Musoma Yetu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2016
- 2,633
- 2,297
Hii shule kwa ufupi imetamkwa Mara nyingi sana. Kiukweli imebidi niitembelee maana ghafla imeingia historia ya nchi kwa mwanasiasa mmoja mashuhuri ambae anaongoza kutajwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii. Ila tuwe tunakumbuka tuliko toka, maana mazingira ya shule pia yamechakaa sana. Ile pesa ya ukarabati ule kwenye ofisi ya CCM ingekuja hapa, hata mazingira ya kusomea yangevutia zaidi na ufaulu kuongezeka zaidi.