Hii ni kwa wana CCM tu

Nataka niwepe ushauri wanaccm wenzangu. Kuna mambo mengi sana ya kipuuzi ambayo yanaendelea kufanywa na serikali yetu kwa sasa. Mambo haya yatatufanya tukose kura mwaka 2015 hasa sehemu zile ambazo chama chetu kimeweka ngome.

Mfano hapa Dodoma, kuna ujenzi wa barabara ambao unaendelea, kweli mtoto wangu ana miaka minne na miezi mitatu. Leo tukiwa kwenye pikipiki tulipokuwa tunapita maeneo ya Chamwino kaniambia, "Baba nani kaharibu bara bara?"

Kuna ujenzi wa barabara wa kipuuzi unaoendelea katika manispaaa ya Dodoma. Kwa hakika kwa ujenzi huu hatuna la kuwaambia wananchi siku zijazo. Mfano katika kata ya Changʼombe kuna diwani wa chama chetu alifariki siku za hivi karibuni. Naamini uchaguzi utakapoitishwa hatuna la kuwaambia wananchi.

Hivi ndiyo kusema tumeshindwa kabisa kuisimamia serikali? Hivi hata viongozi wa chama mnapopita na kuona ugoigoi huu unaendelea mnawaambia nini hawa wakurugenzi wa mkoa, wilaya na watendaji wa kata? Hivi kweli watendaji wa serikali wanawajibika kwenu? Au ndo mnakula nao? Hakika kwa utaratibu huu tutapoteza kila kitu kwani hatuna jema tena.

Hebu tuamke jamani, Angalieni jinsi fedha ya wananchi inavyohujumiwa. Mfano barabara ya kwenda st Gema, ule ni upuuzi umefanyika pale. Kifusi kimemwagwa halafu greda likasawazisha bila kushindia. Huu ni ugoigoi. Hebu tuamke bwana.

Nahamu kubwa sana hapo kwenye RED Malaria Sugu aone!
 
Ww huwezi kuwa mwana ccm hata siku moja , waonekana kama vile unawatumikia ma bwana 2

Kweli kabisa maana asili ya mwana ccm lazima awe anakubaliana na kila jambo hata la kipuuzi linalofanywa na serikali yake. Umenena sawa kabisa...Pongezi mkuu:poa:poa
 
Mlangaja hii ipo kikampeni zaidi muulize jamaa yangu mmoja yupo hapo Dom anaitwa Robert Mwinje ushauri huu unamfaa zaidi kwani aliatempt kugombea ubunge hapo mjini akakuta kuna wana ccm wenzake 40 akachomoa jina lake. CCM kwishney kaka wewe unaongelea barabara wakati kuna maelefu ya Wa TZ wanakufa dakika hii ninapopost hii thread kwa kukosa matibabu sababu mgomo wa madaktari.
Nataka niwepe ushauri wanaccm wenzangu. Kuna mambo mengi sana ya kipuuzi ambayo yanaendelea kufanywa na serikali yetu kwa sasa. Mambo haya yatatufanya tukose kura mwaka 2015 hasa sehemu zile ambazo chama chetu kimeweka ngome.

Mfano hapa Dodoma, kuna ujenzi wa barabara ambao unaendelea, kweli mtoto wangu ana miaka minne na miezi mitatu. Leo tukiwa kwenye pikipiki tulipokuwa tunapita maeneo ya Chamwino kaniambia, "Baba nani kaharibu bara bara?"

Kuna ujenzi wa barabara wa kipuuzi unaoendelea katika manispaaa ya Dodoma. Kwa hakika kwa ujenzi huu hatuna la kuwaambia wananchi siku zijazo. Mfano katika kata ya Changʼombe kuna diwani wa chama chetu alifariki siku za hivi karibuni. Naamini uchaguzi utakapoitishwa hatuna la kuwaambia wananchi.

Hivi ndiyo kusema tumeshindwa kabisa kuisimamia serikali? Hivi hata viongozi wa chama mnapopita na kuona ugoigoi huu unaendelea mnawaambia nini hawa wakurugenzi wa mkoa, wilaya na watendaji wa kata? Hivi kweli watendaji wa serikali wanawajibika kwenu? Au ndo mnakula nao? Hakika kwa utaratibu huu tutapoteza kila kitu kwani hatuna jema tena.

Hebu tuamke jamani, Angalieni jinsi fedha ya wananchi inavyohujumiwa. Mfano barabara ya kwenda st Gema, ule ni upuuzi umefanyika pale. Kifusi kimemwagwa halafu greda likasawazisha bila kushindia. Huu ni ugoigoi. Hebu tuamke bwana.
 
Nataka niwepe ushauri wanaccm wenzangu. Kuna mambo mengi sana ya kipuuzi ambayo yanaendelea kufanywa na serikali yetu kwa sasa. Mambo haya yatatufanya tukose kura mwaka 2015 hasa sehemu zile ambazo chama chetu kimeweka ngome.

Mfano hapa Dodoma, kuna ujenzi wa barabara ambao unaendelea, kweli mtoto wangu ana miaka minne na miezi mitatu. Leo tukiwa kwenye pikipiki tulipokuwa tunapita maeneo ya Chamwino kaniambia, "Baba nani kaharibu bara bara?"

Kuna ujenzi wa barabara wa kipuuzi unaoendelea katika manispaaa ya Dodoma. Kwa hakika kwa ujenzi huu hatuna la kuwaambia wananchi siku zijazo. Mfano katika kata ya Changʼombe kuna diwani wa chama chetu alifariki siku za hivi karibuni. Naamini uchaguzi utakapoitishwa hatuna la kuwaambia wananchi.

Hivi ndiyo kusema tumeshindwa kabisa kuisimamia serikali? Hivi hata viongozi wa chama mnapopita na kuona ugoigoi huu unaendelea mnawaambia nini hawa wakurugenzi wa mkoa, wilaya na watendaji wa kata? Hivi kweli watendaji wa serikali wanawajibika kwenu? Au ndo mnakula nao? Hakika kwa utaratibu huu tutapoteza kila kitu kwani hatuna jema tena.

Hebu tuamke jamani, Angalieni jinsi fedha ya wananchi inavyohujumiwa. Mfano barabara ya kwenda st Gema, ule ni upuuzi umefanyika pale. Kifusi kimemwagwa halafu greda likasawazisha bila kushindia. Huu ni ugoigoi. Hebu tuamke bwana.

Na bado nataka mshindwe kabisa kama mnavyoendelea kushindwa mambo mengi kwa sababu mliwekwa na tume ya uchaguzi siyo watanzania namini Mungu atatulipa CDM kwa hujuma mliyo tufanyia
 
Back
Top Bottom