Hii sio photoshop

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,836
730,304
40f5324fc49f5786ddb267e15ede5f4d.jpg

Kwenye mambo ya mazingara ushirikina na ulozi kitu kama hiki si cha kawaida hata mara moja na hata katika maisha ya kawaida pia
Mganga anakutuma kuku unamleta kwa ajili ya shughuli anachinjwa ili kafara lifanyike , mara nyingi huachwa arukeruke mpaka roho imtoke

Imagine baada ya kuchinjwa haruki hatoi damu bali husimama tuli na miguu yake miwili bila kichwa , kama wewe ni mteja na wewe ni mwingine ni mganga mtafanyaje? Kimsingi mnaweza kutimua mbio

Kuna baadhi ya viumbe si kama vionekanavyo machoni unamuona ni kuku kumbe sio kuku unamuona ni paka kumbe sio paka unamuona ni

mshana jr kumbe sie

Dunia ina mengi ambayo bado hatuyajui

1460957621145.jpg
 
Mkuu hii habari nakumbuka hata BBC Swahili waliiandikaga kwenye page yao siku za nyuma.. Mpaka leo siielewagi
 
Nakumbuka tukiwa Primary kulikuwa na ile michezo ya mazingaumbwe mtu anachinjwa live kabisa na baadae anaunganishwa tena...Kumbe si kweli ni wanacheza na akili zetu na inawezekana hata hii nayo ukaona ni kuku amesimama kumbe ni anacheza na ufahamu wako tu..
 
1460959076690.jpg
sasa hii ni kwa mganga na tiba inatakiwa kuanza
 
Si kuna hata magari engine zake hazipo mbele zipo nyuma? Yumkini huyu kuku naye kichwa kilikuwa kinamsaidia kuokota tu chakula ila hakikuwa kinamsaidia sana kwenye mambo ya kuishi ndo maana kimeondolewa bado yuko fiti!
Kuna kuku maarufu sana aliitwa Mike yeye aliishi kwa miezi 18 bila kichwa
 
Nakumbuka tukiwa Primary kulikuwa na ile michezo ya mazingaumbwe mtu anachinjwa live kabisa na baadae anaunganishwa tena...Kumbe si kweli ni wanacheza na akili zetu na inawezekana hata hii nayo ukaona ni kuku amesimama kumbe ni anacheza na ufahamu wako tu..
Hapo kwenye kuchezewa akili zetu na kutufanya kuona mtu amechinjwa live kumbe sivyo ndipo nadhani wengi wetu tungependa kupata ufafanuzi kwamba inakuwaje. Mshana jr na wengine wenye uelewa wa haya mambo tusaidieni hapa.
 
Kuna mzee bana huku ye analoga kwa majipu!ukimfata anataka umpe jina la huyo mtu afu anakuuliza amrushie jipu la sh ngapi maana anaanzia jero.kuna jamaa aliomba mbaya wake atumiwe la elf5 we ni shida!
 
kweli bongo kuna maajabu nilishawai sikia kuna mti ulidondoka muda mrefu then baadae ukanyanyuka wenyewe sijui ni shinyanga hata sielewi. sijui hii sayansi yetu tunaitaje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom