Hii trick ya CCM inafanikiwa

Najaribu kuwaza, inawezekana kweli wakaua VYAMA VYA UPINZANI, ila wanaweza kuua DHAMIRA ya kipinzani kwenye mioyo ya wenye nchi yao?

Nchi ikishakua ya chama kimoja na kwa bahati mbaya sana haitokua ikiongozwa na mawazo ya wanachama, ni watu wawili tu ndiyo watakaokua wanapanga mambo yaendaje je, wanatosha kuvaa viatu vya watanzania wote zaidi ya 50mil?

Pia hili fukuto litakalo baki na hawa watanzania wenye nchi yao wataweza kulihilimili miaka yote? Wakishindwa nini kitatokea?

Tuombe uzima, Na tuombe hawa wawili wasizime mitandao hasa JF tuje kuona mwisho wake yote haya ni nini.
Watanzania wanazingua acha kibaki Ccm tukifanywa mazombi ndipo tutatia akili hata hao wanaolipwa na maccm wajukuu zao watasulubika kkama sisi
 
Tuache mawazo finyu.Mtu anahaki ya kwenda chama chochote. Mtu akihamia ccm kanunuliwa lakin akihama ccm kajitambua,bas na wao wanunue kama wananunulika
 
Najaribu kuwaza, inawezekana kweli wakaua VYAMA VYA UPINZANI, ila wanaweza kuua DHAMIRA ya kipinzani kwenye mioyo ya wenye nchi yao?

Nchi ikishakua ya chama kimoja na kwa bahati mbaya sana haitokua ikiongozwa na mawazo ya wanachama, ni watu wawili tu ndiyo watakaokua wanapanga mambo yaendaje je, wanatosha kuvaa viatu vya watanzania wote zaidi ya 50mil?

Pia hili fukuto litakalo baki na hawa watanzania wenye nchi yao wataweza kulihilimili miaka yote? Wakishindwa nini kitatokea?

Tuombe uzima, Na tuombe hawa wawili wasizime mitandao hasa JF tuje kuona mwisho wake yote haya ni nini.
Mkuu hicho ulichokiomba mwishoni nadhani ndio gia ya mwisho. Tuombe mungu kwa kweli
 
Wabunge wanaojiudhuru jumbo libaki wazi mpk uchaguzi unaofuata
 
Hivi huyu mtolea kweli mtaani akipita kwann masela wasimpige mitama dawa ya wasaliti ni kipigo tu...nawaaminia CUF.Ila na yy kafanya maamuz mazito kakaa kawaza 2020 hatoboi so bora ale chake mapemaaa afanye mambo mengine kwli siasa inahitaji ukomavu sana
 
Hate or love them, hawa ccm hawana aibu sote twajua,wananunua kwa pesa,wanatumia nguvu na vitisho kufanikisha wanalotaka
Ila kwa hili la watu kurudi kwao especially kwenye issue ya mbunge wa Cuf bwana Mtulia naweza kusema sasa CCM wamejua pa kupigilia msumari au kumwagia chumvi kwenye kidonda
Si nyote mnakumbuka kinondoni mwaka 2015 ni mojawapo ya majimbo ambayo wizi wa kura ulishindikana? vijana walihamasika wakalinda kuara hadi FFU wakapiga mabomu ya kutosha ya machozi?
I was there wakati mtulia anatangazwa ilikuwa ni shangwe kuu hadi kuna FFU mmoja akawa anaongea na simu na mtu huku naye akifurahi kwa kusema ccm kapigwa hukuu
Sasa kama ccm inaanza kununua wabunge waliopitishwa in expense ya damu na viungo vya watu ,tactics yao inafanikiwa,they are winning
2020 HAKUNA TENA KIJANA ATAKAYEHANGAIKA KUPOTEZA VIUNGO AU KUPATA MAJERAHA KWA SABABU YA WABUNGE WA AINA YA MTULIA
MAGUFULI ANAKUWAGA NA MSEMO WAKE WA KUSEMA MSIWAAMINI WANASIASA,NI KWELI KAAMUA KUWAONYESHA WANANCHI WASIWAAMINI WANASIASA,HADI 2020 MSISIMKO WA KISIASA UTAKWISHA KABISA.
Waelewa huangalia hoja na agenda za chama. Waelewa huhitaji zaidi mabadiliko chanya. Chama cha siasa lazima kiwe na agenda zinazokilisha na kukikuza. Lengo la mwanasiasa yeyote ni kukuwa ili aendelee kuchaguliwa tena na tena. Ukiwa ktk chama ambacho hakina agenda zinazolisha na kukuza chama maana yake na wewe unadumaa na hata kufa kabisa. Cancer kwa chama chochote ni ubinafsi, kukosa misimamo madhubuti katika agenda zake, kuwa pinzani kwa hoja zinazoungwa mkono na wengi, kulalamika tu badala ya kuwa imara ktk kujenga hoja na kutatua matatizo yao na ya wananchi nk Hata hivyo, upinzani sahihi na madhubuti ni MUHIMU SANA ktk maendeleo ya Taifa lolote
Tuache mawazo finyu.Mtu anahaki ya kwenda chama chochote. Mtu akihamia ccm kanunuliwa lakin akihama ccm kajitambua,bas na wao wanunue kama wananunulika
 
Binadamu anayekubali kununuliwa na pesa kama mtumwa hawezi kuaminika popote duniani hadi mbinguni. Na hakika ccm haiwezi kutoboa kinondoni labda kwa kuwaondoa mawakala wa upinzani kama walivyofanya awamu iliyopita.
 
Hivi tunaelekea wapi! Inawezekana vipi mbunge/diwani kujiuzulu nafasi yake kirahisi tu kisa anaunga mkono yanayofanywa na chama tawala! Hivi wanaelewa nafasi walizokua nazo na majukum yao! Najaribu kuwaza tu nafasi ya mbunge/diwani na majukum yake kama ni wakusimama upande wa chama
 
Back
Top Bottom