Hii picha imeniponza!

Hii picha imeniponza!

Kama kawaida yangu huwa siachi kamera yangu kwa ajili ya matukio mabali mbali jijini Dar.

Nilipita Ocean Rd na nikaona watu wamepumzika na kupunga upepo.Mimi nikatoa kamera yangu na kuchukua hali ile mwanana.

Mara aktokea Afwande Arufonsi na kuniuliza

"haroo rete kibari chako"

"S..sina.. kibali afwendi kwani kupiga picha hapa inakuwaje" nikamjibu

"Wewe rinatoka wapi, na kama hujui kuwa hapa hakuna ruhusa twende kituoni" Arufonsi akawa mkali

"B... basi afwendi nihurumie nina mke na watoto wanao nitegemea" nikamjibu

"Araaa hutaki kwenda kituoni sioo, ohoo wewe hujui hapa ni njia ya ikuru" bado Arufonsi mkali.

Hapo nikaona nimpooze kidogo,

"Afwande mimi Mbongo pyuwa, na najua hujaweka chochote tumboni, chukua hii kapate ranchi basi"

Kwa mara ya kwanza nikaliona gego la afwande Arufonsi " Nenda sako, hapa mahari pa usarama"

ulienda na msafara wa maharusi??
 
Usirudie kuripa rirushwa rire riArfonsi. Ukiriona tena risiku ringine riambie ww ni mdogo wa rire riafande Angerina ritaogopa
Ha ha ha!
Arafu ririkuwa na sura kama buti rake
 
Picha nzuri, japo ya kawaida tu!
Lakini kutoa rushwa ni kosa ndugu yangu!
 
Picha nzuri na pole mkuu, huu ni ulimbukeni wa watu masikini kwa ikulu na njaa ya huyo afandi koko - watu waingia white house kutembea na kupiga picha na walinzi wa usalama ni tabasamu tu wanatowa
 
Usirudie kuripa rirushwa rire riArfonsi. Ukiriona tena risiku ringine riambie ww ni mdogo wa rire riafande Angerina ritaogopa
Inamaana ile hela uliotoa ndio maana ya usalama wa kwenda ikuru? sasa kama ungekuwa umetega bomu si watu wangekufa kwa kiasi hicho ulichotoa pole sana hata mimi yalishanikuta ila bahati nzuri nilikuwa sijapiga hata picha moja ila nilikalishwa hapo kuanzia saa tisa hadi kuminambili jioni pamoja nakutoa kitambulisho changu cha chuo pole sana ndio TZ yetu hiyo ya kisasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom