Hii tabia Musoma inakera sana

Habari wana JF,

Moja kwa moja niende kwenye mada.

Kumekua na tabia yaajabu sana na ya kusikitisha sana hasa kwenye kumbi mbalimbali za starehe yaani ukiingia kwenye kumbi nyingi za starehe hapa mjini Musoma Kuna kuwa na vijana wengi sana wa kike na wakiume.

Lakini jambo linalo nisikitisha nikua vijana hawa hasa wakiume wamekua omba omba wakiwa kwenye kumbi hizo za starehe tena kazi yao ni kuzunguka na cup wakikufikia kwako wanasogea karibu na kukuambia uwawekee kinywaji kidogo haijalishi ni kinywaji gani unatumia yeye ili mladi aonekane anakunywa na kinachoniudhi zaidi ni pale anapokuja mmoja akikuomba ukimuwekea kidogo tu anaenda kuwaambia wenzake nao wanakuja kukuomba na ukisha mpa mmoja basi jua kuanzia siku hiyo wewe ni rafiki yake wa karibu sana kila unapokuwa unaenda akikuona tu anakufuata na kukubembeleza umnunulie kinywaji au umuwekee kidogo kwakwel hii tabia imekuwa ikinikwaza sana wanapokuona umeingia wanakuja na kuanza kukusumbua.
😆😆 Hii ni hatari sana kwa afya
 
Ndio hapo hapo amepaongelea mleta mada, kuna mmoja alikuja na glasi kuniomba nimpunguzie K Vant ambayo mi nilikuwa napiga tarumbeta, ikabidi nimnunulie.......basi alihangaika ukumbi mzima kunitafutia mtoto mkali wa kwenda kumgegeda
Ndo kawaida yao hao madogo
Ndio hapo hapo amepaongelea mleta mada, kuna mmoja alikuja na glasi kuniomba nimpunguzie K Vant ambayo mi nilikuwa napiga tarumbeta, ikabidi nimnunulie.......basi alihangaika ukumbi mzima kunitafutia mtoto mkali wa kwenda kumgegeda
Ndo kawaida yao hawa jamaa
 
Yaani Kuombwa nao Kinywaji tu ndiyo unakimbilia JF Kuwananga hivi je, wangekuomba vingine ingekuwaje? Wewe ni Mtoto wa Kiume kweli au?

Wewe hakuna wa kiume wa wa kike hapo. Kwenye swala la kuombana vinywaji sehemu za starehe ni ujinga sana tena hao wamezidisha "eti kumiminiana..eeeh". Hata mm sikubaliani na hao omba omba. Kuliko kukaa na kuomba omba si wakatafute hela huko
 
Back
Top Bottom