Hii ni shida wanayoipata Wanawake matajiri

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,784
Achana na hawa wadada ana ka IST na duka la nguo Kinondoni anajiona tajiri. Tajiri anaishi nyumba ya kupanga chumba na sebule na jiko, anajiona kayapatiiiiiiia.

Ninaongelea wale wenye mega projects, mega investments. Kwa kweli wanaishi maisha ya upweke sana.

Jana nilialikwa na rafiki yangu kwa ajili ya mlo wa usiku. Yeye ni mfanyabiashara mkubwa, ana viwanda vyake vya vipodozi na anauza sehemu mbalimbali duniani.

Alinunua nyumba Oysterbay iliyokuwa ya mheshimiwa mmoja mstaafu (zile nyumba waliuziwa kwa bei chee na Mkapa) akaivunja yote na akajenga nyumba za ndoto yake.

Anacholalamika ni kwamba wanaume wanamuogopa kwa ajili ya pesa zake. Hata akomtongoza mwanaume baada ya muda kidogo mwanaume atapotea.

Akaenda mbali zaidi, akasema wanawake wengi matajiri wamejikuta wakiingia kwenye mapenzi ya jinsia moja lesbianism kwa kukosa watu wa kuwa nao.

Tuliongea mengi sana kwa kweli. Wito wangu kwenu vijana, msiogope ma Range Rover yao, watongozeni tu, nao pia ni watu na wanahitaji wenzi wa kuwa nao maishani.
 
Hata akomtongoza mwanaume baada ya muda kidogo mwanaume
Mzee baba ulipata wapi ujasiri wa kusikiliza misamiati na huyo tajiri single mom tena mkiwa kwa nyumba yake pasipo ikulu kukasirika?

Sidhani kama 'kazi na dawa' zimesahaulika kwako, kwa vyovyote ikiwa ukishindwa kukumbuka 'kazi na dawa' I think umeokoka bro.
 
Tatizo wanataka wawe kichwa cha familia kisa wanapesa ,mwanaume akishakuoa hata kama hana pesa ni masikini lazima awe kichwa cha familia , vinginevyo hawezi vumilia ujinga wa kuongozwa na mwanamke...never
Hapo ndio shida inapoanzia, unataka umlunje, yeye anawaza batch ya mzigo wa parachichi alizozituma China
 
Achana na hawa wadada ana ka IST na duka la nguo Kinondoni anajiona tajiri. Tajiri anaishi nyumba ya kupanga chumba na sebule na jiko, anajiona kayapatiiiiiiia.

Ninaongelea wale wenye mega projects, mega investments. Kwa kweli wanaishi maisha ya upweke sana.

Jana nilialikwa na rafiki yangu kwa ajili ya mlo wa usiku. Yeye ni mfanyabiashara mkubwa, ana viwanda vyake vya vipodozi na anauza sehemu mbalimbali duniani.

Alinunua nyumba Oysterbay iliyokuwa ya mheshimiwa mmoja mstaafu (zile nyumba waliuziwa kwa bei chee na Mkapa) akaivunja yote na akajenga nyumba za ndoto yake.

Anacholalamika ni kwamba wanaume wanamuogopa kwa ajili ya pesa zake. Hata akomtongoza mwanaume baada ya muda kidogo mwanaume atapotea.

Akaenda mbali zaidi, akasema wanawake wengi matajiri wamejikuta wakiingia kwenye mapenzi ya jinsia moja lesbianism kwa kukosa watu wa kuwa nao.

Tuliongea mengi sana kwa kweli. Wito wangu kwenu vijana, msiogope ma Range Rover yao, watongozeni tu, nao pia ni watu na wanahitaji wenzi wa kuwa nao maishani.
Kwahiyo baada ya maongezi mzee mwenzangu ukala tunda kimasihara au nawe uliogopa kama wazembe wengine??
 
Tatizo linaletwa na ubinafsi wao. Mwanaume akipata pesa jambo la kwanza anafikiria kuongeza mke, hii inamaanisha sisi ni wakarimu. Mwanamke akipata uwezo tu, jambo la kwanza analowaza ni kuwa haitaji mwanaume kusahau kuwa na sisi tuna umuhimu wetu hata kama ikiwa hatuna pesa.

Apambane na genye zake.
 
Mzee baba ulipata wapi ujasiri wa kusikiliza misamiati na huyo tajiri single mom tena mkiwa kwa nyumba yake pasipo ikulu kukasirika?

Sidhani kama 'kazi na dawa' zimesahaulika kwako, kwa vyovyote ikiwa ukishindwa kukumbuka 'kazi na dawa' I think umeokoka bro.
Kambi ya Fisi, shemeji yako tupo naye hapa JF, mambo mengine hatufunguki, yanaishia hukohuko
 
Back
Top Bottom