Hii ni Taifa Stars iliyoifunga Zambia kuingia African Cup (Tumemkumbuka Peter Tino, tumemsahau Thuwein Ally)

Hapo Kibaden akitupia Hat-trick kama nakumbuka vizuri.

Na ndiyo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Kibadenni kuifunga Yanga akiwa Simba. MWaka uliofuata mkuu wa mkoa wa Songea aliyeitwa Gama alimchukua kukuza kiwango cha mpira kule Songea kwa timu yake iitwayo Majimaji.

Na kweli Majimaji ikaibuka na kuna wakati mwaka 1983 ilikuwa na wachezaji Taifa Stars kama Celestinde Mbunga, Octavian Mrope.
 
Wachezaji wa zamani walikuwa na ufundi sana . Ukitaja zamoyoni mogela, au lunyamila au Tino au kibadeni au amasha ni hatari kweli sio mchezo uwanjani. Wachezaji wa siku hizi hawana ufundi. Ili tufanikiwe Misri inabidi coack amunike Azibe ule udhaifu wa vipaji kwa kuongeza kasi ya uchezaji/ stamina kwa kiwango cha msuva kila mchezaji awe hivyo.
 
Tunaongelea kilichotokea August 1979 hadi March 1980. Edibiliy Lunyamila amewika kwenye challenge January 1993 kule Uganda, Yanga ikachukua ubingwa.
Challenge cup east and central Africa Taifa stars ilishinda kombe Nairobi ,kenya kwa kumfunga Uganda walikuwepo kina lunyamila, masha, nemes nk mchezaji iliyewika alikuwa lunyamila. Kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati lunyamila ameshinda mara mbili. 1993 na 1999 Kampala Uganda
 
Hakuna tatizo kuwa Simba damu na ni kweli mimi ni Simba damu. Na wakati Taifa Stars inaenda Nigeria Simba ndiyo ilikuwa inashikilia ubingwa wa Tanzania kwa miaka mnne mfululizo na miaka mitatu nyuma yake tulikuwa tumemchapa Yanga goli 6-0, mwaka 1977.
Ulivyoandika inaonesha haupo neutral. Usisahau hiyo unayoiita Pan Africa ilikuwa ni Yanga tu. Kwa mheshimiwa (ingawa ni Simba) alichofanya ilikuwa ni sahihi kumtambua aliyefunga bao la kutuwezesha kwenda African Cup> Ushabiki mwingine ulipouonesha ni pale ulipozungumzia Golden Boy ila hukuzungumzia kiboko yake Chama alivyokuwa anamdhibiti mpaka Jongo akaanzisha msemo wa man to man.
Hebu msikilize Jongo alipokuwa anatangaza kuhusu hiyo mechi kuanzia 4:50: ..... tunakwenda lagos.....

1: HATUA ZA MAKUNDI:

Kwanza turekebishe jina, kuna watu wanasema tunaingia AFCON mara ya pili, wakati ule mwaka 1980 ilikuwa ni African Cup, jina AFCON limekuja miaka ya karibuni.

Thread zilizopita zimeongelea sana kuhusu Peter Tino, mchezaji aliyeifungia Taifa Stars bao lililotupeleka Nigeria. Hebu tujikumbushe mambo yalivyotokea na JF ionekane ni mahala pa kukimbilia data.

Kwanza kabisa, ingawa watu wanasema ni mwaka 1980 ukweli ni kwamba mechi tunayoisema ilifanyika mwishoni mwa mwaka1979, tena tukiwa na uchumi mbovu kutokana na kumalizika kwa vita ya Tanzania na Uganda.

Mechi ile tulikuwa tunahitaji draw ili tuingie finali na Zambia walikuwa wanahitaji ushindi na mechi ilifanyikia Ndola, Zambia.

Katika dakika ya 20, Zambia wakapata bao la kuongoza Hadi half-time Zambia (1) na Tanzania (0).

Kipindi cha pili timu zote ziliongeza kasi lakini Zambia ikiutawala mpira zaidi na ikishangiliwa uwanja mzima. Kuna waandishi husema mshambulia hatari wa Zambia, Godfrey Chitalu, hakufua dafu. Huu si ukweli.

Zambia ilitawala mchezo na golikipa wa Tanzania, Juma Pondamali alipohojiwa na waandishia alisema alimwogopa sana Godfrey Chitalu kwani alikuwa anapiga mikwaju hatari na yeye anaipangua.

Hadi watu wanaanza kuondoak uwanjani na wengine kuacha kusikiliza redio walijua Taifa Stars imetolewa. Ndipo zikiwa zimebaki dakika 2 kumalizika mchezo, Peter Tion akaifungia Taifa Stars bao lililotupeleka Nigeria.

Formation ya wakati huo ilikuwa ni 4-2-4. List ya mchezo huo kama nitaikumbuka vizuri ninaiandika humu, kama ina makosa madogo wanaokumbuka wanisahihishe.

01: Juma Pondamali, (Pan)
02: Leopard Tasso, (Balimi-Bukoba)
03: Mohammed Kajole, (Simba)
04: Salim Amir, (Costal Union)
05: Jella Mtagwa, (Pan)
06: Leodegar Tenga, (Pan)
07: Hussein Ngulungu, (Pan)
08: Omari Hussein, (Yanga)
09: Peter Tino, (African Sports)
10: Mohamed Salim, (Costal Union)
11: Thuweni Ally, (Simba)

2: FINALI (NIGERIA):
Baada ya kufuzu hiyo mechi ya mwaka 1979, ndipo fainal zenyewe za AFRICAN CUP zikafanyika March 1980. Mambo yalikuwa hivi huko Nigeria. Tanzania ilipangwa na wenyeji Nigeria, Egypt na Ivory Coast, siku hizi inaitwa Cote d'Ivoire (tamka kwodivaa).

Mechi ya ufunguzi, March 08, 1980, Tanzania tukacheza na Nigeria kwenye uwanja uitwa Surulele, Tanzania tukachapwa 3-1. Nigeria ilikuwa a washambuliaji hatari kama Ousegun, kwa kifupi Segun, Tunde Obamidele. Bao la pekee la Tanzania likafungwa na Thuwein Ally, mzanzibari pekee katika timu ya Taifa.

Mechi ya pili March 08, 1980, Tanzania tukacheza na Ivory Coast, tukachapwa 2-1. Hapo pia bao la pekee la Tanzania likafungwa na yuleyule Thuwein Ally. Kimsingi tukawa tumeshatolewa mashindanoni tukabaki kukamilisha ratiba.

Mechi ya tatu nimekosa kumbukumbu ilichezwa lini lakini cha uhakika ni kwamba Tanzania itulicheza na Egypt, tukatoka sare 1-1. Hapa tena bao la pekee la Tanzania likafungwa na yuleyule Thuwein Ally.

3: JUMA PONDAMALI, PETER TINO, THUWEIN ALLY, ABDALAH KIBADENI:

NImesoma mahala kwamba Peter Tino ameenziwa, sijui ni kweli au la maana sijaipitia vizuri taarifa hiyo. Lakini tukifanya tathmini vizuri, pale Zambia aliyengara alikuwa ni golikipa Juma Pondamali maana Taifa Stars ilizidiwa kasi kwa muda mwingi wa mchezo na Pondamali ndiye aliyeokoa michomo mingi ya wazambia.

Mwishoni wlalipobadili mbinu ndipo Peter Tino akasawazisha. Kama ni man of the Match alikuwa ni Juma Pondamali na si Peter Tino maana alikokoa magoli mengi ya wazi tena wakati mwingine defense imeshapitwa yote.

Kule Nigeria tumeona kwamba Tanzania ilikuwa inapata goli moja kila mechi, mfungaji akiwa ni Thuwein Ally. Huyu alikuwa ni mchezaji wa Simba akitokea KMKM ya Zanzibar.

Yale magoli matatu yalimfanya Thuwein Ally asifike maana hakuwa anajulikana sana na ndiyo yalifanya aonekane Simba imepata mchezji mzuri.

Sifa ya Thuwein Ally ilikuwa ni mashuti makali ya mguu wake wa kushoto. Kuna shuti alipigia free kick pale CCM Kirumba wapo wanaoamini lilikuwa ni moja ya mashuti makali kupigwa hapa nchini.

Hivyo, kule Nigeria, Thuwein Ally alituletea sifa Tanzania na hata jina lake likabadilika kuwa mfungaji wa magoli matatu kule Nigeria. Hivyo, kwa washabiki wa kipndi kile Thuwein Ally alivuma kuliko Peter Tino.

Peter Tino hakuvuma sana wakati ule kwa sababu hata timu aliyokuwa yaani African Sports ya Tanga, ukiachilia uhasama na Coastal Union, haikuwa tishio.

Kimsingi, Peter Tino hakuvuma sana zaidi ya hilo goli la pale Zambia. Mtu aliyekuja kuvuma alikuwa ni beki (centre half) Jelah Mtagwa ambaye hadi aliwekwa kwenye Stamp ya Posta, yaani ukituma barua lazima uone picha ya Jellah Mtagwa.

Leodgar Tenga hakuendelea sana a mpira liukweli ni kama vile alistaafu mpira kipindi hicho aana nadhani alijikita zaidi na tmasomo pale Chuo Kikuu.

4: ZAMOYONI MOGELA:
Mwaka 1980 wote uliisha baridi namna hiyo ndipo mwaka uliofuata (1981) akaibuka mshambuliaji Zamoyoni Mogela, kwenye mashindano ya CECAFA, ambako kama Thuwein Ally, zile mechi tatu alikuwa lazima afunge goli hadi kikamfanya aitwe Golden Boy.

Kimsingi Peter Tino na Thuwein Ally walikuja kipindi ambapo Abdalah Kibadeni umarufu wake ulikuwa unaondoka na hasa alipoanza ukocha kwa Majimaji ya Songea mwaka 1978.

Hivyo, mwaka 1978 hadi 1980 hakukuwa na mshambulia anayemiliki jina ndiyo maana mtu akiibuka kwenye mechi moja anatawala kidogo kama Peter Tino na Thuwein Ally.

Lakini Thuwein Ally alimzidi umaarufu Peter Tino kama ilivyoelezwa huko juu, kutokana na magoli matutu kule Nigeria. Lakini hawa wote wawili walizidiwa na Zamoyoni Mogela kuanzia Novemba 1980 hadi Mogela alivyoacha mpira.

Kama mnakumbuka mwaka 2011, Zamoyoni Mogella alipewa nishani ya kitaifa kuwa mchezaji bora kwa miaka 50 ya uhuru. Hawakukosea waliofanya hivyo.

Kuna wanaosimulia goli ambalo Zamoyoni Mogela alimfuga golikipa Juma Mhina wa Pamba pale CC ingekuwa sasa hivi lilikuwa linafungwa Ulaya, alimfunga baada ya kuipiga chenga difensi nzima ya Pamba na kumdanganya kipa kwenye upenyo mdogo akaingizia hapohapo goli.

Peter Tino alikuja kuhamia Pan mwaka 1981 na hata hivyo hakufua dafu kwa Mogela ambaye kila timu ilikuwa inamuwekea beki maarufu. Yanga ilikuwa inamuwekea beke aliyeitwa Athuma Chama akisaidiwa na Yusuf Bana.

Peter Tino alizidiwa hata na Madaraka Selemani wa CDA ya wakati huo aliyeweza kupiga chenga defense nzima. Peter Tino alisaidiwa sana na urefu wake. Hivyo, suala la Peter Tino unaweza kuliangalia namna hii.

WANASIASA KUVURUGA UZALENDO:
Kingine ni kwamba wakti ule kulikuwa na chama kimoja tu CCM na hata kama kama timu ilisaidiwa au kuhamasishwa waljitokeza kwa nadra sana akijitahidi ni Waziri anayehusika na michezo. Ungeonekana ni kichaa kutojua Taifa stars inacheza, achilia mbali kutoishangilia.

Leo soka imeanza kuingiliwa na wanasiasa, tena wengine hata hawana historia ya mpira na historia hii inayoelezwa humu huenda ni ngeni kwao. Walikuwa wapi wakati huo, jibu mnalo.

Licha ya hayo UCHADEMA na UCCM unaonekana. Akitokea sana mwanasiasa wa chama tofauti akajikita inaonekana anavutia chama chake na ni kweli mwakani atafanya kampeni kwamba kawezesha yeye na chama chake.

Matokeo yako kama timu imewezeshwa na mwanasiasa wa CHADEMA basi yule wa CCM yuko radhi timu ifungwe ilie CHADEMA isije ikachukua sifa hiyo!

Kimsingi, wanasiasa wa vyama vyote wanavurugua utamu wa mpira na walitakiwa wabaki hukohuko kwenye majukwaa ya siasa.

NAWASILISHA.
Makala nzuri. Asante kwa madini.
Labda huyo Leodgar Tenga angeulizwa kuhusu wachezaji aliokuwa nao wakati huo.
Maana kumuenzi yeye tu na Tino na kuwatenga wenzao wakiwemo Thuwein Ally aliyefunga bao kila mechi na Pondamali aliyeokoa sana, sio sawa.
 
Asante kwa kumbukumbu nzuri, lakini ingependeza zaidi kama ungetoa ushauri hapa kwamba nini kifanyike kwa siku za usoni katika kuweka kumbukumbu za mashujaa wetu wa michezo mbalimbali na jinsi ya kuwaenzi tafadhali!
 
Makala nzuri mana yake imefumua mambo ambayo ulikuwa huyajui na sasa umeyajua na kwa hilo nimefaulu lengo nililojipangia. Kama wewe una lengo jingine zaidi ya hilo fanya hiyo kazi wewe.
 
Nilifikiri umeibua kumbukumbu hizo ili kuweka sawa rekodi na kuonyesha makosa yaliyojitokeza, nilidhani basi ungekuwa na mapendekezo zaidi kuhusu nini kifanyike going forward sasa ulivyonijibu nikaona kumbe ni walewale wadanganyika walalamikaji tu bila kupendekeza suluhisho, kama ni hivyo basi umepoteza muda wako bureee!!, endelea kulalamika kama kuna tija! vinginevyo Peter Tino huyoo keshajiondokea na 5m zake!
 
Wewe mwenyewe umeshasema kuweka sawa historia, maana yake tuukumbaite ukweli wa yale yaliyotokea.

Historia ni jambo lililotokea na haliwezi kufutwa. Kunapotokea wanaoifuta historia tunawakumbusha na ndicho nilichokifanya.

Umeisoma makala hii kama mwanafunzi usiyejua kilichotokea na hiyo ni faida kwako.
 
Whatever bana! mi nimefurahi kuwafunga tu waganda walitudominate sn recently na am sure hata WAJE TENA!!!
 
01: Juma Pondamali, (Pan)
02: Leopard Tasso, (Balimi-Bukoba)
03: Mohammed Kajole, (Simba)
04: Salim Amir, (Costal Union)
05: Jella Mtagwa, (Pan)
06: Leodegar Tenga, (Pan)
07: Hussein Ngulungu, (Pan)
08: Omari Hussein, (Yanga)
09: Peter Tino, (African Sports)
10: Mohamed Salim, (Costal Union)
11: Thuweni Ally, (Simba)
.
Hiyo timu ilikuwa ni spririt ya Bukoba, kwa hakika wadau wa pande hii wana haja ya kufikiri juu ya kuifufua timu hii ya wananchi hata kwa jina jipya kama Bukoba united and the like.
Na inabaki katika historia kwa kutoa mchango uliodumu kwa miaka 39!
 
Kaka ndiyo uzuri wa history. Tukikaa kimya kuna watu watatutengeneza history.
 
Asante sana SubiriJibu kwa uzi huu, najua inaweza kuwa kasehemu kadogo ka ufafanuzi lakini katatoa hamasa na mwanga kwa wachambuzi wengine walio halisi kuturudisha kwenye msitari ili kutunusuru na wanamichezo uchwara ambao wanadhani hata kubadili historia ili waonekane wao ndio kila kitu kumbe ni pumba tu!
 
Back
Top Bottom