Hii series ya Daudi na Goliati imenibamba sana

Hii series ya Daudi na Goliati imenibamba sana

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,459
Nimetokea kuikubali sana hii series

  • Maisha ya Daudi akiwa mchungaji wa kondoo huko milimani akipambana na wanyama wakali huku kaka zake wakiwa nyumbani
  • Maisha ya mfalme Sauli aklivyolewa sifa kuona mafamiko yote ni yake na jinsi alivyo kiuka maagizo ya Mungu
  • Nabii Samueli alietumika kumsaidia Sauli kuwa Mfalme alivyoona kapoteza Dira na kumteua Daudi awe mfalme kwa maelekezo ya Mungu.
  • Jinsi Sauli alivyoteswa na mauza uza baada ya kupewa laana na Sauli
  • Kipaji kikubwa cha Daudi kuweza kupiga chombo cha muziki kilivyoweza kumtuliza Sauli na kupewa kazi Ikulu
  • Penzi la siri ndani ya ikulu kati Daudi na mtoto wa Sauli pamoja na upinzani mkali toka kwa watoto wa matajiri na viongozi wakubwa waliotaka kumuoa.
  • Nabii Samueli alipoenda kumfuata Daudi, Baba yake Daudi aliwaleta kaka zake tu, ilibidi Daudi akatafutwe milimani kwasababu ndie aliechaguliwa
  • Stori inaonyesha Goliati hakuwa na noma wala kutaka kujichanganya na watu, aliishi huko porini kwenye pango kubwa, Mfalme wa wafilistini alimfuata Goliati kumshawishi awe sehemu ya jeshi lake ila Goliati akatoa sharti yeye ndio awe mfalme, dili likashindikana , kilichotokea ulichezwa mchezo mchafu kuua furaha ya Goliati na kusingizia ni Israel,
  • Watoto wa Sauli, moja akiwa ameendekeza umalaya na ulevi, mwengine akiwa hodari mzalendo wa taifa

Uzuri wa hii series mnaweza kuangalia na watoto wenye miaka 13+, Hakuna vipande vya Sex, mapenzi ya jinsia moja wala lugha ya matusi, ila kuna scenes fupi za kukiss pale Daudi alipomkata kichwa Goliati na kupewa mke binti wa Sauli


View: https://youtu.be/GrGfIHBIVL4?si=9t7KFVvdLbwE8ddq
 
Back
Top Bottom