibamba ..another destination of satelite city....
lakini pia kuna umuhimu wa watu kulipwa kihalali...
Hapo kuna ulazima wa sheria za ardhi kuwekwa bayana... sheria nyingi na kanuni mbalimbali zimeendelea kufaidi vumbi makabatini. Ni kuziuja sheria hizo na kanuni, kwani itasaidia kuondoa dhuluma na aina zingine za ufisadi.
Kwa ufahamu wangu finyu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 na Town Planning Ordinance serikali ikiamua kuchukua ardhi(acquisition)basi wananchi walio eneo hilo hukadiriwa malipo kulingana na bei iliyopo kwenye soko kwa muda huo.Chaajabu nikuwa pamoja na wathamini ardhi ambao wamesomea taaluma hiyo kufanya uthamini ambao ni Tsh 3000/= kwa mita moja ya mraba, serikali ilipangua uthamini huo na kupunguza hadi kufikia pungufu ya sh 500/=ambayo ni valuation rate ya miaka mingi iliyopita,na hivyo kuwanyonga sana wananchi ambao walikuwa na mategemeo makubwa kulingana na bei ya soko,mtu badala ya kulipwa lets say million thelathini (30,000,000/=) mtu analipwa chini ya milioni tano.(5,000,000/=).Eti wizara wanajisifu kuwa wamesave zaidi ya billion moja sijui ni kwa manufaa ya nani.
Ningependa kuwauliza, hivi DSM itaendelea kupendelewa mpaka lini?
Msongamano wa DSM hauwezi kupungua iwapo miji mingine haipewi kipa umbele. Kwanini mradi mzima usipelekwe Tanga, Mwanza, Mbeya au Bukoba.
Cha kushangaza zaidi ni kuwa wanaopanga mipango hiyo, wanatoka mbali na DSM na hata siku moja hawafikiri kuwa sehemu walizotoka zinahitaji miji vilevile.
Wewe bepari kweli? Tangu lini katika mfumo uupendao serikali ikamuamulia mwekezaji mahali pa kuweka? Unaamini kweli huko uliko Bush anaweza kumuamrisha Toyota mahali pa kujenga kiwanda?
Katika ubepari miji inajengwa kwenye uzalishaji. Ukuaji wa DSM unatokana fikra potofu za Ujamaa ambavyo mapato yote ya nchi ni lazima yaendee DSM na baadaye kuanza kugawiwa. Hivyo ata mji usiozalisha unakuwa na access sawa ya mapato kama sehemu zenye uzalishaji.
Vile vile serikali ikiweka mazingira ya miji mingine kuwa mazuri wawekezaji watakwenda huko.
Katika ubepari wa kimarekani, miji inajengwa na mabepari (wawekezaji) kutokana na vivutio ambavyo wenye sehemu wanatoa. Angalia historia ya Las Vegas uone kama kuna mkono wa federal government pale! Kwa misingi hiyo, serikali haiwezi kuwaamulia mabepari wapi kwa kuwekeza bila kuweka vivutio. Huko uliko. states zinashindana kwa kuweka vivutio ili vivutie wawekezaji sio kutoka nje ya nchi tu bali hata kutoka state nyingine. Kama tunataka tuwe hivyo, inabidi mikoa yetu ianze kushindana yenyewe na kila mmoja ijitahidi kuweka vivutio bila kusubiri serikali kuu. Serikali kuu na yenyewe inabidi iachie baadhi ya mamlaka yake ili mikoa ipate uwezo zaidi wa kujiamulia yenyewe.Tatizo ni kuwa watu wataona tunaelekea kwenye majimbo. Tukirudi kwenye mada hii, inaelekea hapa mwekezaji(wenyewe wanamuita mfadhili) ameishapatikana na kinachogomba ni hiyo fidia. Hiyo ikitatuliwa jamaa anamwaga vitu na Dar inapata Manhattan yake! Wengi wetu watafurahia hilo wakiona hayo ndiyo maendeleo lakini ukweli ni kuwa kwa mara nyingine tena tutakuwa tumeweka rehani vizazi vijao kwa uroho wa makombo wanayotutupia hao tunaowaona ni wafadhili wetu!
Las Vegas ni Jangwani na kama kusingekuwepo na interstate au airport, ni bepari gani angeenda huko? Miji kama vile New York, Washington DC ikionyesha miradi ya Mass Transit yenye kuhudumia kiasi fulani inapata msaada kutoka Federal.
Bepari aliyeenda huko wakati kalikuwa kajimji tu anaitwa Bugsy Siegel ambaye alikuwa mshiriki wa Lucky Luciano na Meyer Lansky. Huyu na wenzake ndiyo waliongoza maendelezi makubwa ya Las Vegas na kuufanya uwe mji ulivyo sasa. Kilichowavuta ni sheria ya kuruhusu kamari na sio airport na vinginevyo. Sasa mbona unajikanganya? Federal Government inasaidia tu pale ambapo miji imeishaanzisha miradi. Federal government haianzishi miradi ya biashara kama Mass transit ndiyo maana haina shirika la ndege, haina viwanda vya silaha, haina makampuni ya treni. Haya yote ni makampuni ya kibiashara ambamo Federal government inanunua huduma. Najua unaona sisi tulio bongo ni wakuja lakini si kwa kila kitu. Serikali ya Tanzania ilikuwa inawekeza kwa misingi ya kuleta maendeleo ( Diamond cutting Iringa wakati almasi iko Mwadui, Steel Mill Tanga, Musoma Textile, Tabora Spinning, n.k) na mara nyingi havikufanikiwa. Cha msingi ni kuweka vivutio kama infrastructure nzuri, sheria pendelevu, elimu bora na wawekezaji watakuja. Hawa tunaowaita wawekezaji wengi wao ni matapeli ambao interest yao ni kuvuna chap chap na kuondoka with minimal investment. Na sisi kwa bahati mbaya tumebaki kuwa rahisi mno kuwaamini.
Biashara kuu ya Las Vegas ni kamari. Pamoja na kuwako bwawa la Hoover na hiyo barabara unayoizungumzia ni sheria ya kuruhusu kamari ndiyo iliyowavuta wakina Bugsy na wenzake. Las Vegas ukatangazwa kuwa ni mji usio na Familia na ndipo biashara ya kamari ikapanuka. accessibilty na sheria vyote vilichangia kuvuta mabepari. Nilivyokuelewa mwanzoni (niwie radhi kama nimekukosea)ni kuwa serikali ipeleke wawekezaji kule ambako hakuna maendeleo. Kama hiyo ya Dumila. Serikali walijenga barabara na wawekezaji wakaanzisha soko la mahindi na kadhalika, mji ukajikita. Hapa Kimara kuna infrastucture tayari (kwa hali ya kiTanzania) na inaelekea tayari ameshapatikana muwekezaji atakayejenga hiyo satellite city. serikali haiwezi kumwambia kuwa ati badala ya kujenga hapo aende mathalani Kwimba, Kibondo au hata hapo Dumila. Njia pekee ya kumpeleka huko ni kumwekea mazingira mazuri ambamo ataweza kufanya biashara. Mimi tatizo langu ni aina ya uendelezaji atakaofanya huyu bwana/bibi hapo Kimara. Tuna kawaida ya kumwogopa yule tunayemwita mwekezaji kiasi cha kumpa blank cheque afanye chochote atakacho. Maendelezi kama haya yanatakiwa yajadiliwa kwa uwazi na jamii nzima kabla ya utekelezaji kuanza.
Nitakupa mfano wa New York. Sehemu kubwa iliyobaki inayoweza kuendelezwa Manhattan ni eneo la railyards lijulikanalo kama Hudson Yards. Mipango ya awali ilikuwa ni kujenga stadium kwa ajili ya timu ya the Jets ambayo ingegharimu zaidi ya $1.2 billion. Wakaazi waliipinga kutokana na sababu za kimazingira( ongezeko la magari wakati wa mechi, kelele, historia ya pale mahali n.k). Mpango huu umekufa. Sasa mpango ni kujenga business centre nyingine ( kama hii sisi tunayoiita satellite City) juu ya hizo railyards. Watu wa mipango miji wa jiji la New York wameishatayarisha ramani zao za awali ya nini wanachotarajia pale KABLA ya kupapiga mnada kwa waendelezaji. Wao wanataka maofisi,sehemu za burudani, sehemu za wazi, sehemu za tamaduni na makazi. Wananchi wanaoishi jirani wanataka wahakikishiwe kuwa patukuwa na makazi kwa ajili ya wale wasio na uwezo. Sasa kwa vile patakuwa na public review za mradi mzima ni lazima muwekezaji ahakikishe kuwa patakuwa na haya makazi ama sivyo mradi utakufa. Makisio ni kuwa mradi utachukua si chini ya miaka 10 kutekeleza. Sasa sisi ( nasikitika kuwa na wengi humu JF mmo) tunagombea hicho tunachoita fidia bila kuuliza ni kitu gani kinachokusudiwa kujengwa. Je wakija jenga sehemu ambayo wakina yakhe hawana nafasi(Tumeona haya kwenye mahoteli ya ufukweni ambapo wavuvi wenyeji hawaruhusiwi kuendelea na shughuli zao ati kwa sababu watawabughudhi watalii)tutamlaumu nani? Si tumeshachukua vipande vyetu vya fedha? Kabla ya hata kuzungumzia hiyo fidia ilibidi mamlaka husika ituelezee hiyo satellite city hasa inahusu nini? Kutakuwa na nini pale? na sisi kama jamii tutafaidika vipi? Maelezo haya yasiwe kwa maneno tuu bali maandishi na michoro. Baada ya hapo ndiyo tugombee hayo makombo.