Hii vita itaisha lini?

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,305
10,580
Habarini wanazengo

Unajua mwanzoni ilianza kama mzaa hivi watu walikuwa wanataniana wakicheka na hakuna aliyekuwa anamaindi lakini upepo umebidalika kwa kiasi kikubwa na kama hatua madhubuti hazitachukuliwa basi kuna jambo baya linaenda kutokea.

Vita hii inapigwa kila kona, uwanja mkuu wa mapambano ni huko mtandaoni hasa katika mtandao wa Facebook, hata humu Jf kunakuwaga na milio kadhaa ya risasi baadhi ya siku.

Stori ipo hivi:
Jana nilienda Hotel fulani kupata moja baridi nikiwa nivuta mafumba ya kinywaji changu pembeni yangu kulikuwa na maongezi ya watu wawili ambao kwa mikao yao walikuwa ni wapenzi sikusikiliza mazungumzo yao ijapokuwa nilikuwa nasikia kila kitu mara nilisikia yule mlimbwende akimwambia mshikaji, ndio maana u mwanaume wa Dar.

Kauli hiyo ilimfanya mshikaji ampige kofi mrembo wawatu jambo lililonifanya na mimi nigeuke alimpiga cha banzi la pili hali iliyomfanya demu uvumilivu umshinde wakashikana niliamka kusuluhisha ule ugomvi.

Sasa nikajiuliza kwani kuitwa mwanaume wa Dar ni tatizo maana kwa sasa vita niionayo huko mtandaoni si lelemama watu wanatukanana matusi ya laana kabisa picha za utupu zinazotupwa huko zikiwaonyesha wanaume waliouchi na viguo vya kike zimetanda kila pahala.

Naiomba serikali iamulie ugomvi huu kwa maana tunapoelekea si kuzuri kabisa.
Vita tuliyonayo si ile ya ukabila au udini kama tulivyozoea bali vita ya Wanaume wa Dar na wale wa Mikoani.

Nawasilisha
 
Ha ha haaaa! Yani kuitwa mwanaume wa Dar ni bora mtu akupige ngumi tu. Ni aibu na fedheha mkuu. Ndo maana umeomba akutake radhi
 
Back
Top Bottom