Habarini ndugu watanzania wenzangu. Huu ni uzi wangu wa kwanza tokea niweke uzi wa mwisho hapa kwasababu niliacha kuandika kwa muda ili kupisha harakati na purukushani za uchaguzi kupita.
Nawasalimia nikiwa na huzuni kubwa sana moyoni kutokana na misiba mingi ya ndugu,jamaa, marafiki na majirani ambayo imetuzunguka na la kusikitisha ni kuwa misiba hii mingi tunaishiriki bila kuwa na maziko kwasababu tumetafuta miili ya wapendwa wetu katika mahospitali yote tulipoelekezwa bila kufanikiwa kuipata na hivyo basi tumeshiriki ibada na Dua bila miili kwa baadhi ya misiba hii.
Kwa kifupi bado nipo katika wiki ya kimaombolezo sipo sawa kabisa kiakili kwa sasa, akili yangu imejawa huzuni,butwaa, mshangao, ganzi, vitendawili visivyo na majibu, nimekuwa mtu wa kukaa pekee yangu mara nyingi nikijaribu kujiweka sawa kwasababu nikisikiliza watu wakisema maisha yamerudi mimi natafakari wale majirani zangu ambao wameuwawa na jinsi taarifa za misiba yao zilitufikia, natafakari kilichotokea kama kilikuwa na ulazima wowote kufanywa mbona wengi wa waliotutoka ni responsible citizens wa Dar es salaam na hawana hata shughuli zozote za kihalifu au siasa za visasi na pande zozote bali ni makabwela wa kufanya shughuli za kujikimu "hand to mouth life style"?
Ukiwa hauna hata chembe ya ubinadamu na utimamu wa kiakili utalinganisha uharibifu wa miundo mbinu ya mwendo kasi,majengo ya serikali na uhai wa mwanadamu. Hivi ni vitu viwili tofauti na havifanani kwa hadhi hata kidogo. Majengo na miundo mbinu tunaweza kuijenga upya na kurudisha mvuto wake uliopotea au tunaweza kutengeneza miundo mbinu ya kisasa zaidi kushinda ile ya kwanza. Ila nambie, ni wapi utanunua au kupata uwezo wa kurejesha hawa ndugu, jamaa, majirani na marafiki walio uwawa?
Natoa onyo kali kwa wale waoleta hoja za kipumbavu kujustify uwendawazimu uliotokea kuwa ni kwa mujibu wa sheria na watekelezaji walikuwa wanalinda usalama wa inchi, njoo nikuonyeshe familia ambazo hawajui mama zao na baba zao wapo wapi hadi sasa wametuachia mayatima na wajane wakiwa hawaamini kilichotokea.
Watoto wetu wamekuwa traumatized na mabomu na milio ya risasi iliyokuwa inapigwa mfululizo as if nyumba zetu zimejengwa kwenye viwanja vya shabaha za mazoezi ya kulenga risasi na mabomu. Watoto wetu na familia zilipaliwa na moshi mkali wa mabomu ya machozi. Nani anaweza kuruhusu ushenzi wa kiwango hiki kwa raia watulivu kama wa tanzania?
Nipo kwenye maombolezo kwasasa sijui nitamaliza lini ila itanichukua muda mrefu sana kukubaliana na ukweli kuwa mambo yalikuwa hivi na haikuwa ndoto.
MUNGU awalaani wote kuanzia aliyetoa wazo na aliyekuwa wa mwisho kutekeleza amri hii ya kishetani, laana kubwa inawajia juu yenu kwa muda mtakaokuwa hapa duniani na mfe midomo ikiwa imepinda kushoto na macho yakatae kufunga.
"......................satutariduk allaeanat aleazimat watutariduk limudat 400 eam qadimat hataa yatima tadmir bidhratik bialkamil ................................."