kofuli
JF-Expert Member
- Feb 9, 2019
- 505
- 568
Sijawahi kucheka kwa kiwango kama nilicho cheka leo kiasi kwamba watu wamehisi pengine nimechanganyikiwa ghafla ndani ya daladalaNliacha kabisa kucheza draft.kipindi cha nyuma uncle wangu mmoja alinifundisha draft nikawa vizuri sana.kiukweli niliweza kuwagonga gonga baadhi ya watu kiroho mbaya.
Maeneo flani Kino clan kulikuwa na bench nje ya nyumbani kwa jamaa yangu.siku hiyo nikaona nami ni socialize na wananzengo.walikuwepo wazee na vijana na kakijana kamoja kana ulumbi wa maneno.
Baada ya kumfunga mtu super kakaanza maneno ya shombo "mi sijaona mtu hapa...naona tu mnapuyanga puyanga hakuna anayejua draft"
Wale wengine wakawa wanajiuma uma.nikaomba nikae kwenye bench...kajamaa kakacheka sana...mpaka machozi yakakatoka.tena kwa kebehi.
"Daaah yaani wewe poyoyo ndo unataka kuja kupakaza makamasi na udenda kwenye kete?" Nlikwazika maana kajamaa kenyewe ni namba moja hasa.
Tukaanza, kakanambia nichague kuanza kusukuma kete au kaanze kenyewe.nikasukuma...kakatikisa kichwa kwa huzuni.
"Kweli akili si mwili, unacheza kibwege sana kama ndondocha...we unajua draft kweli?au unasukuma tu kete kama ulivyokuwa unamwona huyo mzee aliyetoka?"
Kalinikwaza sana kajamaa ila nikanyamaza.nikataka sukuma kete flani kakanishika mkono.
" Hiyo usisukume...ntakupiga super" nikakaambia "please dont touch me huku nmekunja sura..."
"Aaah wakusoma usiwe mkali...simba mkali na anazaa utakuwa wewe" hapo kweli kalinila kete mbili.huku kanacheka kwa kebehi.
Nikataka sukuma nyingine kakanambia..."big usisukume hiyo ntakupiga super ujue" nikasukuma.kakanila tatu... Hapo hasira zinakipanda kiasi.maana nikawa sielewi inakuaje nacheza kama boya.
Tumecheza kidogo nikataka sukuma nyingine....kakatikisa kichwa..."kweli nmeamini ukubwa wa mwili si wingi wa akili...yaani nyie wote ndo mmeniletea huyu ndondocha ananuka maziwa aje kucheza na mwanaume?kwa nini mnanikosea heshima?oneni anavyo bong'oa kwa furaha kabisa nifanye yangu"
Hapo sikuvumilia nilimgonga kichwa akaanguka chini akawa kama amezima hivi.jamaa wakaniwahi....nlikuwa natetemeka kwa hasira na ghadhabu.wazee wakanishika na kunisihi niwe mvumilivu. kama dk moja kajamaa kakawa kanakohoa wakakamsha na kukakalisha kwenye kiti...kametoa macho kama ngumi.
"Amenigonga na nini?" Wakaanza kucheka kwa lile swali...mzee mmoja akajibu " ndoo hiyo fala wewe unadhani wote wnapenda maneno ya shombo...tunakwambia kila siku acha shombo huelewi"
Kajamaa kakatikisa kichwa ili ubongo urudi sehemu yake nadhani ulishake kidogo.halafu kakasikilizia kakaona bado ubongo haujakaa sawa.kakatikisa na kugonga gonga pembeni ya kichwa.halafu kakanicheck na kukenua meno.
" Huu mchezo hautaki hasira...unataka akili" hapo jamaa waliniwahi kunikamata...na kuniondoa maana waliniona kabisa naanza kuchemka...
mpaka leo nahisi kale kajamaa kalikuwa kachawi kangeweza nitafutia kesi ya kijinga tu.
Sikuwahi cheza tena draft hadharani. Nmepita sehemu nmekuta watu wanacheza nikasimama tu kutizama nmemkuta mzee ambaye anaweza kuwa baba yake yule jamaa....ana maneno machafu.nmesimama anauliza "na wewe unataka kufirwah?" Hawa wengine wote tayari hawana marinda nmewachana chana" niligeuka na kuondoka nisije pata murder case bure.
Sent using Jamii Forums mobile app