Hii ni tathmini yangu ucl 2010/2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni tathmini yangu ucl 2010/2011

Discussion in 'Sports' started by Observer2010, Mar 21, 2011.

 1. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nikiwa kama mchambuzi wa soka la kimataifa niliyebobea na pia muangalizi wa kimataifa (INTERNATIONAL OBSERVER) katika masuala ya soka nisiye na upendeleo wala ushabiki wa timu yoyote, huu ndio uchambuzi wangu wa hii ligi bora zaidi hapa duniani baada ya kufanyika kwa draw siku ya ijumaa.

  Hapa napanga magame kwa kufuata urahisi wa matokeo kama ifuatavyo.

  Game 1. Inter Milan vs Shakle 04

  Hili ndio game jepesi zaidi kati ya magame hayo manne, na ni jepesi kwa kuzingatia uwiano wa uwezo wa hizi timu mbili. Shakle 04 imekuwa katika kiwango kibovu sana, na hata kufika hapo imekuwa ni kama bahati kubwa sana. Kwenye table ya Bundesliga, Shakle ni timu ya 10 na ikiwa na point 5 tu zaidi kutoka ukanda wa kushuka daraja. Inter Milan imekuwa inaimarika kadri siku zinavyoenda baada ya kumtimua kocha wao Raphael Benitez na kumuweka Leonardo. Kwa siku kadhaa zilizopita ilikuwa point 10 nyuma ya vinara wa serie A ila mpaka sasa wamepunguza gap na kubaki point 2. Samuel Etoo Fils pia amekuwa katika kiwango bora sana na mwiba mkali kwa wapinzani, na ndiye atakayekuwa tishio kubwa kwa Shakle 04.

  Tathmini: Inter Milan watavuka kwenda nusu fainali.

  Game 2. Chelsea FC v Manchester United

  Wakati kiwango cha Chelsea kikizidi kuimarishwa na usajili walioufanya mwezi wa kwanza especially usajili wa David Luiz, ambaye amefill vema kabisa gap la beki wa kati lililokuwa limeitatiza sana Chelsea baada ya kumuuza Ricardo Calvarho na kuumia kwa Alex, kiwango cha Manchester United kimekuwa kikiporomoka kwa siku za karibuni na hii ikichagizwa zaidi na idadi kubwa ya wachezaji muhimu kuwa majeruhi. Bila ya kuwa na central defenders wenye udhoefu mkubwa Nemanja Vidic na Rio Ferdinand, hakika Man U wapo katika hali tete sana especially kuweza kuwazuia killing strikers wa Chelsea.

  Tathmini: Chelsea FC itavuka kwenda nusu fainali.

  Game 3. FC Barcelona v Shaktah Donetsk

  Naamini watu wengi mtakuwa mnashangaa kwa nini hili game ni gumu kuliko la Manchester United v Chelsea. Asilimia kubwa ya wapenda soka wanaona Shaktah ni kama ashatoka, lakini binafsi nawaambia unapocheza na timu ambayo ipo katika hali ya kwamba they have nothing to loose, hapo tegemea upinzani wa hali ya juu mno. Shaktah imekuwa katika kiwango bora sana katika siku za karibuni ikiwa inaongoza ligi ya nyumbani mbele ya Dynamo Kiev kwa pointi 12, na huku msimu huu ikiwa imefungwa game moja tu katika Champions league huku ikiwa haijadraw mchezo hata mmoja katika mechi 8 ilizocheza, kumbuka ilimaliza ikiongoza kundi la Arsenal. Itakuwa ni mechi ngumu sana hasa ukizingatia poor performance ya Barcelona kwenye away games katika Champs League na kiwango bora kabisa cha Shaktah katika mechi za nyumbani. Kosa pekee Shaktah ambalo wakifanya litawacost ni kwenda Camp Nou na mentality ya kudefence zaidi.

  Tathmini: Kwa uwepo wa Leonel Messi, Xavi Hernandez na andes Iniesta, natoa nafasi kwa Barcelona FC kuvuka kwenda nusu fainali.

  Game 4: Real Madrid v Totenham Hotspurs
  Hii ndio the best counter katika hizi mechi za robo fainali. Kiwango bora kabisa cha Totenham katika msimu huu sana sana wanapocheza na timu kubwa ndio ogopesho kubwa kwa Madrid. Wakiwa na play maker anayeaminika kuwa ni bora zaidi kwa sasa katika ligi ya Uingereza Luka Modric, pia wakiwa na the rising star Gareth Bale, pamoja na attacking midfielder bora zaidi Mdutch, Rafael Van Der Vart ambaye Madrid ilimdrop huku wakichagizwa na winga tereza Aaron Lennon na Msauzi Steven Pieneer. Huku holding midfielder ikishikiliwa vyema kabisa na Mbrazil Ranieri Sandro, Madrid watakuwa na kazi sana kuweza kuvuka hiki kikwazo. Upungufu mkubwa wa Totenham ni ukosefu wa killing striker. Tegemeo kubwa kwa Madrid ni uwepo wa the special one, Jose Morinho katika benchi la ufundi. Hapa lolote linaweza kutokea, hii ni 50/50 game.

  Tathmini: Kukiwa na uwezekano mkubwa wa Christiano Ronaldo kukosa game la kwanza ndani ya Santiago Bernabeu baada ya kuumia harmstring, Madrid watakuwa na wakati mgumu sana. Natoa nafasi kwa Totenham Hotspurs kuvuka kwenda nusu fainali.

  Baada ya huo uchambuzi, katika nusu fainali magame yatakuwa kama ifuatavyo.

  Game 1. Inter Milan v Chelsea FC
  Tathmini: Hapa Chelsea FC itavuka kuelekea fainali.
  Game 2. Barcelona FC v Totenham Hotspurs
  Tathmini: Barcelona itavuka kuelekea fainali

  Hivyo basi mechi ya fainali itakayopigwa katika uwanja wa Wembley tarehe 25 May 2011 itakuwa ni kati ya,
  FC BARCELONA v FC CHELSEA

  Na hivyo basi, bingwa atakuwa ni :behindsofa::behindsofa::behindsofa: !

   
 2. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Observer 2010 ,hongera kwa kuweka mada hii hapa robo fainali ya mwaka huu iko 50-50 kwa game karibu zote
  Game 1. Inter Milan vs Shakle 04
  Tangu Leonardo ameichukua Inter,wachezaji wameweza kujiamini tena ,na hata magoli waliyofungwa na Bayern mengi yalikuwa ni uzembe wa kipa Julio Cesar kurudi kwa Iniesta kumerudisha makali ya fowadi ya Inter inayoongozwa na Etoo,
  Kura yangu nawapa Inte
  r

  Game 2. Chelsea FC v Manchester United
  Hii game itakuwa ngumu sana kutokana na timu zote kuwa na defence nzuri,vidic atarudi kuja kupambana na Torres kumkosa David Luiz itakuwa pengo kubwa sana kwa Chelsea maana kwa sasa ndio mchezaji bora zaidi kwenye defence na pia anasidia kwenye mashambulizi.Tatizo Anceloti hadi leo hajatengeneza pair ya srtiker ,huenda hii game ikaenda hadi kwenye penati
  Kura yangu nawapa ManU


  Game 3. FC Barcelona v Shaktah Donetsk

  Kwa sasa Baraca hawako kweny form sana hasa Foward yao kwa sasa imekuwa butu sana,kumkosa Puyol na Abidal itakuwa pigo sana hawa Shakhtar wana wachezaji kutoka Brazil kama Costa,Eduardo,Wiliam,Fernandinho,Luiz Adriano lakini hawana defence ya kuweza kuizuia Barca kama Pedro,David Villa na Messi
  Kura yangu nawapa Barca


  Game 4: Real Madrid v Totenham Hotspurs
  Hii itakuwa mojawapo ya mechi nzuri sana kwaenye robo fainali Spurs wana viungo wakali sana kama Mondric,Van De Vart,Pienaar na mawinga wakali kama Bale na Lennon ingawa wana tatizo kwenye defence na tatizo kubwa la Madrid ni kumtegemea sana Ronaldo
  Kura yangu nawapa Spurs

  Nusu fainali
  Inter Vs Man U
  Barca Vs Spurs   
 3. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Belo, ngoja tuone itakuwa vp wiki chache zijazo. So unatoa nafasi kwa timu zipi kucheza fainali ?
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Fainali ni baina ya Barca na Man utd.
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Game 2. Chelsea FC v Manchester United

  Wakati kiwango cha Chelsea kikizidi kuimarishwa na usajili walioufanya mwezi wa kwanza especially usajili wa David Luiz, ambaye amefill vema kabisa gap la beki wa kati lililokuwa limeitatiza sana Chelsea baada ya kumuuza Ricardo Calvarho na kuumia kwa Alex, kiwango cha Manchester United kimekuwa kikiporomoka kwa siku za karibuni na hii ikichagizwa zaidi na idadi kubwa ya wachezaji muhimu kuwa majeruhi. Bila ya kuwa na central defenders wenye udhoefu mkubwa Nemanja Vidic na Rio Ferdinand, hakika Man U wapo katika hali tete sana especially kuweza kuwazuia killing strikers wa Chelsea.

  Tathmini: Chelsea FC itavuka kwenda nusu fainali.
  [/FONT][/QUOTE]

  mkuu hapo umeleta unazi kidogo... remember vidic will be back come may, fletcher na park wanarudi hivi karibuni.. kurudi kwa valencia kumeongeza nguvu ya mashambulio kule mbele, bado sioni chelsea watatokaje hapo, ni ngumu sana kutabiri nani atasonga mbele kwa mechi hii mechi nyingine ngumu kutabiri ni madrid vs spurs hii nayo itakua ngumu sana
   
 6. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu hapo umeleta unazi kidogo... remember vidic will be back come may, fletcher na park wanarudi hivi karibuni.. kurudi kwa valencia kumeongeza nguvu ya mashambulio kule mbele, bado sioni chelsea watatokaje hapo, ni ngumu sana kutabiri nani atasonga mbele kwa mechi hii mechi nyingine ngumu kutabiri ni madrid vs spurs hii nayo itakua ngumu sana[/QUOTE]  Sijaweka unazi mkuu, mimi binafsi nipo neutral kabisa, sina unazi wa timu yoyote ya Europe. Km Vidic atakuwa amerudi na atakuwa fit basi ugumu wa mchezo utaongezeka sana. Hii itategemea pia na fitness yake, maana hapa tunaongelea wiki mbili tu zijazo. All in all bado tathmini yangu haitabadilika. Kuna nafasi ndogo ya Man U kuiondoa Chelsea, kuliko otherway round. Lets wait and see.
   
 7. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ule usiku wa champions league ndio umewadia. Someni kwa umakini hii tathmini then by next week tutakuwa tushapata majibu halisi.

  Game of the night leo ni Real Madrid vs Tottenham Hotspurs. Huku timu zote zikiwa na lundo la majeruhi, lakini bado kutakuwa na burudani nzuri sana kwa sisi wapenda mpira.
   
 8. k

  kiparah JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kweli hii ni tathmini yako!
   
 9. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  David Luiz yuko cup tied kwa hiyo hachezi UCL msimu huu, tangu umeandika hii tathmini yako wachezaji wengi wa Man Utd wamerudi Valencia, Vidic, Park wakati Rio, Rafael na Anderson wametrain na timu leo.
   
 10. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mkuu utabiri wako nimeupenda sana na binafsi niko tayari kukupa nafasi ya kubadili msimamo. good try
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Mpaka sasa predictions zako kuhusu mechi za jumanne zimekwenda kinyume, Spurs na Inter wote wamepigwa...
   
 12. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wadau ni mapema sana kuzungumza na kucomment kuhusiana na hii tathmini, japo ilikuwa ni shocking defeat kwa bingwa mtetezi tena akiwa nyumbani. Mechi ya Madrid v Tot iliamuliwa mapema kabisa (dk. 15) kwa kadi nyekundu ya Crouch, hebu tuone mwisho wa hii tathmini then ndio tutaelezana imefanikiwa kwa kiwango gani.
   
 13. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Du! Yaani bado unamatumaini na prediction zako?
   
 14. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #14
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Matumaini yote yamepotea, na huu ndio utamu wa mpira wa miguu ! Ngoja tuone semi finals zitakuwaje, baada ya hii tathmini kufanikiwa kwa kiwango cha asilimia 25 tu.
   
Loading...