Najaribu kuwaza, inawezekana kweli wakaua VYAMA VYA UPINZANI, ila wanaweza kuua DHAMIRA ya kipinzani kwenye mioyo ya wenye nchi yao?
Nchi ikishakua ya chama kimoja na kwa bahati mbaya sana haitokua ikiongozwa na mawazo ya wanachama, ni watu wawili tu ndiyo watakaokua wanapanga mambo yaendaje je, wanatosha kuvaa viatu vya watanzania wote zaidi ya 50mil?
Pia hili fukuto litakalo baki na hawa watanzania wenye nchi yao wataweza kulihilimili miaka yote? Wakishindwa nini kitatokea?
Tuombe uzima, Na tuombe hawa wawili wasizime mitandao hasa JF tuje kuona mwisho wake yote haya ni nini.