CCM wanajua kucheza Kete za Draft

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,905
CCM WANAJUA KUCHEZA NA KETE ZA DRAFT

Na, Robert Heriel

Siasa ni kama mchezo wa Draft, mchezo unaohitaji akili zaidi kuliko jambo jingine, Mchezo wa Daft unahitaji mtu mwenye hesabu za mbele na haraka mno, Mchezo wa Draft unahitaji mtu anayejua na kuiona mitego ya adui, Mchezo wa Draft unahitaji mtu anayejua kutega mitego. Kanuni moja ya kifo kwenye mchezo wa Draft inasema, Kula ni lazima, kanuni hii ni muhimu sana hata kwenye siasa. Yaani ukipewa kete lazima ule,

Mimi kama Taikon moja ya michezo ninayoimudu zaidi ni pamoja na mchezo wa Draft, kwenye mchezo wa Draft nitakupa kanuni chache ambazo nafikiri kama unaakili nzuri utaweza kuzitumia kwenye mizunguko yako ya kila siku, lakini hapa nitawalenga zaidi wanasiasa.

Kanuni kuu za mchezo wa Draft ili ushinde
1. Ona hatua tatu za kete utakayosogeza
2. Tega mitego kabla hujategwa
3. Mpunje adui yako kete. Hakikisha unakuwa na kete nyingi kuliko adui yako. Kumbuka wote mkianza mnakuwa na kete zinazolingana. Sasa hakikisha unakula kete na kumzidi adui yako kete zaidi ya mbili.
4. Jua force- King. Hakikisha unajua kulazimisha kuiingiza kete yako kingi kwa lazima. Kama adui yako atakuwa naye ni mtamu basi lazimisha force-king
5. Jua kutoa suluhu, ikiwa utakuwa umezidiwa.

Kanuni hizo tano ndizo sisi mabingwa wa Mchezo wa Draft tunazitumia kuwaburuza vibonde wetu.

Technique muhimu za maneno mengi huwa pia ni moja ya kanuni lakini sio kanuni kuu kwani kwenye mashindano makubwa mtu unaweza kubanwa kuwa usiongee, mcheze kimya kimya, hivyo kama unategemea maneno zaidi unaweza kujikuta unapigwa.

CCM na Upinzani nawaona kwenye Mchezo wa Draft. Moja upande huu mwingine upande huu. Kila mmoja anasukuma kete zake kuhakikisha anamshinda mwenzake.

Taikon Nafurahia nikiona mchezo huu wa siasa hasa ukiwa na uhuru na amani. Binafsi sina Chama, na sina mpango wa kuwa na Chama. Licha ya watu kunisingizia kuwa mimi ni CCM pale ninapoukosoa upinzani, na wengine kuniita Mpinzani pale ninapokosoa CCM. Jambo muhimu kusema ni kuwa, kila mtu anayohaki kufikiri vile akili yake ionavyo, hivyo wako sahihi.

Kwa muono wangu mpaka sasa katika mchezo huu wa Draft katika siasa, nawaona wana-CCM wakisukuma kete zao vizuri sana. Wanajua hatua tatu kwa kila kete wanayoisukuma.

CCM imezingatia kanuni tano kuu katika kushinda mchezo wa Draft, hii inawaweka katika nafasi ya ushindi kama wataendelea kuzisukuma kete zao vizuri.

Wapinzani wanatumia kanuni moja tuu kwenye mchezo wa Draft ambayo ni maneno matupu, maneno ya shombo, maneno ya kejeli na dhihaka, ni kweli kabisa mbinu hiyo inaruhusiwa kwenye mchezo wa Draft lakini haima nguvu sana katika kutoa ushindi. Kwa sisi wachezaji mahiri wa Draft tunajua kuwa mbinu ya maneno ya shombo kwenye Draft hutumiwa zaidi kwa lengo la kumchanganya adui, kumpagawisha, kumtoa kweye shabaha, kumkosesha kujiamini. Mbinu hii inasaidia kwa adui asiye na uzoefu katika kucheza Draft, lakini haina nguvu ikiwa adui anauzoefu wa kucheza Draft. Utapiga kelele na kufungwa utafungwa. Tena ukizubaa utafungwa Super.

Kwenye siasa kete ni wananchi, kumbuka wananchi wamegawanyika. Ikiwa Chama kitajua mgawanyiko wa wananchi ni wazi kitakuwa kinauwezo wa kuwatumia kila mmoja kwa kazi yake.

CCM wanajua Role za kila mwananchi, wanajua kuwa kuna
1. wananchi fuata upepo hawa ndio wengi na ndio muhimu kwani kura nyingi zipo kwao,

2. Kuna wananchi wenye elimu, watumishi na wafanyakazi wa umma, hawa sio wengii, hawa wanajielewa hivyo CCM haiwategemei sana, alafu kuna kundi la mwisho.

3. Kuna watu mashuhuri, maarufu, na matajiri. Hawa sio wengi lakini wakitumiwa wanaweza kuteka akili za wananchi fuata upepo.

4. Kuna vyombo vya dola. Hawa hutumika kwenye force King, yaani upende usipende kete lazima kete iliyokusudiwa lazima iingie kingi

Hiyo ni safu kwenye Draft la Siasa.

Jana CCM walitumia safu namba tatu, hizo kete zilizosukumwa na CCM lengo lake ni kuchota akili za wananchi fuata upepo ambao kimsingi ndio wengi. Hawa huona yanayoonwa na yale wanayoambiwa wayaone.

Hawa hata usimame uwaambie kuwa Tanzania ndio taifa kubwa dunia ifikapo mwaka kesho wataamini, na watashangilia. Ukiwaambia Tanzania ndio inauchumi mkubwa Afrika kwa sasa, wataamini na kushangilia, hakikisha unatoa na mifano miwili mitatu inayoonekana mbele ya macho yao. Nakuhakikishia wataamini.

Ukiichukua kete kama Diamond ukamwambia aseme, Watanzania kwa sasa wanaongoza Afrika kwa kuwa na pesa, wananchi hao watashangilia na kukubali. Sababu kubwa ni kuwa wananchi hao ni bendera na watu mashuhuri ndio upepo, hivyo wananchi hao huufuata upepo. Hawatumii akili kufikiri, wao wanatumia macho pekeake kufikiri.

CCM ninachoisifu inatambua jambo hilo, kingine naisifu kwa sababu inatoa pesa kwa kundi la watu mashuhuri wakijua hiyo ni kete yao muhimu. Wanajua wapo wafuasi wa Diamond, Ali Kiba, Harmonize, N. Wafuasi hao ni bendera na wasanii ni upepo.

Upinzani wameshindwa kutambua nafasi ya kete ya watu mashuhuri katika sanaa. Upinzani mngepaswa mtenge pesa nono kisha tafuteni vijana mashuhuri wa fani zote, wapeni pesa kisha Draft lichezwe. Upinzani wanapenda kufanyiwa kazi bure, Kwa mfano mtu Kama Roma Mkatoliki, Ney wa Mitego, na wengineo mlipaswa muwe mmeshawapa pesa ya kutosha ili siku mapambano yakianza nanyi mnaweza kurudisha mashambulizi.

Ukweli ni kuwa hakuna atakayewafanyia kazi bure. Msiwalaumu wasanii wanaoipigia chapuo CCM, ni kwa sababu mkono mtupu haulambwi. Hata kama hawapewi pesa nyingi lakini wanajiona wapo salama.

Tunafahamu wasanii wengi elimu zao ni sifuri, hawajasoma, hawana wanalolitegemea zaidi ya sanaa. Sasa wasipojipendekeza kwa CCM na hawana elimu yoyote huoni watakuwa kwenye wakati mgumu. Angalau wangekuwa wasomi, kuwa hata sanaa ikibuma wanaweza endelea na taaluma zao. Hata ningekuwa ni mimi.

Kesho kutwa nafikiri kutakuwa na tamasha lingine la kumpongeza Magufuli, nafikiri ni Dodoma. Huko CCM imewaandaa tena watu mashuhuri ili kusomba kura za wananchi fuata upepo.

Naipongeza CCM kwa namna wanavyoweza kusukuma kete zao.

Nawashauri wapinzani, wasijikite zaidi kwenye kanuni ya kupiga mdomo, wawekeza pia kwenye kanuni zingine.

Pia watoe pesa kwa vijana, mbona kuna maelfu ya vijana wasomi, wenye ujuzi, wasanii, wanamichezo, wanaharakati, viongozi wa dini, wafanyabiashara, wamiliki wa media.
Wapeni pesa hao watu, acheni kudhani mambo yanaenda kwa urahisi.

Watu wanajua kuwa hata siku upinzani ukichukua nchi hautaweza kutoa pesa kwa kila mtu, mtu akifikiri hivyo tuu anaona hamna umuhimu wa kukufanyia kazi bure. Toeni pesa vijana wapate kuwapigia chapuo.


Sukuma kete, acha porojo, mchezo wa Draft hauhitaji hasira.

Taikon na Raia wengine tunafuatilia mchezo huu kwa karibu.

Kumbuka; Kwenye Draft kula na kuliwa ni kawaida. Kuolewa na kuoa ni kawaida. Tunasubiri mwaka huu nani ataolewa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Watu wanapenda kazi za hao wasanii ndomana wanapenda kuwa karibu nao ukitaka kujua Kama wanaungwa mkono ktk siasa wanazofuata wasanii, jiulize wasanii wangapi walipita Kura zamaoni CCM? Na walipata kura ngapi ngapi ktk hizo chaguzi? Wapo watu wapo upinzani wanampenda daimond wapo watu wapo timu ya Simba ukija kwenye siasa hawapo pamoja Kuna watu wapo yanga kwenye siasa hawapo pamoja, hizi mbinu zakuaminisha watu ndozile zilizofanya watu wakaaminishwa upinzani umekufa leo tunachokiona nitofauti Sana, wasanii wapo kibiashara zaidi hivyo hivyo kwawacheza mpira,unaweza muona mchezaji anacheza Simba lakini niyanga damu Ukiyaelewa haya huwezi shangaa ya Uhuru,,
 
Mimi sijaelewa,Ila kitu kimoja ninachojua ni kwamba serikali ni Mali halali ya watanzania bila kujari itikadi zao,kwenye uchaguzi Kama huu tunaoenda kufanya October chama kinaenda kuomba ridhaa kwa wenye serikali ili kiongoze serikali yao.Sasa kitendo Cha chama fulani kupora na kutumia Mali or organs za serikali kwa faida yake au kuhadaa wananchi any how ni uhalifu Kama uhalifu mwingine,ndo maana natamani movement ya kuiondoa ccm Tanzania kwa nguvu itokee nami nijiunge
 
Mtazamaji usingeandika yote haya, kete yako inaweza isiwe kwenye siasa moja kwa moja ila kuna sehem inatafutwa kingi

Mkuu maisha yangu hayategemei siasa, napenda kuandika, nimeanza kuandika huu ni mwaka wa nane, hata kabla awamu hii haijaingia madarakani.

Siandiki ili nitegemee hisani yoyote
 
Hahaha..yaani hauja ona weakness zote zilitokea hapo nyuma wakati ccm ikfanya siasa pekeeee.?Na ukweli ni kwamba walitumia nguvu kubwa na Zambi pamoja na dhuluma za mali na uhai wa watu.Leo yale yote yakisemwa ni kijeli na matusi na dhihaka kwa ccm. wapinzani wana vingi vya kusema maana vyote ambavyo havikusemwa leo vinasemwaa ni bora wengeruhusu waseme mwanzo.
ccm wabebaki na madaraja, Strigrers, na barabara za juu.tu.
 
Back
Top Bottom