Hii tabia ya wavulana ikome

Hii tabia ya wavulana ikome

Hii inaonyesha jinsi wavulana wasivyotumia akili. Na ukiwa "ke" usipende kudate na vi vulana cause nowdays technology imekuja juu waweza hata tegesha simu pahali bila wewe kujua.
Nawashauri watu wawe makini sana maana waweza kujibastola bila kujua kisa starehe ya muda mfupi. Ndo maana wale wenye ufahamu wanapenda kutumia maneno haya " kabla hujatenda jambo, fikiria athari zake na faida zake cause starehe ya muda mfupi yaweza ku cost maisha yako yote"
 
Nyingi zimevujishwa na hao hao wadada. Eti rekodi kwa kumbukumbu
 
Aisee..
Na nyie wasichana hamnazo pia.. Inakuwaje unakuwa mwepesi kurekodiwa? Au huwa mnaleweshwa kwanza?
 
Mapenzi ni starehe bwana,mapenzi kupeana raha.

Siku hizi imezuka tabia ya mijitu hasa wavulana ( ndio nawaita wavulana kwani akili zao ni za kitoto hata kama ni wanaume),unakuta jitu linaacha kufanya kile kinachotakiwa kufanywa (mapenzi/sex) jitu linakazana kurekodi tendo lile kwenye visimu vyao,mbaya zaidi yeye hajichukui sura ila binti wa watu ndio full kuonekana.

Najiuliza hivi wewe una akili gani mpaka kuacha kufanya yanayofaa kufanywa na kuanza kumrekodi mwenzako ili tu kesho ukamdhalilishe kwa wenzako?hivi unawezaje kwanza kuchukua hiyo video au picha katikati ya tendo ilihali nijuavyo mimi katika tendo lile mtu hutamani hata macho yaangalie kwengine?au ndio unakuwa umeenda pale tu ili ukamdhalilishe mwenzio?

Juzi nilikuwa kijiwe kimoja nikakuta watu wanaonyeshana video za ngono,anayewaonyesha wenzake ndiye aliyepiga hiyo video.yule binti yule wa pale naniii..(sitaji eneo) ndio huyu bwana,jana nimemgonga na video angalieni hii hapa na wenzake wanamshangilia eti we jamaa mkali balaa.

Tabia hii siipendi na inadhalilisha sana dada zetu(sisi wengine tuna dada wengi tu).Hebu fikiria siku moja ndio unakutana na video ya dada yako ndio amefanyiwa hivyo utajisikiaje?au ghafla unakutana na video ya mama yako mzazi alikuwa na michepuko huko wakamchukua video utajisikiaje?
Vile ambavyo utajisikia ndio vile ambavyo mwenzio uliyemfanyia hivyo pamoja na ndugu zake wanavyojisikia.

Achezi tabia hii kwani ni ya kishenzi na ya kidhalilishaji kabisa.kama unaona huwezi kufanya mapenzi bila kurekodi basi acha.

Nyinyi DADA zetu mkiona mpo faragha na jitu linatka likupige picha au video usikubali,vaa nguo zako tembea tena iwe ndio mwisho wa mahusiano yenu,maana huyo hana nia nzuri,anakupiga picha au video ili kesho akakudhalilishe,na mnadhalilika kweli nyie hamjui tu.Video zenu za utupu watu wnaonyeshana vijiweni au hata whatsapp.Wewe ukipita mitaani unaona kama upo sawa tu kumbe watu wankuchora tuu ndio si wameisha kujua kila kitu kuanzia ndani mpaka nje.

Kwa waungwana hii tabia hatuifanyi hata kidogo,naomba na wewe unayependa tabia hii tafadhali badilika maana vinginevyo utakuwa kwenye kundi la washenzi na wapumbavu tu.

Mlishaambiwa ikimbieni zinaa, uasherati usitajwe kwenu ila hamsikii!! mnadhani mngekuwa tayari mmeolewa mngefanyiwa huo mnaouita ushenzi?
Kama makatazo ya mungu tu yamewashinda hayo ya kupigwa picha mtayaepuka vipi?
UKILIMA VIAZI USITARAJIE KUVUNA MIHOGO.
 
Wajinga ni wale wanaokubali kupigwa picha au video,cdhani kama mwanamke akikataa atalazimishwa.Ni kweli sio jambo zuri maana linakuwa na madhara sana after break up,lakini husilaumu mpigaji picha wakat hata mpigwaji alikuwa anaweka mapozi kwa madaha.
 
Back
Top Bottom