Hii trick ya CCM inafanikiwa

ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,890
2,000
Hate or love them, hawa ccm hawana aibu sote twajua,wananunua kwa pesa,wanatumia nguvu na vitisho kufanikisha wanalotaka
Ila kwa hili la watu kurudi kwao especially kwenye issue ya mbunge wa Cuf bwana Mtulia naweza kusema sasa CCM wamejua pa kupigilia msumari au kumwagia chumvi kwenye kidonda
Si nyote mnakumbuka kinondoni mwaka 2015 ni mojawapo ya majimbo ambayo wizi wa kura ulishindikana? vijana walihamasika wakalinda kuara hadi FFU wakapiga mabomu ya kutosha ya machozi?
I was there wakati mtulia anatangazwa ilikuwa ni shangwe kuu hadi kuna FFU mmoja akawa anaongea na simu na mtu huku naye akifurahi kwa kusema ccm kapigwa hukuu
Sasa kama ccm inaanza kununua wabunge waliopitishwa in expense ya damu na viungo vya watu ,tactics yao inafanikiwa,they are winning
2020 HAKUNA TENA KIJANA ATAKAYEHANGAIKA KUPOTEZA VIUNGO AU KUPATA MAJERAHA KWA SABABU YA WABUNGE WA AINA YA MTULIA
MAGUFULI ANAKUWAGA NA MSEMO WAKE WA KUSEMA MSIWAAMINI WANASIASA,NI KWELI KAAMUA KUWAONYESHA WANANCHI WASIWAAMINI WANASIASA,HADI 2020 MSISIMKO WA KISIASA UTAKWISHA KABISA.
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
8,908
2,000
Najaribu kuwaza, inawezekana kweli wakaua VYAMA VYA UPINZANI, ila wanaweza kuua DHAMIRA ya kipinzani kwenye mioyo ya wenye nchi yao?

Nchi ikishakua ya chama kimoja na kwa bahati mbaya sana haitokua ikiongozwa na mawazo ya wanachama, ni watu wawili tu ndiyo watakaokua wanapanga mambo yaendaje je, wanatosha kuvaa viatu vya watanzania wote zaidi ya 50mil?

Pia hili fukuto litakalo baki na hawa watanzania wenye nchi yao wataweza kulihilimili miaka yote? Wakishindwa nini kitatokea?

Tuombe uzima, Na tuombe hawa wawili wasizime mitandao hasa JF tuje kuona mwisho wake yote haya ni nini.
 

Jumaaofficial

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
255
250
Na mm nataka ubunge nione-kama wataninunua

Bei ya kwanza nitawaaambia $5 bilion.


Then nitawapa mrejesho naombeni Sapport Yenu wana Jf

Nipeni kura zenu
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,090
2,000
Binafsi nimekuelewa...wasiwasi wangu naanza kuona Giza mbeleni...take it from me..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom