Hii tabia vipi wakuu wangu.....

Hii tabia vipi wakuu wangu.....

Jana katika pita pita yangu mjini nikabahatika kukutana na binti mmoja, tukabadilishana namba za simu, time za jioni nikaamua kumrukia hewani tukutane town tufahamiane zaidi, akaibuka na rafiki zake wawili, ikawa timu ya watu watatu, tumekaa kunywa mabinti wale wakaanza kuagiza vinywaji vya bei kubwa kubwa, mwenyewe nikaagiza maji tu, wanywaji mnajua kuna kakinywaji nikawa nasikia nipimie nzima, hapo Tsh 12,000 cash, mwingine nipatie henken. Kana kwamba hiyo haitoshi ulipofika wakati wa msosi, mwanamke anaagiza mnavu kuku mzima peke yake, huku kichwa kinaniuma nawaza kumbe wanawake wa mujini ndo wana matumbo makubwa hivi, kumbe ndiyo maana wanawake wengi sasa hivi wana vitambi. Pigo la mwisho ni wakati wa kuondoka, wanaagiza vinywaji na chakula cha take away, kidogo niumbuke ila uzuri bar ile wanapokea hela kwa tigo pesa, nimeondoka pale sina hamu, nimeinamisha kichwa na wala sina hamu tena na mwanamke yule. Hii tabia unapopewa offer ndo unaagiza kinywaji cha bei mbaya, mtu kila siku anakunywa fanta, siku hiyo anataka redbull, vipi wakuu wangu?

we hapo ndo umeonekana mshamba,huyo sio mama,dada,shangazi wala mke.kwanini usimwambie bajeti yako hairuhusu?ndo maana wabongo wengi tunajitahidi kutafuta hela kwa tabu sana na nguvu zote lakini tunafilisika ndani ya siku moja tu.
 
Jana katika pita pita yangu mjini nikabahatika kukutana na binti mmoja, tukabadilishana namba za simu, time za jioni nikaamua kumrukia hewani tukutane town tufahamiane zaidi, akaibuka na rafiki zake wawili, ikawa timu ya watu watatu, tumekaa kunywa mabinti wale wakaanza kuagiza vinywaji vya bei kubwa kubwa, mwenyewe nikaagiza maji tu, wanywaji mnajua kuna kakinywaji nikawa nasikia nipimie nzima, hapo Tsh 12,000 cash, mwingine nipatie henken. Kana kwamba hiyo haitoshi ulipofika wakati wa msosi, mwanamke anaagiza mnavu kuku mzima peke yake, huku kichwa kinaniuma nawaza kumbe wanawake wa mujini ndo wana matumbo makubwa hivi, kumbe ndiyo maana wanawake wengi sasa hivi wana vitambi. Pigo la mwisho ni wakati wa kuondoka, wanaagiza vinywaji na chakula cha take away, kidogo niumbuke ila uzuri bar ile wanapokea hela kwa tigo pesa, nimeondoka pale sina hamu, nimeinamisha kichwa na wala sina hamu tena na mwanamke yule. Hii tabia unapopewa offer ndo unaagiza kinywaji cha bei mbaya, mtu kila siku anakunywa fanta, siku hiyo anataka redbull, vipi wakuu wangu?

hamna kitu hapo,pasua kichwa huyo na ukiendelea nae anakufilisi,wanawake weng wa aina hyo wanajua matumizi tu,pesa inatafutajwe hawajui!
 
pole best hao walikuja kusafisha nyota...wamekaa miaka 5 bila kutolewa out unafikili wangekuwaje...au na wewe uliaza na swaga za mtoto wa mbunge wakati unaomba namba ili mtoto asikuchomolee..siku izi ujanja kuwai sio kuwahiwa .pole wamekuwai ..

asante, kwa kweli nimewavulia kofia.
 
Kwani hiyo bar uliyoenda kuspend hakuna choo cha nyuma?....c ungepitia mlango wa nyuma usepe uwaachie msala wao wenyewe eboo!
 
kablA ya miadi inabidi umpe taarifa kuwa hutaki msongamano. kama hataki basi aandae pochi lake. nyambaf zAo
 
naogopa kuendelea nisije umia zaidi.

...hahahaaa,,, kama ngapi vile walikukula......komaaa kamanda.......samaki wanaotafuna chambo lazima uwazamie ukawanase na mikono hata kama ni kimo kirefu mno....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom