Hii tabia inanikera sana

Haya mambo magumu, mimi ninaenda kanisani na vitabu wanaoenda na wakati watajijua na Mungu wao.
Kwa kweli hii technologia ya sasa imekuwa ikileta mkanganyiko kweli anyway tuwaache na simu zao
 
Kwa sisi wa Rc hawaruhusu hayo mambo..tena siku hizi umakutana na bango "simu haziruhusiwi ibadani"
 
Kwa sisi wa Rc hawaruhusu hayo mambo..tena siku hizi umakutana na bango "simu haziruhusiwi ibadani"
Kwanza utaanzia wapi kuingia na simu mana kila mtu macho kodoo
 
Why usitumie hard copy?
 
Biashara bila matangazo konki hailipi. Hayo the so called makanisani ya kiroho ni taasisi binafsi za kujipatia ulaji. Japo hata makanisa mama kama RC na Lutheran siku hizi yamekuwa vituo vya kukusanya mapato na kutoa vitisho kwa wasiofuata taratibu za kanisa.
 
Tunatumia simu kusoma biblia,tenzi za rohoni nk.
Acha kuishi dunia ya kale.
Acha uongo wewe. Nimeshuhudia mtu anatoa simu ili apigwe picha kuonesha kwamba na yeye alikuwepo kanisani.
 
Mi hi huwa natumia Sana kwenye jumuiya...inanifanya nafatilia kwa umakini Sana.
 
Barikiwa
 
Ninaposali mimi biblia ya mchungaji ipo kwenye iPad.
 
Hapo sasa na mm hiwa na kereka balaa watu an hawaheshmu ibada
 
Hahahaaa, "makanisa ya kisasa"! Siyo kwamba nadharau madhehebu ya wengine la! Halafu si ndiyo hayo yanajiita pia "makanisa ya kiroho"? Wacha tu nibaki huku huku niliko bwan, nimeridhika.
 
Muda wenyewe tunaokaa kanisani hauzidi masaa saa nne kwanini usizime, mwengine anakwambia anatumia kwa ajili ya kusoma biblia wakati kusoma hard-copy ni vizuri zaidi, naona soft copy imewekwa uitumie kama uko safarini au lunch time kama uko kazini. Tabia nyengine inayonikera ni kunywa soda na maji mtu akiwa kanisani, wengine wanakula mpaka chakula, kutafuna bigi jii, kusoma magazeti wakati ibada inaendelea. Mungu atuhurumie....
 
Kwanini wakataze mkuu,au zile sio Biblia au sio Tenzi?najua una hoja hebu iweke wazi tukuelewe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…