Hii simu imeganda, baadaye ikazimika kabisa

Hii simu imeganda, baadaye ikazimika kabisa

Ctrlp

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
340
Reaction score
285
Habari ya muda huu viongozi.

Kuna hii simu hapa ni TECNO C7 hii simu niko nayo muda mrefu tangu mwaka 2017 sijawahi kupeleka kwa fundi na haijawahi kunisumbua

Sasa juzi hapa nilikua na peruzi humu jf kupitia app ghafla ikaganda ikawa haifanyi chochote.

ikanibidi nijaribu kuizima napo ikawa haizimiki basi nikachukua uamuzi wa kutoa battery halafu niirudishe

baada ya kurudisha battery ikawa inawaka lakini inaishia kwenye logo halafu haiendelei.

Nikaipeleka kwa jamaa fulani basi akaukorokochoa ila hakuifungua basi ndo akaizima kabisa kwa sasa haiwaki wala moto haionyeshi kama inapeleka..

naomba mafundi mnambie kama inaweza kupona nikaitumia tena..

Location: Dodoma
 
Duu ingekua inatoa chochote ningekuambia ijaribu kwenye pc kama ingesoma, hapo mchezo ungeishaa, ngoja wengine waje..

Ila mkuu ionee hio simu hurumaaa..
Tecno kwa miaka 3, ni more than fair...
Life span ya uhakika ya simu nyingi ni 3yrs hata watengenezaji wanatengeneza kwa kujua hilo.
 
Ooh pole sana mkuu, hiyo tupa kule maana haitapona kabisa. Ndo mtindo wa simu za tecno, zinakufa kihivo yani.
Nilikuwa na J7 ilikufa kizembe hivo hivo
 
Mkuu walanti ya simu za techno ni 1 yr,sasa wewe kama umeitumia toka 2017 hadi Leo ni almost 2+ ,sasa swali ulitaka ukae nayo miaka mingapi ndo ulidhiki?

Nunua simu nyingine,Mimi huwa nakama na simu 1yr baada ya hapo nauza nanunua nyingine
 
Duu ingekua inatoa chochote ningekuambia ijaribu kwenye pc kama ingesoma, hapo mchezo ungeishaa, ngoja wengine waje..

Ila mkuu ionee hio simu hurumaaa..
Tecno kwa miaka 3, ni more than fair...
Life span ya uhakika ya simu nyingi ni 3yrs hata watengenezaji wanatengeneza kwa kujua hilo.

Hii 3 years sio kwa Apple Devices.
 
Mkuu Walanti ni 1 yr kwa simu za tecno
 
Peleka kwa fundi ataifanyia factory reset na itapona,hiyo wenyewe mafundi wana mbinu za kuiamsha itawaka tu hiyo mkuu...
 
Hii 3 years sio kwa Apple Devices.
Mkuu Walanti ni 1 yr kwa simu za tecno

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Wakuu hapa sikua namaanisha warranty..
Max warranty inakuaga ni 2yrs na mengins ni 1yr, refurb ni miezi..
Hiki ni kipindi ambacho wanajua simu ukiitumia vizuri basi itatoboa....
Na ukishafika mwaka wa tatu kuendelea uhakika huo haupo tena, ndio maana kampuni haihusiki tena..

HAKUNA KAMPUNI YA SIMU YENYE WARRANTY YA MIAKA 3.
 
Peleka calcare wataitengeneza. Hiyo simu ina tatizo la software. Na huo mtindo wa simu kutokuwaka wala kupokea moto linatokea kwa simu kama hizo.

Nilishashuhudia shida kama hiyo kwenye tecno Phantom pad mini na tecno L3. Simu inaweza isiwake wala kupokea charge lakini kwenye PC inaonekana kwa hivyo jamaa wataiFlash na Stock Rom. Usikubali fundi aipige hot gun maana ataiharibu kabisa.

From JF App
 
Duu ingekua inatoa chochote ningekuambia ijaribu kwenye pc kama ingesoma, hapo mchezo ungeishaa, ngoja wengine waje..

Ila mkuu ionee hio simu hurumaaa..
Tecno kwa miaka 3, ni more than fair...
Life span ya uhakika ya simu nyingi ni 3yrs hata watengenezaji wanatengeneza kwa kujua hilo.
hahaha mkuu lakini si unajua sisi wazee hatuna mambo mengi
 
Peleka kwa fundi ataifanyia factory reset na itapona,hiyo wenyewe mafundi wana mbinu za kuiamsha itawaka tu hiyo mkuu...
shukrani kiongozi ngoja nifanye hivyo huenda bado bahati ikawa upande wangu
 
Peleka calcare wataitengeneza. Hiyo simu ina tatizo la software . Na huo mtindo wa simu kutokuwaka wala kupokea moto linatokea kwa simu kama hizo. Nilishashuhudia shida kama hiyo kwenye tecno Phantom pad mini na tecno L3. Simu inaweza isiwake wala kupokea charge lakini kwenye PC inaonekana kwa hivyo jamaa wataiFlash na Stock Rom. Usikubali fundi aipige hot gun maana ataiharibu kabisa.

From JF App
asante kiongozi kwa hapa dodoma wana ofisi kweli??au hadi nikirudi dsm kariakoo kule
 
ahaa kwahyo huenda kuflash kukasaidia,hawawezi wakaiua kabisa kwel!!
 
Back
Top Bottom