Hii story imemtokea mwenzetu humu

Phb_himself

Senior Member
Jul 5, 2017
130
225
Jamaa anasoma na demu wake chuo huko Kigamboni jana ndio ilikuwa aondoke aende likizo maana wamemaliza mtihani wakaagana na demu jamaa akasepa mida ya saa kumi jioni. Demu ni mtu wa Chuga imefika mida ya saa moja jamaa akarudi akasema kakosa usafiri wa kumfikisha feri akamcheki demu wake ili ampe taarifa, kupiga simu hapatikani mpaka mida ya saa nne akaenda kulala akijua labda demu kalala.

Imefika asubuhi mida ya saa moja anapigiwa simu na demu wake kupokea kinaongea kidume jamaa akaweka loudspeaker kidume kinadai ni demu wake na muda huo wapo lodge jamaa haamini akazima palepale daaaah! Wahuni hatuamini kwanza demu huwezi mdhania ila jamaa mpaka sasa hivi bado haamini na ukicheki ni couple ya mfano na jamaa ni moja ya watu peace sana hana makuu ila katendwa na mtu ambaye dah!
 

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,575
2,000
Ushauri wangu kwake ni kuwa atafute pesa na mengine yatamfuata bila shida.Mpenzi wangu niliyesoma naye A-Level ,baada ya kuhitimu tulikuwa tynawasiliana vizuri tu,baadae yeye matokeo yake haya kumruhusu kwenda chuo kikuu ikabidi akasome diploma ya ualimu miaka miwili

Muda wote huo tulikuwa tunawasiliana vizuri tu,alipoajiliwa wakati mimi nikiwa bado nasoma akajua tayari mimi nimzigo kwake,hivyo akaanza kujitenga na Mimi,nami sikuwa na hiana nikasema let her go.Hivyo nikawekeza muda na nguvu zangu katika kusoma na kutafuta pesa
 

official scandal

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
344
1,000
Hakuna jipya linalohitaji ushauri hapo:-
Nikiwa chuoni (chuo kikongwe zaidi hapa nchini) nilishuhudia mengi kwenye mahusiano ya wanachuo.
Kijana kama unajua, mapenzi ya chuo ni ya kupoteza muda usiweke akili yako yote hapo.
Kuna mambo ya msingi ya kuzingatia ukiwa chuoni kuliko mapenzi.
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,478
2,000
pole kwa yalokufika japo unajaribu kujificha nyuma ya kibodi, ushauri wangu ni kua umdhaniae sie kumbe ndie.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom