Hii ni Taifa Stars iliyoifunga Zambia kuingia African Cup (Tumemkumbuka Peter Tino, tumemsahau Thuwein Ally)

Idi Pazi alikuwa ni reserve golie, jana tu katoa tweet yake kwamba kilichofanyika siyo haki. TEna inaelekea wote walikuwepo kuwapa moyo hawa wachezaji lakini ameitwa Peter Tino peke yake.
tino na tenga ndio walialikwa!
 
Asante kwa historia nzuri lakini naona umejikita kumu undergrade Peter Tino. Wachezaji wote walioshiriki kutuvusha mwaka 1979 wanastahili pongezi kubwa sana lakini kibinadamu yule aliyefunga goli lililotuvusha anakuwa na historia ya pekee bila kujali mengine yote uliyosema.

Nafikiri kwasasa hatupo kwenye mjadala wa mchezaji gani alikuwa mkali enzi hizo ila kupitia kufuzu Afcon safari hii imetufanya leo tuone thamani ya goli lile la Peter Tino.

Hii ni kawaida kibinadamu ndio maana hata Iniesta pamoja na kuwa fundi wa hatari lakini lile goli lake la world cup final itabakia kuwa alama yake kwa wahispania daima.

Nafikiri kwa namna ya kujenga tungeshauri wale wachezaji waliotuvusha mwaka 1979 au familia zao wafanyiwe kitu cha kumbukumbu. Yes, tunashukuru kwa zawadi ya Tino leo ikulu lakini hili litazamwe kwa mapana.

Peter Tino alikuwa mchezaji bora ndio maana akaitwa timu ya Taifa na kuwakilisha nchi, zuri zaidi ndiye aliyefunga lile goli la dhahabu na kutuvusha. Hilo linatosha wala hutufanyi zoezi la comparison la mkali nani.

Sent using Jamii Forums mobile app
. (Nukta)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...
imenikumbusha hizo enzi Gidamis Shahanga akipewa zawadi ya national bendi 3 mono kaseti baada ya kuleta gold ya marathon jumuia ya madola.
...
 
...
imenikumbusha hizo enzi Gidamis Shahanga akipewa zawadi ya national bendi 3 mono kaseti baada ya kuleta gold ya marathon jumuia ya madola.
...

kaka umekumbusha mbali, Shahanga alikuwa noma kuliko Filbert Bahi, hawajui wengi hilo.
 
Nimekubali masahishisho haya.
Nimekubali masahishisho haya.

Thuweini Ally aliingia Simba 1979, ikiundwa na vijana wengi wakiwa shule:Umiseta, baada ya wakongwe wengi kuondoka, akabaki Marehemu Omari Mahadhi; Daudi Salum; na Marehemu Kajole. Coach akiwa ...Willy Mwaijibe. I think alitokea Kikwajuni. Alikuwa akifunga kila mechi.

Simba ya vijana wale akina Filbert Rubibira, Hussein Tindwa (Alifia uwanjani mechi ya Racca Rovers), Abbas Kuka, George (Best) Kulagwa, Nicodemus Njohole, Thuweini Ally, Rahim Lumelezi na Martin Kikwa ndiyo ilifungwa 4-0 na kurudisha 5-0 Zambia. Nafikiri kwenye 5-0, Thuweini alifunga goli/magoli.

Peter Tino akiwa amemaliza form 4 na akiwa star wa umiseta na kina Njohole, Peter Muhina e.t.c ndiyo alienda Taifa Stars.

Kwa kuwa Yanga ilikuwa na hali ngumu baada ya mastaa wake kuunda Pan, Simba na Pan ndiyo walikuwa mahasimu wapya, ingawa sikumbuki kama Pan iliwahi kuifunga Simba.
Akina Adolph;Mkwenche;Gordian;Pondamali na wengineo wa Pan: Yanga Kids na B ya zamani ndiyo walikuwa mahasimu wapya wakipambana na akina Nico, George Kulagwa waliokuwa awali Simba B na wengine wageni.

Kwa record: Wakati Tanzania inashiriki fainali ya 1980, Leodgard Tenga alikuwa ameisha maliza Chuo: 1978, unless kwa sababu zingine. Aliacha mpira baada ya fainali, zaidi kwa sababu za kitaaluma/kikazi baada ya kuhitimu chuo.

Peter Tino, anaenziwa kwa ajili ya impact ya goli lake. Wangebadilishana na Adolph, yeye akafunga Dar, Adolph Zambia, Adolph ndiyo angeenziwa. Dynamics za mashindano, uwezo wa kuleta mabadiliko wakati ambao ungeweza kukata tamaa au kuharibu kwa kukosa uangalifu hatimaye kutoka na matokeo ya mwisho, ndipo kwenye heshima, ingawa kiujumla wote wanastahili pongezi.

Tuulizane, mechi ya juzi TZ-UGANDA, aenziwe nani? mmoja tu!
 
Yanga ilivunjika mwaka 1976 na ndipo Pan ikaundwa na wale wachezaji wote wa Yanga. Ni kweli ungetegemea Pan iwe mahasimu wapya lakini haikuwa hivyo. Tena kama unakumbuka walihasamiana wao wenyewe Yanga akijiita Yanga Kandambili na Pan akijiita Yanga Raizon. Pan imeshakufa lakini Yanga iko hadi leo na wasioujua ndiy kisa cha cartoon za Yanga wakati mwingine kuonekana kama ndala yaani Kandambili.

Kuhusu ushindani ni kwamba kwa miaka mitano yaani kuanzia 1976 hadi 1980, siyo Yanga wala Pan ambao walitoa ushindani kwa Simba ambaye alichukua ubingwa kwa miaka yote hiyo. Wote Yanga na Pana hakuna aliyewahi kuifunga simba kwa miaka yote mitano.

Pan alikuwa akijitahidi anakuwa wa pili na kama unakumbuka wale wanigeria waliotufunga kwenye timu ya Taifa March 1980 walikuja kivingine kwa timu iitwayo Enugu Rangers (kama sijasahau)kwenye kombe la Washindi ambapo Juma Pondamali wa Pan alileta mbwembwe zake golini akina Tunde Obamidele na Segun wakamtundika goli 2-0 na Pan ikatolewa raundi ya pili tu.


Kwa kuwa Yanga ilikuwa na hali ngumu baada ya mastaa wake kuunda Pan, Simba na Pan ndiyo walikuwa mahasimu wapya, ingawa sikumbuki kama Pan iliwahi kuifunga Simba.
 
Ulivyoandika inaonesha haupo neutral. Usisahau hiyo unayoiita Pan Africa ilikuwa ni Yanga tu. Kwa mheshimiwa (ingawa ni Simba) alichofanya ilikuwa ni sahihi kumtambua aliyefunga bao la kutuwezesha kwenda African Cup> Ushabiki mwingine ulipouonesha ni pale ulipozungumzia Golden Boy ila hukuzungumzia kiboko yake Chama alivyokuwa anamdhibiti mpaka Jongo akaanzisha msemo wa man to man.
Hebu msikilize Jongo alipokuwa anatangaza kuhusu hiyo mechi kuanzia 4:50: ..... tunakwenda lagos.....


Ndiyo raha ya JF. Habari huzaa habari nyingine!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi sijafurahia zawadi kwa TINO peke yake... hii haileti muunganiko kwenye timu.
Kama hawa akina NYONI, MSUVA n.k wamepewa wote, kwa nini hao wa 1980 APEWE MMOJA TU?
Serikali itafakari tena huu ni UNYANYEMBE kabisa.
 
Hata mimi sijafurahia zawadi kwa TINO peke yake... hii haileti muunganiko kwenye timu.
Kama hawa akina NYONI, MSUVA n.k wamepewa wote, kwa nini hao wa 1980 APEWE MMOJA TU?
Serikali itafakari tena huu ni UNYANYEMBE kabisa.
Utakuta Jiwe, pamoja na kuwa alishakuwa mtu mzima mwaka huo, lakini hajui lolote kuhusu kilichotokea mwaka huo. Hata huyo Tino inawezekana anasimuliwa tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utakuta Jiwe, pamoja na kuwa alishakuwa mtu mzima mwaka huo, lakini hajui lolote kuhusu kilichotokea mwaka huo. Hata huyo Tino inawezekana anasimuliwa tu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Alikuwa wakati huo November 1979 anafanya mtihani wa Form Four na wakati tunacheza kule Nigeria alikuwa anasubiria majibu ya mtihani kijijini.

Tena wakati huo magari kwenda Bukoba yalikuwa hayapiti huko yalikuwa yanapita Biharamuro.
 
suala hili linatufunza kitu kikubwa sana,bila kujali nani alifanya nini na kwa wakati gani,tunajifunza umuhimu wa team work na jinsi team players wanavyoshirikuana kuleta mafanikio ya malengo yao.Tunachoshindwa ni namna ya kutoa motisha kwa team players wetu,ili kuwapa hamasa kubwa zaidi,motisha haitolewi kwa mtu mmoja au wawili miongoni mwa team players

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa, kizazi cha sasa wanahitaji taarifa za Watu kama hawa.

Nakumbuka tukio moja aliumia akafungwa bandeji kichwani akarudi uwanjani akiwa na bandeji yake kichwani.
Kulikuwa na battle ya kipekee kati ya Chama na Mogella. Hakuwa na umbo kubwa ila akilitazama goli basi ni balaa.
 
Kwenye hiyo picha ya Taifa Stars, Kutoka kushoto ni:

Godian Mapango (Pan), Salim Amir (Balimi-Bukoba), Idi Pazi (African Sports), George Kulagwa (Simba), Thuwein Ally (Simba), Ibrahim Kiswabi (Pan), Peter Tino (African Sports), Omar Hussein (Yanga), Juma Mkambi (Yanga), Hussein Ngulungu (Pan), Juma Matokeo (Pan), Mohamed Salim (Coastal), Adolf Rishard (Pan).

Uwanja wa Ndege ni Dar Esalaam International Airport, Terminal 1
Sahihisho mkuu..iddi pazi 'faza' hajawahi kucheza African sports alikuwa nyota ya mtwara kipindi hicho!
 
Back
Top Bottom