😂😂😂😂Habarini wanazengo
Unajua mwanzoni ilianza kama mzaa hivi watu walikuwa wanataniana wakicheka na hakuna aliyekuwa anamaindi lakini upepo umebidalika kwa kiasi kikubwa na kama hatua madhubuti hazitachukuliwa basi kuna jambo baya linaenda kutokea.
Vita hii inapigwa kila kona, uwanja mkuu wa mapambano ni huko mtandaoni hasa katika mtandao wa Facebook, hata humu Jf kunakuwaga na milio kadhaa ya risasi baadhi ya siku.
Stori ipo hivi:
Jana nilienda Hotel fulani kupata moja baridi nikiwa nivuta mafumba ya kinywaji changu pembeni yangu kulikuwa na maongezi ya watu wawili ambao kwa mikao yao walikuwa ni wapenzi sikusikiliza mazungumzo yao ijapokuwa nilikuwa nasikia kila kitu mara nilisikia yule mlimbwende akimwambia mshikaji, ndio maana u mwanaume wa Dar.
Kauli hiyo ilimfanya mshikaji ampige kofi mrembo wawatu jambo lililonifanya na mimi nigeuke alimpiga cha banzi la pili hali iliyomfanya demu uvumilivu umshinde wakashikana niliamka kusuluhisha ule ugomvi.
Sasa nikajiuliza kwani kuitwa mwanaume wa Dar ni tatizo maana kwa sasa vita niionayo huko mtandaoni si lelemama watu wanatukanana matusi ya laana kabisa picha za utupu zinazotupwa huko zikiwaonyesha wanaume waliouchi na viguo vya kike zimetanda kila pahala.
Naiomba serikali iamulie ugomvi huu kwa maana tunapoelekea si kuzuri kabisa.
Vita tuliyonayo si ile ya ukabila au udini kama tulivyozoea bali vita ya Wanaume wa Dar na wale wa Mikoani.
Nawasilisha
Wanaume wa Dar hilo ni jina tu la wanaume walegevu na waoga kwenye maisha ila jina hilo halimaanishi wanaume wote wanao ishi Dar ndio wana tabia hizi,
Mwanaume yeyote hata uliopo Kigoma, Iringa, Arusha, Dodoma ukiwa na tabia za ulegevu na uoga kwenye maisha automatically utaitwa mwanaume wa Dar,
Wanaume wa Dar tunakaza roho, watu wametuamulia sababu tukienda mikoa yao tunajidai, tunabeba mabeibe wao yani manzi akisikia wewe kwenu ni Daslama "kama wanavyoipaitaga wa mikoani" wanazimika hatari...
Mi navyoelewa kuhusu kuitwa mwanaume wa Dar si kwasababu tuu unakaa Dar bali mwanaume wa Dar ina maana ya mwanaume yoyote kokote nchini aliye na vijitabia na swaga za kike, Yaani Mambo yake ni Umama tupu, mfano Umbea, madeko, lifestyle na vyakula,mnaenda kula na demu wako wote mnaagiza chipsi, Dume zima kwny simu yake unakuta limejaza taarabu tupu,Dume zima linakutumia SMS' xafi' badala ya Safi huu ndo Umama wenyewe Tabia hizi ni nyingi sana kwa Wanaume walio Dar
Hahahah mkuu tunapigwa vita sana lakini mioyoni mwao wanaume wa mikoani wanatamani wangekua sisiHhahahaah! Ukitongoza demu wa mikoani tayari anadhani ka-win life coz anajua Bongo hii hapa
UNATAMAN KUWA KAMA DADA ??Hahahah mkuu tunapigwa vita sana lakini mioyoni mwao wanaume wa mikoani wanatamani wangekua sisi
Nimezungumzia wanaume wa mikoani wapi nimeashiria kutamani kua dada? Au ndo akili za wanaume wa mikoani hizo?UNATAMAN KUWA KAMA DADA ??
pengine swali nimeliwasilisha vibaya. samahan kwa hlo . umesema wanaume wa mkoani tunatamani tuwe Kama wanaume wa dar na Mimi nakuuliza swali je we ungetamani uwe na tabia Kama za kidada ? ni swali tu dogo .ni hayo tu mkuuNimezungumzia wanaume wa mikoani wapi nimeashiria kutamani kua dada? Au ndo akili za wanaume wa mikoani hizo?