Hii ni kwa wana CCM tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni kwa wana CCM tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlangaja, Oct 5, 2011.

 1. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nataka niwepe ushauri wanaccm wenzangu. Kuna mambo mengi sana ya kipuuzi ambayo yanaendelea kufanywa na serikali yetu kwa sasa. Mambo haya yatatufanya tukose kura mwaka 2015 hasa sehemu zile ambazo chama chetu kimeweka ngome.

  Mfano hapa Dodoma, kuna ujenzi wa barabara ambao unaendelea, kweli mtoto wangu ana miaka minne na miezi mitatu. Leo tukiwa kwenye pikipiki tulipokuwa tunapita maeneo ya Chamwino kaniambia, "Baba nani kaharibu bara bara?"

  Kuna ujenzi wa barabara wa kipuuzi unaoendelea katika manispaaa ya Dodoma. Kwa hakika kwa ujenzi huu hatuna la kuwaambia wananchi siku zijazo. Mfano katika kata ya Changʼombe kuna diwani wa chama chetu alifariki siku za hivi karibuni. Naamini uchaguzi utakapoitishwa hatuna la kuwaambia wananchi.

  Hivi ndiyo kusema tumeshindwa kabisa kuisimamia serikali? Hivi hata viongozi wa chama mnapopita na kuona ugoigoi huu unaendelea mnawaambia nini hawa wakurugenzi wa mkoa, wilaya na watendaji wa kata? Hivi kweli watendaji wa serikali wanawajibika kwenu? Au ndo mnakula nao? Hakika kwa utaratibu huu tutapoteza kila kitu kwani hatuna jema tena.

  Hebu tuamke jamani, Angalieni jinsi fedha ya wananchi inavyohujumiwa. Mfano barabara ya kwenda st Gema, ule ni upuuzi umefanyika pale. Kifusi kimemwagwa halafu greda likasawazisha bila kushindia. Huu ni ugoigoi. Hebu tuamke bwana.
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ww huwezi kuwa mwana ccm hata siku moja , waonekana kama vile unawatumikia ma bwana 2
   
 3. F

  FUSO JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  kijana unasema serikali yetu ni ya kipuuzi siyo!!! yaani imefikia hatua uansema haya wazi wazi bila kufanya utafiti?

  Kama sisi ni wapuuzi kwa nini tumeshinda igunga tena kwa kishindo? kijana kama umekosa cha kuandika logout nenda nyumbani ukapumzike - kwanza wewe si mwana CCM hai kama unavyodai - nakuonya tena usirudie kuandika habari hizi za uchochezi na kuvuruga amani ya nchi. Utulivu tulionao inatakiwa tuudumishe hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kusherehekia miaka 50 ya uhuru wetu.

  Mungu ibariki Tanzania - wananchi oyeeee!!!!! -- Uhuru oyeeeeee!!!!!! -
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hakika wewe ndio mwana-CCM kweli......

  maana nilikuwa nashangaa huyu jamaa mwana CCM gani ambae hajui kuwa chama chake sasa ni sikio la kufa halisikii dawa yoyote....

  Careless whispers................
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Aha ha ha ha ha ha Jamaa unajifanya kama intelejensia vile biti kubwa kumbe hakuna kitu...jamaa kawapa ukweli manaleta hoja uharo hapa...
   
 6. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,967
  Trophy Points: 280
  wana ccm hawapo bado wanasherehekea ushindi wa (kishindo?) igunga. Kuhusu wakati wa uchaguzi usijali watu watagawiwa fedha, chakula, na tshirt mtapata tu watanzania hicho ndicho wanachohitaji.
   
 7. Tyta

  Tyta JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 12,846
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa...mwanaCCM huwa hakosoi, ni kusifia tu hata kama ni upupu
   
 8. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mhhhhhhhhhhhhhh
  ccm hoyeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 9. Tyta

  Tyta JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 12,846
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  hahahh..umeonae...biti la jamaa ni kama anamfaham mpaka chumba anacholala...eti anavuruga amani ya nchi
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Akitoa ushauri basi anapoteza uhalali wa kuwa mwana CCM?????????? Mbona Prof Bana hujamtoa UCCM alivyo toa tathimini ya kuisha kwa CCM????????Brain Zero mwizi mkubwa wa maghamba!!!!!!!!!
   
 11. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Usiogope ndugu yangu lazima tushinde.Usijali sana mambo ya mabarabara sijui mahospitali na maelimu hayo ni maneno ya wapinzani.
  Sisi CCM mambo yetu ni makofia,matisheti,maubwabwa na mangoma.
  We unaongelea sana mabarabara au we ni CHADEMA umetumwa?
  TUACHE NA RAHA ZETU SIE.
   
 12. N

  NIMEKIMBIA CCM Senior Member

  #12
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We cjui fox/mama wa ccm kapmwe akl kwanza ndo urud Jf sawaaah!chadema oyeee
   
 13. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Hiyo ccm yenu itawachachia tu si muda mrefu.
   
 14. S

  Salimia JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kijana epuka kutumia mimea korofi
   
 15. Tyta

  Tyta JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 12,846
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  username yko kiboko
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada umejionea mwenyewe majibu ya chama chako dhidi ya upuuzi wanaoufanya tena umetoa hadi mfano hai wa barabara husika lakini bado wamekukana, pole sana Mkuu.
   
 17. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Majibu yenu ya kibabe ndiyo sababu za kushuka kwa mvuto wa chama. Sitasema sana, ila kuna msemo usemao, "Chungu kipikacho mifupa, hupasuliwa na mifupa."
   
 18. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwa vile nafahamu wanachama wenzangu tupo kwa wingi sana katika mtandao huu ni vizuri niseme tena suala la ujenzi wa barabara unaoendelea hapa Dodoma. Mkikumbuka nilisema kuhusu ujenzi usiokidhi uliofanywa miezi kama mitatu hivi iliyopita. Barabara zote sasa hivi ni makorongo. Ni jambo la ajabu sana, wapo walionijibu kwa kashfa.
  Hivi leo kuna barabara ya area C ambayo inafanyiwa ukarabati. Mifereji inayochimbwa inahuzunisha. Kweli wana CCM wenzangu tumeshindwa kuisimamia serikali. Piteni barabara ya Hombolo hapo area C mtajionea. Hivi kwa uchimbaji huu kweli kuna malipo yatafanywa kwa kampuni hii au ni volunteers tu hawa. Hivi kweli tunajali fedha za wananchi. Where is the value of money? Where are we going? Do we want to kill these people. Who will then pay the tax? Lazima tumwogope Mungu.
  Nina hakika viongozi wangu ni wasikivu mtalifanyia kazi hili.
  Hata hivyo nimeandika barua mara nyingi sana kwa mkurugenzi na kwa kweli sijawahi pata jibu. Nawahakikishieni, kama hii bara bara haitarekebishwa, nitaondoka rasmi katika chama, na nina hakika nitaanguka na kundi la watu and one day you will pay for that.
   
 19. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Usiwe kibaraka wa Chadema, masuala ya CCM yanamalizwa kiofisi, njoo makao makuu ya chama chetu KIPENZI CHA WATANZANIA, utoe dukuduku lako na utekelezaji utafuata. Hao Chadema wamekalia majungu tu
   
 20. M

  Mwafrika Halisi Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mwnccm haruhusiwi kujikosoa? huwezi kupendelea kila uchafu mwisho wake majuto
   
Loading...