Code za Uchawi na Miujiza; Fahamu haya machache

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
CODE ZA UCHAWI NA MIUJIZA, FAHAMU HAYA MACHACHE.

Na, Robert Heriel.

uchawi ni nguvu za Giza zinazotenda kinyume na akili ya mwanadamu.
Miujiza ni nguvu za Nuru zinazotenda kinyume na akili ya mwanadamu.

Ili Jambo liitwe uchawi au muujiza lazima liende kinyume na akili ya mwanadamu, liende kinyume na Sayansi ya kimwili, mambo yaonekanayo.

Ili Jambo liitwe uchawi au muujiza sharti livunje kanuni za asili.

Jambo lolote lisiloweza kuvunja kanuni za asili kamwe hakiwezi kuitwa uchawi au muujiza isipokuwa ni Akili, maarifa na ujuzi wa Hali ya juu.

Watu wengi hasa kutoka jamii zenye elimu duni na maarifa hafifu hushindwa kutofautisha mambo ya akili, maarifa, ujanja, ujuzi na mambo ya miujiza na uchawi.

Kwenye jamii mtu anaweza akafanya Jambo la akili kubwa, ujanja au maarifa akaitwa mchawi au mwanamiujiza.
Hii ni kutokana na kasumba ya watu miongoni mwetu.

Kikawaida, palipo na akili, maarifa, ujuzi mwingi basi matumizi ya uchawi na Miujiza huwa chini.

Akili, maarifa, ujuzi, ambazo baadaye huzalisha Teknolojia yameathiri Kwa kiasi kikubwa nafasi ya miujiza na uchawi.
Hata hivyo bado nafasi ya uchawi na Miujiza katika jamii nyingi za Afrika, Asia na Nchi nyingi zinazoendelea ni kubwa ukilinganisha na Nchi za ulimwengu wa Kwanza.

Nikirejea kwenye mada;

Uchawi na Miujiza ni Jambo lile lile katika pande mbili tofauti.
Uchawi ni nguvu itendayo Kwa matokeo hasi.
Wakati muujiza ni nguvu hutenda Kwa matokeo chanya.

Hata hivyo, uchawi huweza kuwa na manufaa Kwa muda Fulani, manufaa ya Muda mfupi, ambayo huwa Kama chambo kuwateka watu.

Uchawi ni nguvu ya kiroho ambayo asili yake imetoka Kwa Mungu mwenyewe, Muumbaji, nguvu hiyo iliwekwa katika Falme za Giza za kiroho, Kwa viumbe waishio GIZANi.

Uchawi Kama ulivyo muujiza, Una rank zake kulingana na nguvu husika.

Zipo Grade za chini kabisa mpaka Grade ya juu kabisa.

Uchawi na uchawi Kama ilivyo nature ya viumbe vionekanavyo,
Upo katika muundo wa Pyramid Hierarchy, pyramid Structure,

Katika kitako cha pyramid ambapo ndio papana/pakubwa ndipo walipo Wachawi/Waganga na watenda Miujiza wengi Sana.

Kadiri unavyopanda juu ya pyramid ya uchawi au muujiza basi idadi ya wenye nguvu inazidi kupungua mpaka kufikia kilele cha Piramidi basi mtawala hubakia mmoja kabisa ambaye ndiye mtawala au watawala.


1626154802902.png

(Mfano wa Piramidi(Pyramid)

Uchawi na miujiza ya level ya chini watu wengi huweza kuwa nao kwa ajili ya kutatua mambo madogo madogo yanayowakabili katika maisha yao.
Kama tulivyoona kwenye picha hapo juu, upande wa kitako cha piramidi ni pakubwa kieneo na pana-cover eneo kubwa kijiografia, pia pana watu wengi kulinganisha na sehemu ya juu kabisa ya piramidi.

Hata katika mambo ya kawaida, mfano pesa/utajiri, au elimu na ujuzi, pia vipo katika muundo wa piramidi, yakuwa wenye ujuzi na elimu kubwa wapo wachache sana ukilinganisha na wenye elimu ya kawaida au ya chini ambao wapo wengi kama mchanga. Halikadhalika na wenye pesa/matajiri ni wachache kuliko masikini/wenye vipato duni.

NAMNA UCHAWI NA MIUJIZA INAVYOFANYA KAZI

Watu wengi hasa wenye upeo mdogo hawaamini katika uchawi na miujiza, wenye upeo wa katika wanaamini uchawi na miujiza ipo lakini hawataki kuiendekeza, na wale wenye upeo wa juu kabisa, wanaamini uchawi na miujiza ipo na wanaiendekeza kwa kuitumikia.

Uchawi na miujiza zina code au patterns zake ili ziweze kufanya kazi.
Hata wanaoenda kujifunza Uchawi au masuala ya miujiza huenda kufundishwa Code, au patterns ili kuufanya uchawi au muujiza ufanye kazi.

Code au patterns za uchawi na miujiza zipo katika mfumo ufuatao
1. Mfumo wa namba
Kama vile hesabu ya mara tatu, mara saba, mara tisa, mara 13, mara 18, mara 28, mara 36 kuendelea.
Hesabu ya siku, mwezi au miaka kama 1,3, 5, 7, 9, 12, 40, 32, 36 kulingana na code za kudhuru au kunufaisha.
Mfumo wa namba husaidia uchawi au muujiza kufanyika kwa kusema, au kutenda kitu kwa kadiri ya mpangilio wa namba.

Kwa mfano; Mchawi au mganga, Jini, mzimu afanyapo uchawi lazima afungue code na pattern za namba ili uchawi au ulozi wake ufanikiwe. Mfano anaweza kutenda au kusema jambo fulani mata 3, 7 lakini isizidi 12 ikiwa atahitaji kudhuru, na isizidi mara 36 ikiwa atahitaji kuponya au kuleta manufaa.

Halikadhalika na muujiza, Nabii, kuhani, mtume, malaika itampasa afanye au amuagize mtu afungue code za namba ili muujiza uweze kutokea. Anaweza akaamrisha mara tatu, ikiwa ni jambo dogo lakini akamrisha mara saba isizidi 10 ikiwa ni jambo kubwa.

2. Malighafi
Malighafi kama vile madini, mimea, viungo vya viumbe, maji miongoni mwa mengine pia ni code au pattern za uchawi na miujiza. Uchawi na miujiza ya chini naya wakati ambayo ndio wengi huwa nayo sharti itumie malighafi zilizopo duniani kufungua na kufunga code zilizopo. Kuchanganya miti, madini na viungo vya baadhi ya viumbe ni lazima kwa level ya chini . Na hapa lazima mfumo wa namba pia uhusike, kwani malighafi hizo hazichanganywi kama mtu apendavyo bali kwa hesabu maalumu.

3. Ishara na amri kwa sauti ya chini au kimoyo moyo
Uchawi na muujiza mkubwa ni ile inayotumia ishara na amri kufungua code, yaani mhusika atatumia ishara iwe ya macho, mkono, mdomo au ulimi, kukunja uso, kuvuta au kutoa pumzi au kuchezesha sehemu yoyote ya mwili na kutoa amri kwa sauti ya chini au sauti ya juu.
Hapa uchawi au muujiza wa kati naya juu hutumia mfumo huu kufungua code. Mtu huweza kusema jambo fulani likatokea pasipo kutumia malighafi yoyote ile.
wenye kiwango hiki ni wachache, hata hivyo level hii sharti uwe unawanguvu za viumbe au miungu wenye nguvu sana.

Mambo yanayoathiri uchawi au muujiza kufanyika

1. Uwezo binafsi wa mchawi au mwanamiujiza
Watu wengi hupenda kwenda kwa waganga huku wakiwa na fikra kuwa waganga wote wanaweza kukutatulia matatizo yao bila kujali ukubwa wa tatizo. Hiyo dhana ni potofu.
Hata katika Wanamiujiza wanaomuamini Mungu, hawafanani uwezo, wengi wanauwezo wa chini kabisa kama ilivyo kwa waganga na wachawi.
Kila mganga au mwanamiujiza atakusaidia kulingana na uwezo wake.

Kwa mfano unaenda kwa mganga kutafuta utajiri, kama mganga uwezo wa akiba yake ya kukupa pesa ni kila mwezi ni 300,000 basi utapata hizo kila mwezi. Au kama ni 200,000 basi utapata hizo kila mwezi, shida ni kuwa hatakuambia kuwa uwezo wake wa kukupa utajiri ni 200,000 kipato kwa mwezi, ila atakuambia anaweza kukusaidia kupata utajiri. Wewe utaondoka ukiwa na matumaini ya kupata utajiri kumbe utajiri anaouzungumzia mwenzako ni 200,000 kwa mwezi kulingana na uwezo wake. Na kweli hizo 200,000 kwa mwezi utapata lakini hutaona amekusaidia kwani wewe ulikuwa unahitaji kwa mwezi walau uingize milioni 6.

Ni sawa uende bank au taasisi ya kifedha yenye uwezo wa kukukopa milioni 10 alafu wewe utake usaidiwe mkopo wa milioni 20, hiyo hiyo haiwezekani, watakachokifanya watakuambia wanaouwezo wa kukukopa hiyo pesa, ila kwanza anza na milioni 10.

2. Uwezo wa mtu wa kupokea uchawi au mibaraka
Watu wanatofautiana vibaba vya kupokelea uchawi au baraka, kuna wenye uwezo wa kupokea uchawi au baraka kubwa na wapo wenye uwezo wa kupokea kidogo kabisa, Inategemeana na Storage capacity.

Huwezi kwenda kwa mganga kutaka utajiri wa milioni mia moja au bilioni moja wakati capacity yako ni inauwezo wa kupokea milioni tano tuu. Hapa ndio ishu ya kuipandisha nyota, kuisafisha nyota kama waitavyo hutokea, kuisafisha nyota ni kama kughushi storage capacity ya mtu iwe kubwa ingawa kiasili ni ndogo, matokeo yake baadaye huwa mabaya ukilinganisha na mtu ambaye ananyota ambaye hata akisaidia matokoe yake mwisho hayawezi kuwa mabaya na hata gharama sio kubwa.

Hata hivyo kwenda kwa waganga ni hatari sana kwani uwezekano wa kuibiwa nyota na hao hao waganga ni mkubwa sana kuliko kusaidiwa. Mganga aonapo nyota yako iko juu(yaani internal storage capacity ) na akikuona huna pesa ya maana ya kumpa zaidi ya kulia lia na kuomba kusaidiwa, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuibiwa nyota/local disk yako na ukapewa local disk kimeo,

Ndio maana inashauriwa au inakatazwa kwenda kwa waganga wa kienyeji au walozi kutaka msaada, msaada pekee upo kwa Mungu,

Waganga au wachawi waibapo local diski au nyota yako huweza kuiuza kwa wateja wao waaminifu wanaowapa pesa nyingi au wanaweza kuitumia katika shughuli zao.
Fahamu kuwa waganga wakienyeji au wachawi ni kama mafundi simu au computer, kazi yao kubwa ni kutengeneza au kuharibu, Nyota au local disk yako ni moja ya spea muhimu katika ofisi zao mbali na malighafi zingine, lakini nyota yako ni spea muhimu sana katika kutatua matatizo yako au matatizo ya wenzako.

3. MUDA WA UCHAWI AU MUUJIZA
Watu wengi hufikiri kuwa baraka hazina expire date au laana hazina expire date jambo ambalo ni uongo kabisa. Kila jambo lina expire date yake, hata katika uchawi na muujiza.
Unapoibiwa 100,000 usidhani ukiomba Mungu amlaani mtu huyo ukadhani laana yako itakaa miaka yote hasha! Au ukadhani kuwa ukimloga mtu kwa kukuibia 100,000 au hata milioni moja ukadhani atalogeka daima, hapana!
Kila baraka au laana, au ulozi au muujiza una expire date yake, hivyo ku-update ni jambo ambalo haliepukiki.

Uchawi na miujiza lazima ia-updetiwe ili iendelee kuwa na nguvu.

Miujiza kuiapdeti ni kutenda yaliyomema ili baraka ziendelee kukutokea na kukufuata. Hivyo kafara kubwa inayotolewa kwenye miujiza ni kujizuia na tamaa ya mwili ili utende mema, wakati kwenye uchawi kafara zipo nyingi sana na zenye gharama kubwa na matokeo hasi siku zote.

Kumbuka; wachawi na waganga wa level ya juu watakaokusaidia kwa mambo makubwa ni wachache,
kama ilivyo kwa madaktari wa uspeshalist walivyo wachache na sio kila hospitali utawakuta ndivyo ilivyo kwa waganga, usikubali kuibiwe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Kwa mtindo huu unaweza kuwa mchawi mzuri sana kama unajua mpaka uchawi unavyotenda kazi, jiandae kusumbuliwa na "wateja" tena umeacha namba kabisa.

Umeandika; uchawi hutenda kwa matokeo hasi, na miujiza hutenda kwa matokeo chanya, sasa hapa kwa mtazamo wangu, vipi ile miujiza tunayoishuhudia makanisani ambayo huku mitaani tunaambiwa imetokana na nguvu za giza?

Inasemekana kuna "watumishi" "manabii" ambao hutumia nguvu za giza kutenda miujiza wakiwa kwenye nyumba za ibada, na vitu kama mafuta ya upako, keki, na maji hutumika. Kwasababu hivi vitu huweza kumsaidia mgonjwa kupona, sasa hapo huoni kama miujiza imepatikana kwa nguvu za giza?
 
Sawa mkuu. Huwezi kujua haya bila kuwa mchawi wa rank fulani. Wewe uko uchawi wa rank gani mkuu?. Ili nijua kabisa nichague niwe mchawi wa level yako au nikuzidi
 
Sawa mkuu. Huwezi kujua haya bila kuwa mchawi wa rank fulani. Wewe uko uchawi wa rank gani mkuu?. Ili nijua kabisa nichague niwe mchawi wa level yako au nikuzidi

Mtu kuelezwa Jambo Fulani haimaanishi yeye ni moja ya Jambo Hilo.

Mimi kuelezea habari za Mungu haimaanishi Mimi ni Mtumishi wa Mungu halikadhalika na mambo ya kichawi.

Mengine tunayajua Kwa tafiti na chunguzi huru
 
Mbona machache Sana Mkuu
Kwangu Mimi hayo ni mengi mno. Yaani mambo ya namba hayo hata nilikuwa sifahamu hata kidogo. Ko hata baadhi ya manabii hasa wale wanaotabiri yajao au kuona yaliyopita inawezekana isiwe nguvu ya ki Mungu eti?
 
Nimepapenda pia hapo kwenye "storage capacity" ulivyohusianisha na nyota, nakubaliana nawe sababu nimewahi kusikia mtu wa freemason hawezi kumuunga mteja mwingine mpaka ajue nyota yake ipoje.

Hii ilitokea tulikuwa tunapiga story na wana, sasa mmoja wetu ikaingia meseji kwenye simu yake ajiunge na freemason, akatuambia akataka na kuifuta ile meseji, tukamwambia usiifute piga hiyo namba tumsikie huyo alietuma meseji.

Jamaa akatetemeka kidogo then akapiga, ikapokewa akajitambulisha, akamwambia anataka kujiunga kama meseji aliyotumiwa inavyosema, akaulizwa majina yake yote matatu, wapi anaishi, mwishowe akaambiwa na yule mtuma meseji ngoja niangalie nyota yako nitakupigia.

Baada ya hapo ndio kimya, jamaa hakupiga tena, nahisi yule mshkaji atakuwa na storage capacity ndogo, au labda ndio alishaibiwa nyota yake, I dont know.

Note. Kwa hili somo ulilotoa nawashauri watu wakiulizwa majina yao na watu wasiowajua, au waganga wa kienyeji wasiwaambie ya ukweli, au wasiwajibu kabisa.
 
Ulichoandika ni kweli, tukiweza kujizuia na tamaa za mwili, tukaenenda kwa kadiri ya mafundisho basi hapo tunakuwa wasafi na miujiza na baraka nyingine inakuwa rahisi zaidi kwetu kuzipata tukimuomba Mungu (Yesu), lakini kumuomba Mungu (Yesu) huku kutwa unawaza wanawake/wanaume ni kujidanganya.

Lile tendo likitumika isivyopaswa au kinyume cha utaratibu kwa mwanadamu linageuka laana, na huo ndio huwa mwanzo wa kukaribisha majanga kwa muhusika, kwasababu huko anakopita na kulala na asiowajua huokota roho za kila aina zinazoweza kuja kumuathiri muhusika binafsi au na kizazi chake mbeleni.

Mfano: mtoto anaweza kuzaliwa akawa na tabia za ajabu za tofauti wazazi wasijue alikozipata, kumbe mzazi aliziokota kule alipokuwa anazurura kuuchafua mwili wake akidhani "anakula bata"
 
Du bro uko sahihi nime cross check na data zangu ( mi sio witch) asilimia kubwa uko sahihi. Na hasa kuhusu nyota.

Nadhani wewe ni ex witch au ume google hizo taarifa na kwa kuwa umeacha namba watu wengi watapigwa mchana kweupe. Bora uwe wazi nia yako ya kuacha namba ya mawasiliano ni nini

Jambo moja ambalo uongezee hapo ni kwamba nguvu iliyo juu ya nguvu zote ni Nguvu ya Mungu kupitia jina la Yesu.

Itasambaratisha nguvu zote hizo top down Na kama mchawi ni king'anga'nizi mfuatiliaji basi atakutana na kifo.

Hata hivyo Mungu ana huruma sana na neema ya ajabu wengi hawafi ila wanashangaa mabomu yao yote hayafanyi kazi kwa watu fulani. Na wanaishia kudhani amekutana na mchawi aliyemzidi maarifa. Ndio anaa nza kuwa na woga na hofu.


Hata hivyo uko sahihi sana kwamba kuna bidii ya ziada kuzipata hizo nguvu za Mungu na kuzi maintain. Naona wewe umetumia neno ku update.
 
Kwahiyo hizi vurugu zote humu ulimwenguni ni matokeo ya ugomvi kati ya Mwenyezi Mungu na mwanae mpendwa lucifer?
 
Mtu kuelezwa Jambo Fulani haimaanishi yeye ni moja ya Jambo Hilo.

Mimi kuelezea habari za Mungu haimaanishi Mimi ni Mtumishi wa Mungu halikadhalika na mambo ya kichawi.

Mengine tunayajua Kwa tafiti na chunguzi huru
Sawa mkuu. Sasa nisaidie nipate kuwa mchawi wa level ya katikati ya pyramid kwenda juu kwa chini hapo
 
Mbona kuna waganga wanaoishi kwenye vijumba vidogo vya nyasi, ila wanatoa uganga wa misukule na mtu anakuwa tajiri mkubwa?
 
Back
Top Bottom